Je, ni kweli Mwalimu Nyerere alitumia mizizi ya Makobo kuwashawishi watu?

Gxcsed

New Member
Nov 22, 2021
1
0
Majuzi nilikuwa kijijini kwetu!

Lengo kuu la safari yangu lilikuwa kuwasalimia ndugu na jamaaa, maana ni miaka mingi sana imepita toka nikanyage bush kwetu.Lakini nilipofika killage yalizuka mambo mengine ambayo sikuwahi kuyasikia wala kuyaota. Na moja ya mambo hayo yanamuhusu baba wa taifa hili, mwalimu Julius kambarage nyerere.

Ilikuwa hivi, baada ya kuwasalimia ndugu na jamaa, wazee wa pale kijjini waliita kikao cha gafla na kunitaka nihudhurie. Hili jambo lilikuwa geni kwangu, na kwa kiasi Fulani niliogopa. Moyoni sikuwa najua ni kitu gani wanataka kwangu.

Baada ya kufikiria sana niliamua niondoke kimya kimya bila ya kwenda kwenye kikao, maana wazee wengi ambao niliambwa watakuwa kwenye kikao walikuwa wanaogopeka sana pale kijijini kwa uchawi, Hivyo sikutaka kabisa mazoea nao. Basi bana kimya kimya nilipanga mipango ya kuondoka pasipokushtukiwa.

Lakini bahati mbaya nikiwa hatua za mwisho, babu yangu alifika chumbani kwangu bila ya mimi kutarajia. Aliponiona tu, alijua nimejaa hofu na woga, Kwa sekunde kadhaa alinitazama kisha akaniamba maneno yaliyonipa ujasiri. Aliniambia kamwe hawezi kuruhusu jambo baya linipate, hivyo niwe na amani na niende kwenye kikao.

Maneno yake yalinipa nguvu, na kwa ujasiri wote nilienda kwenye kikao.Tofauti na nilivyotegemea kwamba kuna jambo labda nimewakosea, haikuwa hivyo, Badala yake wale wazeee walinieleza matatizo mengi yanayowasumbua wao na kijiji chao, walinieleza jinsi wanavyoumia kuona vijiji vingine vinaendelea lakini kile bado kipo vile vile, na mwisho walinitaka nigombee udiwani ili niweze kuleta maendeleo pale kijiji na kwenye kata kwa ujumla.

Ombi lao lilikuwa nzito kwangu, nililikataa. Na niliwaeleza sababu mbili kuu, moja sina ushawishi wa kisiasa. Niliwaeleza sina Uwezo wa kuongea na watu wakaniamini na kunifata, na mbli niliwaeleza sikuwa na mpango wa kuishi pale, maana tayar nlikuwa na biashara zangu mjini.

Kupitia hoja hizo nilijua nitachomoka, lakini haikuwa hivyo, wazee walinieleza mimi kuishi mjini sio shida. Niishi popote nitakapo, ila wao wanataka niwe diwani wao, na mbili kuhusu kutokuwa na uwezo wa kuongea mbele za watu na kuwashawishi, waliniamba watanipa mizizi ya makobo. Waliniambia mizizi hii ikichanganywa na dawa Fulani halafu mtu akatafuna inamfanya akubalike sana hata kama anaongea pumba.

Waliniambia hata mwalimu nyerere katika harakati za uhuru alipewa mizizi ya makobo ili kuongeza ushawishi wake na ndio mana alikubalika sana. Sasa wakuu nimekuja kwenu, najua jf limejaaa wajuzi wa mengi.

Naomba wale wenye kujua waniambie, ni kweli mwalimu nyerere alikuwa anatumia mizizi ya makobo? Umewahi kusikia au kusoma sehemu kuhusu mizizi ya makobo?

Kwa wale wanasiasa wakubwa na wenye ushawishi, najua mpo humu ndani/ je mnatuma mizizi ya makobo ili mkubalike?
 
Back
Top Bottom