Papa D
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 753
- 182
Bara la Afrika limekuwa likikumbwa na matatizo yanayofanana mfano: angalia Uchaguzi wa Tanzania, Ivory coast, Zimbabwe, Kenya, Sudan na kwingine. imefika wakati baadhi ya watu wanajiaminisha kwamba hali hii inatokea kwa sababu Waafrika wenye akili, nguvu na mawazo ya kimapinduzi walichukuliwa utumwani. waliobaki walikuwa waoga na wenye uwezo mdogo kiakili na wachache wenye vinasaba vya akili walobaki wanaonekana mbele ya Wenzeo kama Waleta vurugu, wagomvi na vibaraka wa wazungu. Je, kuna ukweli wowote katika hili? kama kuna ukweli, tufanyeje? kama hakuna ukweli je, mfumo mbovu wa maisha tulonao ni stahiki yetu?