Je ni sahihi kumuosha mzazi wako anapopatwa na magonjwa au kuzeeka

Ndio ni jambo sahihi na ni jambo jema kwa wazazi wako......na Mungu atakubariki Sana.......

Wewe ndio wa kuficha aibu za wazazi wako kwa kuwa aibu zao ni aibu zako

Tumeagizwa baada ya kumuabudu Mungu tuwatendee wema wazazi wetu.........

Na hapo ndipo ulipo mtihani kwa vijana wengi kupata radhi za wazazi.......
 
Ni swali ambalo nimekuwa nikiliwaza Sana.Hivi ni kweli mzazi (Baba au Mama) anapopatwa na majanga kama vile kupooza mwili, Magonjwa ambayo inampasa kusaidiwa au umri wake kwenda na kushindwa kujihudumia, je ni sahihi kuchukua hatua kama mtoto kumsaidia katika mambo kama vile;Kumuogesha, Kumsaidia anapoenda msalani, Kumvalisha nguo.

Pia Kuna uhalali wowote wa mtoto kumfulia mzazi wake nguo za ndani pindi umri wake unapoenda na hawezi kujitunza?

Kama mtoto ni mwanaume je ataruhusiwa kufua nguo za ndani za mama yake aliyezeeka?

Au ataruhusiwa kufua nguo za ndani za Baba yake aliyezeeka?

Kama mtoto ni mwanamke je ataruhusiwa kufua nguo za ndani za Baba yake aliyezeeka ?

Au ataruhusiwa kufua nguo za ndani za Mama yake aliyezeeka?

Je Kuna uhalali wowote Mtoto anaposhuhudia nguo za ndani wazazi wake(Mama au Baba)zimeanikwa kwenye kwamba wazi wazi?

Je pale ambapo mtoto yupo nyumbani na Mama au Baba yake walianika nguo za ndani nje wazi wazi alafu mvua ikataka kunyesha mtoto akakimbilia kuzianua, unaporudi nyumbani kama mzazi kukuta nguo zako za ndani zimeanuliwa na watoto unajiskiaje?
Sasa shida iko wapi mkuu
 
Kama mtoto ni mwanaume je ataruhusiwa kufua nguo za ndani za mama yake aliyezeeka?
na mimi nakuuliza swali lenye maudhui kama hayo;

Je ni sahihi single father kumuogesha mtoto wake wa kike?

Ukipata jibu hapa, basi utakuwa umeshapata jawabu la hilo swali lako.
 
Back
Top Bottom