Je, ni vita vya wanandugu? Israel v. Palestina

ASUMWISYE EDWARD

New Member
Oct 14, 2023
1
2
Toka nikiwa mdogo katika vita ambavyo masikio yangu yamesikia kwa muda mrefu ni vita vya Israel na Palestina. Sina hakika lakini nadhani ni vita ambayo inapigana mara kwa mara. Kipindi kile hakuna mitandao ya kijamii ni radio tu na magazeti. Nilikuwa nikimsikia Samadu Hassan akiitangaza vita hii kwa umahiri kabisa kana kwamba anatangaza jambo la kufurahisha, Florence Dyauli, David Wakati, Abdul Wajih Sheh pia na sauti moja maarufu idhaa ya Kiswahili ya radio Deutsche Welle (Oumilkheir Hamidou). Sikujua wanapigania nini? Nilikuwa nasikia tu makombola yanarusha kutoka upande mmoja kwenda mwingine. Maeneo ambayo nilikuwa nikiyasikia ni Ukanda wa Gaza, ukingo wa magharibi mwa mto Jordani na Jerusalem pia.

Umri unakwenda, tunakua na vile vile tunapata shauku ya kutaka kujua vitu kiundani Zaidi. NINI CHANZO CHA HII VITA? HAIISHI? KAMA ITAISHA ITAISHA LINI?

Wengi wanajiuliza maswali hayo bila majibu. Kuna watu wanahusisha hii vita na mambo ya kiuchumi, wengine wanasema wanapigania ardhi na wengine wanasema ni vita ya kiimani kama Alpha Blondly Alivyosisitiza Amani na upatano wa kidini katika kibao chake cha reggae alichokiimba kwa Zaidi ya lugha tatu, YERUSALEM alichokiachia mwaka 1986.

Ili kujua asili ya vita hii ni muhimu kurudi zamani karne ya 18 KK aliyopita. Na hapa tutamzungumzia Baba wa Imani, Abrahamu na uhusika wake katika hili sekeseke la ndugu zetu.

ABRAHAM ALIZALIWA WAPI? (ENEO LA SASA LA DUNIA)

Mahali halisi alipozaliwa Abrahamu ni somo la mjadala wa kihistoria na kiakiolojia, kwani linatokana na masimulizi ya kale ambayo yanaanzia maelfu ya miaka. Kulingana na Biblia, ambayo ni mojawapo ya vyanzo vya msingi vya habari kuhusu Abrahamu, alizaliwa katika sehemu inayojulikana kuwa Uru ya Wakaldayo.

Uru ya Wakaldayo inaaminika kuwa jiji la kale katika eneo ambalo sasa ni kusini mwa Iraq. Tovuti ya kiakiolojia ya Uru, inayojulikana kama Tell el-Muqayyar, inachukuliwa na wengi kuwa eneo linalowezekana la jiji hili la zamani. Ni tovuti inayojulikana sana ya kiakiolojia ambayo imefunua mitazamo na mdokezo katika historia ya eneo hilo na watu walioishi huko wakati wa Ibrahimu.

Mahali alipozaliwa Ibrahimu kuna umuhimu mkubwa katika dini za Ibrahimu (Uyahudi, Ukristo, na Uislamu), kwani anachukuliwa kuwa mtu mkuu katika historia ya imani ya Mungu mmoja (Monotheism) na agano na Mungu. Ingawa eneo kamili halijulikani kwa uhakika, Uru iliyo kusini mwa Iraq inahusishwa sana na mahali alipozaliwa kulingana na akaunti za kihistoria na za Biblia.



WATOTO WA ABRAHAM

Kulingana na Biblia ya Kiebrania (Agano la Kale) na mapokeo ya Kiislamu, Ibrahimu/Abraham alikuwa na wana kadhaa wa wake au masuria tofauti. Wana wawili mashuhuri zaidi wa Ibrahimu ni:

Ishmaeli (Ismail): Ishmaeli alikuwa mwana wa Ibrahimu na mjakazi wa mkewe, Hajiri binti kutoka Misri. Alizaliwa Abrahamu akiwa na miaka 86. Anachukuliwa kuwa baba wa watu wa Kiarabu. Katika utamaduni wa Kiislamu, Ishmaeli ni nabii, na inaaminika kwamba Mungu alimbariki yeye na mama yake walipokuwa nyikani. Ni muhimu sana kukumbuka kuwa Ismail ana asili ya Misri, hii itakusaidia kuelewa vizuri hapo baadae.

Isaka (Ishaq): Isaka alikuwa mwana wa Ibrahimu na mkewe Sara, ambaye mwanzoni alikuwa tasa. Alizaliwa Abrahamu akiwa na miaka 100. Isaka anachukuliwa kuwa nabii katika mila za Kiyahudi na Kiislamu. Yeye ni mtu muhimu katika dini za Ibrahimu na anaonekana kama baba wa Waisraeli (katika mapokeo ya Kiyahudi) na babu wa manabii.

Jambo la msingi kulikumbuka hapa ni kuwa wakati haom watoto wa Abraham wanazaliwa, Abrahamu tayari alikuwa anaishi nchi ya Kaanani kwa Zaidi ya miaka kumi ( MWANZO 16:03) . Hivyo basi ni muhimu kutambua kuwa Ismail na Isaka walizaliwa Kanaani lakini maeneo tofauti, Kulingana na Biblia, Ishmaeli alizaliwa katika nyika ya Beer-sheba, katika eneo ambalo sasa linaitwa Israeli. Isaka alizaliwa huko Hebroni, unaojulikana pia kama Mamre. Mji huu uko katika Ukingo wa Magharibi (West Bank), ambao kwa sasa ni eneo linalozozaniwa kati ya Israel na Palestina.

Machapisho, maandiko na Makala mbalimbali zinaelezea sehemu tofauti tofauti kuhusu sehemu ambazo Ismail na Isaka walizaliwa. Lakini kwa mujibu wa Biblia na maandiko mengi yamesema kuwa Ismail na Isaka walizaliwa sehemu tajwa hapo juu.



KANAANI NI WAPI?

Turudi nyuma kidogo, Abrahamu alipokuwa na umri wa miaka 75 kipindi hicho akiitwa Abramu alifanya agano na Mungu. Lilikuwa ni agano la kubarikiwa wakati huo Abrahamu alikuwa akiishi Harani. Harani inaaminika kuwa iko karibu na mpaka kati ya Uturuki ya kisasa na Syria ya sasa. Kwahiyo hapa Harani Abrahamu aliondoka na mkewe Sara pamoja na motto wa kaka yake Lutu. Ilikuwa ni sehemu ya agano na Mungu kuwa aondoke hapa na kwenda nchi ambayo Mungu atampa. Akiwa safarini kama alivyoagizwa na Mungu, Abrahamu alipita Shekemu, sehemu ambayo alikuwa inakaliwa na Wakanaani, hivyo basi akiwa Kanaani baada ya kujenga Madhabahu hapo Mungu akamtokea tena Abrahamu na kumuahidi kuwa ile nchi aliyopo wakati huo yani Kanaani basi atampa Abrahamu na uzao wake wote. (MWANZO 12:1-7) . Kwa kuwa kulikuwa na njaa kali sana katika hiyo nchi Abrahamu akapita hiyo nchi akaendelea na safari mpaka Misri.

Nimekupitisha kwenye hayo maandiko ili uone jinsi Mungu alivyomuahidi Abrahamu na uzao wake kuwapa Nchi ya Kanaani. Kanaani ilikuwa eneo la kale ambalo ni takriban sawa na nchi za kisasa za Israeli, Palestina, Lebanoni, Yordani, na Syria. Ilikuwa ni njia panda ya biashara na utamaduni, na ilikuwa makao ya watu mbalimbali kwa vipindi tofauti tofauti, Wakanaani( wenyeji kabla ya agano la Mungu na Abrahamu, baadaye tutakuja kuona walivyokuja kuuza nchi yao kwa Yakobo ambaye naye baadaye akaitwa Israel) Waisraeli, Wafilisti ( Hawa waliishi ukanda wa Gaza, baadae watakuja kuwa wapinzani wakubwa wa Israeli), na Wafoinike.





SASA TURUDI KWA ISAKA NA ISMAIL.

ISMAIL ALIISHI WAPI?

Kwa mujibu wa mapokeo ya Kiislamu, Ishmael (Ismail kwa Kiarabu) na mama yake Hagar (Hajara kwa Kiarabu) waliishi katika eneo la Makka, hasa katika eneo karibu na Kaaba. Hadithi ya safari ya Hajiri na Ismaili na makazi yao katika eneo la Makka ni sehemu muhimu ya mila ya Kiislamu na historia ya Kaaba.

Hadithi ya Kiislamu inasimulia kwamba baada ya kuzaliwa Ishmaeli, mama yake Hagari na yeye waliachwa katika eneo la jangwa la ukiwa la eneo ambalo lingekuwa Makka kwa amri ya nabii Ibrahim (Ibrahimu) kama tendo la utii kwa mapenzi ya Mungu. Tukio hili mara nyingi hujulikana kama "dhabihu" au "Hajiri na Ishmaeli jangwani." Makazi ya Hajiri na Ishmaeli katika eneo karibu na Kaaba ni sehemu kuu ya mila ya Kiislamu na yanaunganishwa na umuhimu wa kidini wa Makka na Hija ya kila mwaka ya Hija.

Mapokeo ya Kiislamu pia yanaeleza juu ya utoaji wa kimiujiza wa Mungu kwa Hajiri na Ismaili, pamoja na kisima cha Zamzam, ambacho kinasemekana kuwa kilichipuka ili kuwapatia maji katika jangwa kame. Eneo walilokaa, ambalo lilikuja kuwa Makka, lina umuhimu mkubwa katika Uislamu, likitumika kama eneo la Kaaba na patakatifu patakatifu katika dini.

Hadithi ya Hajiri na Ishmaeli huko Makka ni sehemu muhimu ya ufahamu wa Kiislamu wa umuhimu wa kidini wa jiji hilo na hukumbukwa na mahujaji wakati wa Hajj.

Sara ndiye aliyependeza kufukuzwa kwa Ismail na mama yake, Abrahamu hakupenda suala la kumfukuza mtoto wake na mama yake, alikubali kwa shingo upande. Japo baadae alikuja kukubali baada ya Mungu kumwambia Abrahamu amsikilize mkewe. (MWANZO 21:9-21)

Hivyo basi Ismail aliishi Saudi Arabia.

Mungu alimuahidi Abrahamu kuwa atamfanya Ismail Taifa Kubwa.



Je ni taifa gani hilo?



Itaendelea.



By Asumwisye Edward
 
Kwa dunia ya Leo haya mapokeo hayana uwezo wa kuleta suluhu.Inatakiwa kuanzia Azimio Namba 181 la 1947 la UN.Kama itabidi ku adjust mipaka iliyochorwa wakati huo ni Bora ili kumaliza mgogoro.Kuendelea kushikilia misimamo na mapokeo ya miaka maelfu na maelfu ambayo huenda si sahihi,tatizo hili litdumu milele.
 
Back
Top Bottom