Je, ni haki kuchoma picha za Mpenzi wako wa zamani na kumtangaza kwa mabaya?

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Habari yenu wakuu,

Hivi kuchoma moto picha za mpenzi wa zamani ikiwemo kuchoma cards na zawadi mbalimbali, kudelete jina kwenye simu, kumunfriend kwenye mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na kumblock, kumtangazia sifa mbaya yaani kila baya ni lake, je ina tija?

Mimi naona sio Vizuri, inakua ni Mihemko tu. Inakuaje mtu unasahau mazuri yote Mliyotendeana mlipokua wapenzi hadi mfikie hatua hiyo? Kitendo kama hicho ndo nasema ni mkono wa shetani unakua unatenda kazi.


Kwa mfano mimi sijui kuacha au kumchukia kupita kiasi aliyekua Mpenzi wangu, hua naendelea kumheshimu na kumthamini kama binadamu yoyote yule. Unakuta mpenzi wako mmesaidiana katika shida na raha lakini mwisho wa siku mnapishana kama manyani..duh! hainiingii akilini.

Ipo ile kuonesha kuchukia au kuchukizwa na kitendo fulani, hiyo ni sawa. Na unaweza kukaa kwa muda ili hasira ziishe lakini sio kujivisha roho mbaya ya shetani na kuanza kukomoana sijui unaanza kusambaza picha mlizopiga wakati mlipokua wapenzi mkiwa kwenye furaha ya mahaba ya dhati sio Vizuri. Mkikutana uzeeni mtaoneana aibu. Tenda mema utakutana na neema mbele ya safari.

Mimi labda nipo tofauti na wengine, Hivi mkikorofishana na Mpenzi wako haummiss kabisa? Mwenzenu hata kama kaniudhi vipi naendelea kummiss hadi nakonda sema najikaza tu. Vipi wewe mwenzangu.

Naombeni experience ya haya mambo, Je wewe unayachukuliaje?

Nawapenda sana ndugu zangu wanajamiiforums. Mia
 
sio vizuri kumtangaza mabaya yake (ingawa kuna wachache wanaouliza sababu za kuachana)
...ila hapo kwenye picha...mmmmh! sidhani kama mpenzi wako mpya atavumilia
kuona picha za EX wako hata kama ana roho ya malaika..
----
However kama kila unapokua na mpenz unahifadhi picha (hasa wale wanaobadili kila kukicha)
hope utakua na PICTURE LIBRARY ya maana kama MAKUMBUSHO ya taifa
 
Aiusuu kuchoma picha na kumnunia. Wee songa mbele mkikutana salam haigombii akili kichwani kwako. Baya 1 uharibu mazuri 99 lkn asume wewe ufanyiwe hayo. Mie nakiburi saana ila kuna ntu na ntuuu aisee....
 
sio vizuri kumtangaza mabaya yake (ingawa kuna wachache wanaouliza sababu za kuachana)
...ila hapo kwenye picha...mmmmh! sidhani kama mpenzi wako mpya atavumilia
kuona picha za EX wako hata kama ana roho ya malaika..
----
However kama kila unapokua na mpenz unahifadhi picha (hasa wale wanaobadili kila kukicha)
hope utakua na PICTURE LIBRARY ya maana kama MAKUMBUSHO ya taifa

Sasa si unamuambia ukweli mpenzi wako? Akikataa mrudishie mwenye picha au unaonaje?. Mia
 
Hali iyo inategemea mmeachana kwa staili gani km mmeachana kwa ugomvi na dhaura lazima mchukiane.

Asilimia kubwa ya wanaoachana huwa wanakorofishana. Kumbuka hasira hasara. Itafika kipindi unataka hata msaada utaukosa. Mia
 
mi tukiachana kama ulinipa tshirt ntashukuru nimepata dekio jipya ila sijui picha na vinginevyo vyoooote nachoma moto. akishaitwa x, hakuna haja ya memories... kila mtu ashike 50 zake. nawashangaaga sana wanaoachana na baadae wanapeana game la ukumbusho.. aaagggghhhrr wananikera basi tu kila mtu na maamuzi yake
 
Inategemea mmeachana kwa sababu gani, za msingi au zisizo za msingi.Kama mmeachana kwa mabaya mara nyingi mtapenda kuoneshana ubabe ikiwa ni pamoja na kunyang'anyana zawadi tangible mlizopeana,kuchomeana picha,kusemana kwa mabaya na jambo moja baya kusambaza picha za uchi au video zenu za faragha.

Binafsi mimi sina tabia hizo za kishenzi maana najiheshimu sana ila kuna mijitu mingine bhana sijui inakuwaga na akili kama ndezi mpaka kufikia kufanya mambo ya ajabu.
 
tumeshaachana picha nazitunza za nini? tupa kuleeee hata salamu yake sitaki itakuwa ya unafiki tu
nadelete kila kituuuuuuuu kwendaaaaaaaaaaaaa mwana kwenda
 
Kutukana,kutangaziana mabaya,kupigana vikumbo njiani,au kuombeana mabaya ni dalili ya kutojiamini na kupoteza matumaini.

Picha/kadi-choma,hazina nafasi tena wala kazi kwenye maisha yako,bali kuendelea kukuumiza,na ni hatari zikikutwa na mpenzi wa sasa mwenye akili kama zangu.

Namba-futa hazina kazi tena labda kama mlibahatika kupata katoto,at least una sababu ya uzito kumueleza mwenzio kuwa unazo kwa case ya mtoto.

Mitandao ya kijamii-hii haina uzito kwa ambao wameamua kuishi pamoja maana hata facebook yenyewe kuingia ni ishu.mambo mengi mnawaza pango ,usafir,ndoa lini....fb,insta,viber ect,kupiga piga picha za makalio na kulike achia watoto.
Unaweza block yeye au hata acc nzima au ukaacha pia,acc ikawa ipo ipo tu kumaanisha sasa umekua.

Sent from my radio
 
Mkuu figganigga..
Haya mambo mara nyingi yanaendana na hasira za kudanganywa.. Na haswa watoto wa kike wanapoona wamekuwa betrayed by their loved ones.. Asilimia kubwa ya wanaofanya haya ni wale wenye mahaba mazito.. Kuchoma picha na zagazaga nyingine kwake ni sehemu ya kujaribu kupunguza maumivu.. Baadae huwa ni majuto na huwa wanakuwa tayari kwa usuluhishi.. Ubaya utazidi pale usuluhishi utakaposhindikana kwa kuwa tu mwanaume umeamua ku-move on.. Mwanaume atakuwa amejitengenezea a permanent enemy..
Wanaume tunatakiwa tuyajue haya yote na kuyaelewa kwa sababu sie ndo tunaokuwa (mara nyingi) chanzo cha haya..
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom