Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 32,427
- 34,247
Kuna taarifa kutoka Turkiye kwamba Kampuni ya Yapi Merkezi huenda imefilisika na Kushindwa kutimiza wajibu wake wa kujenga na kukamilisha mradi wa reli kama ilivyotarajiwa hivyo kuilazimisha Serikali ya Tanzania kutafuta plan B ya kupata pesa Ili kujenga mradi wa reli ya Sgr.
Ikumbukwe waliowaleta Yapi Mwekezaji walikuja Kwa mbwembwe kwamba huyu ni mkandarasi wa viwango ambae anajenga Sgr yetu ya viwangi vya Juu Kwa bei chee yaani cheap.
Je kusua sua Kwa ujenzi ni matokeo ya mkandarasi kutokuwa na uwezo kama tulivyoambiwa ama? Ikumbukwe siku za hivi karibuni Wafanyakazi wa kampuni hii ya mchongo waligoma kufanya kazi Kwa sababu wamekaa zaidi ya miezi 4 bila kulipwa.
View: https://twitter.com/The_EastAfrican/status/1708741101954457728?t=iW9CZMs2cqFcvpDmSaDjcQ&s=19
Swali.
Je Ile Kauli ya Cheap is Expensive kudhihirika Kupitia Mkandarasi huyu wa Kituruki? Tusipende vya Bure mara nyingi vina gharama.
Wafanyakazi wa kampuni ya Yapi Merkezi kwenye ujenzi wa SGR wagoma kufanya kazi kutokana na Madai ya kutokulipwa kwa miezi 7
Takriban wafanyakazi 2,000 wa Uturuki walioajiriwa na kampuni ya ujenzi ya Uturuki ya Yapı Merkezi katika mradi wa reli nchini Tanzania wamegoma tangu Agosti 5, wakidai kulipwa mishahara yao ambayo hawajalipwa kwa muda wa miezi saba iliyopita. Katika siku ya saba ya mgomo wao (Agosti 11)...www.jamiiforums.com
Kwahiyo watarudi kwao wakiwa wamejitwisha mikono kichwani
Lakini si ndiyo hawa tuliwasaidia majuzi walipokumbwa na matetemeko!!