Je ni nani Mzalendo wa kweli: Zitto, Pinda, JK au Lipumba?

Josh Michael

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,523
77
Kwa karibu siku kadhaa sasa nilikuwa najiuliza maswali kwamba labda Tanzania tupate kiongozi aliye mzalendo wa kweli mwenye hulka za kijamaa kidogo.. Lakini katika mawazo yangu nimekuwa najiuliza kuwa Tanzania tumeingia kwenye mfumo wa Soko huria bila kufuata misingi yake.

Kwa Kipindi cha miaka 20 iliyopita Tanzania tumekuwa tunafuata Free market na demokrasia ya vyama vingi, lakini katika kipindi hicho tumeshuhudia Taifa Letu likigeuzwa kuwa sehemu ya watu wachache na wageni kufaidi zaidi kuliko wengine na wananchi wa Tanzania, Je katika hatua tuliyofikia ni nani aliye mzalendo wa kweli na wa kupenda Taifa lake yaani mwenye mawazo ya uzalendo Zaidi Je ni Mheshimiwa Zitto Dr Slaa, au Pinda, Rais wetu Kikwete Je ni nani ambaye tunaweza kufuata mawazo yake??
 
Last edited:
Uzalendo is an illusion, to be pursued but never attained, kwa hiyo basi, hamna mzalendo wa kweli katika wote.

Labda unakusudia mzalendo zaidi?
 
Piga chini JK na Pinda.

Dr. Slaa anauzalendo, I mean anafanya vitu toka moyoni, anaweza akaona mwanafunzi kaonewa na konda, atafanya juu chini afuatilie ishu.

vs
Zitto ana uzalendo kwa style yake, far more than any of those above. Anataka kutumia mabavu ili mradi haki ipatikane! angekuwa na uwezo(silaha) angefanya yasiyotarajiwa. Huyu kama angekuwa kwenye chama kizuri na system nzuri basi tungetengeneza another Raila,Morgan Tsvangirai.... etc.

Uzalendo wake unaendana na umri wake wa kutaka kufanya kila kitu kwa wakati mmoja. His is best I think.
 
Ni kweli Kabisa labda tuanze kutengeneza Viongozi wazalendo kwa Taifa letu kwa sasa ndio maana wanaweza kutumika katika kujenga Taifa lenye nguvu sana katika Dunia kwa kuona rasilimali za watu zinatumika katika watu wote
 
Dr Slaa ni kiboko yao hakuna Kabwe wala Pinda hapa wala JK wao wote hamna anayemuweza huyo dr wa CHADEMA. Ni mkali sana kiuwezo wa kufuatilia mambo yuko makini sana na kazi yake,tena atapendeza sana kama chama chake kitamsimamisha agombee urais katika uchaguzi ujao watanzania wengi wanaonyesha kuwa na imani naye sana.

Hawa wengine kina Kabwe ni kundi hilo hilo la akina Jk,j. Mashaka watu wenye uchu wa madaraka na uroho wa kujilimbikizia mali kila siku bila hata kujali raia wako katika hali gani,nasikia tena huyo John Mashaka yuko mbioni kugombania urais mwaka 2015 nafikiri anaota sana kwani hatutofanya makosa tena ka ya kumchagua JK na kumpatia madaraka kama ya uraisi, huyo J. Mashaka anajifanya kuwa yeye ni investiment banker ndio atakuja kuibinafsisha nchi yote mpaka urais utachukuliwa na jews na watu wa Wall street ataweza kutuletea night mares mbaya sana ka tutampa madaraka anayoyakusudia. Nasikia hivi sasa yuko nchini keshaanza kufanya campaign ndani ya chama tawala. Atakutana na kupambana na wabunge machachari ka akina Lucas Seleli Lumambo wa ccm Nzega , huyo naye ni mzalendo sana mwenye uchungu na nchi yake.

Baba Manka.
Peace!
 
Kwa karibu siku kadhaa sasa nilikuwa najiuliza maswali kwamba labda Tanzania tupate kiongozi aliye mzalendo wa kweli mwenye hulka za kijamaa kidogo.. Lakini katika mawazo yangu nimekuwa najiuliza kuwa Tanzania tumeingia kwenye mfumo wa Soko huria bila kufuata misingi yake.

Kwa Kipindi cha miaka 20 iliyopita Tanzania tumekuwa tunafuata Free market na demokrasia ya vyama vingi, lakini katika kipindi hicho tumeshuhudia Taifa Letu likigeuzwa kuwa sehemu ya watu wachache na wageni kufaidi zaidi kuliko wengine na wananchi wa Tanzania, Je katika hatua tuliyofikia ni nani aliye mzalendo wa kweli na wa kupenda Taifa lake yaani mwenye mawazo ya uzalendo Zaidi Je ni Mheshimiwa Zitto Dr Slaa, au Pinda, Rais wetu Kikwete Je ni nani ambaye tunaweza kufuata mawazo yake??

Hili swali sio rahisi kama linavyosomeka .... ni vigumu kupambanua!!Kama tunatumia mawazo yao pekee kupima uzalendo wengi tutaamua kwa kufuata ushabiki. Tunataka mzalendo wa kweli ambae anaweza akaanzisha kitu kikaonekana .... Hata hao tunaowataja na kuwakubali hapa ni kwamba wanakosoa tu (japo sio vibaya) hawaji na mawazo yao... yaani wao kama wao!!So at the end of the day tunagundua kuna asilimia za uchama,ushabiki na umaarufu tu!!

Ni mtazamo tu!!
 
klwa zito labda hapo nyuma kabla hajashika fedha alikuwa na uzalendo ila kwa sasa anakimbilia matawi yanayomeremeta kama ya mafisadi ambaye anauzalendo wa kweli ni Dr Slaa akifuatiwa na Pinda
 
Wakuu, kaswali haka ni kepesi sana kwa mtizamo wa harakaharaka. Lakini ukifanya detailed trend analysis unagundua kuwa si kepesi kujibu. Hata hivyo sipendi kura yangu iharibike. Kwa hao aliowataja mkuu JojiPoji, kura yangu nampa Mh.... Nicheme au nichicheme? Slaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
 
Hili swali sio rahisi kama linavyosomeka .... ni vigumu kupambanua!!Kama tunatumia mawazo yao pekee kupima uzalendo wengi tutaamua kwa kufuata ushabiki. Tunataka mzalendo wa kweli ambae anaweza akaanzisha kitu kikaonekana .... Hata hao tunaowataja na kuwakubali hapa ni kwamba wanakosoa tu (japo sio vibaya) hawaji na mawazo yao... yaani wao kama wao!!So at the end of the day tunagundua kuna asilimia za uchama,ushabiki na umaarufu tu!!

Ni mtazamo tu!!
Kwa suala la uzalendo nafikri yatupasa tuupime kwa vitendo na si kwa kuongea na kukosoa sana serikari wanakofanya wabunge wetu wawapo bungeni, sababu wanacho tetea bungeni wanaogopa kukitetea katika vikao vya NEC, hilo ni la wabunge ukija Rais wetu ndo sijui niuweke kwenye kundi gani! nasema hivyo kwasababu hajui kukemea, hajui kuonya na wala hana sauti na nguvu ya kutetea wananchi wake pamoja vyeo tulivyompa in short ni muoga wa kundi fulani la watu. Yote kwa yote naweza sema bado hatujapata mzalendo wakweli anayeweza kutetea wananchi wake kama hayati SOKOINE na Mwl. Nyerere.
 
Mawazo yao ni yepi hayo? Yana tofauti gani? Yabainishe tufanye uamuzi/uchaguzi sahihi!
Mawazo Dhabiti kwa Taifa hili yenye kufanya mambo magumu sana na kuona kuwa yale ambayo anasimamia na kufanya katika Tanzania na kupewa msukumo mkubwa. Kumbuka wakati wa Mwalimu Nyerere aliweza kuunganisha Taifa Hili kwa mawazo yake, Lakini Leo hakuna hata kiongozi mwenye kudhibiti hali yoyote ile , Tazama hata kule Zanzibar utaweza kuona hali kama hiyo, Hakuna Kauli hata ya Rais kuzungumzia hali hii. Haya ndio mambo magumu sana
 
This is an illusion hakuna mzalendo wa kweli nchi hii si hao ulowataja tu bali hata mimi na wewe.
 
This is an illusion hakuna mzalendo wa kweli nchi hii si hao ulowataja tu bali hata mimi na wewe.
Kama basi hakuna hapa MZalendo wa kweli basi ni Mwanakijiji ndiye wa kweli maana wewe huna mtu wala mtu unayefungamana mawazo na wewe
 
Mizengo Pinda- ingawa kazungukwa na wachafu.
Dr.Slaa anfuatia,then Zitto ingawa nae kwa wadada ndio mwisho.
Lipumba na Jk Sio wazalendo halisi-mambo machafu awakemei- nawasirisha.
 
Mizengo Pinda- ingawa kazungukwa na wachafu.
Dr.Slaa anfuatia,then Zitto ingawa nae kwa wadada ndio mwisho.
Lipumba na Jk Sio wazalendo halisi-mambo machafu awakemei- nawasirisha.
Naweza kusema kuwa Mzee MWanakijii ndiye mzalendo wa kweli na yeye anapigana akiwa karibu na mbali sana. I know it man kuwa Dr.Slaa na wanachama wote wa Chadema???
 
Back
Top Bottom