Je mifuko inayosemekana ni mbadala wa ile ya plastic ni rafiki kwa mazingira?

KITEKSORO

JF-Expert Member
Sep 25, 2012
346
425
Wakuu jukwaani humu naamini wote tumeshuhudia marufuku ya mifuko ya plastic na tunaiona mifuko iliyotapakaa madukani, sokoni nk ambayo inasemekana ni mbadala wa ile ya plastic. Je kuna uthibitisho wowote kitaalamu kuwa mifuko hii mipya ni rafiki kwa mazingira? Kila nikiiangalia napata wasiwasi kuwa nayo siyo biodegredable!! Tuelimishane wadau.
 
Attachments

  • 15596724885717006624543059548994.jpg
    15596724885717006624543059548994.jpg
    155.7 KB · Views: 17
Unaweza kufanya utafiti.
Fukia na mwagia maji. Then angalia baada ya siku kama 5 au 7 kama umeoza.
Utaleta majibu
 
Wakuu jukwaani humu naamini wote tumeshuhudia marufuku ya mifuko ya plastic na tunaiona mifuko iliyotapakaa madukani, sokoni nk ambayo inasemekana ni mbadala wa ile ya plastic. Je kuna uthibitisho wowote kitaalamu kuwa mifuko hii mipya ni rafiki kwa mazingira? Kila nikiiangalia napata wasiwasi kuwa nayo siyo biodegredable!! Tuelimishane wadau.
Suala sio kuwa biodegradable in that case, tunachoangalia ni 'reusability', yaani huo mfuko ukiununua una uwezo wa kuutumia mara nyingi bila kuutupa, na hicho ndicho kinaangaliwa hapa.
 
Hio mifuko inaoza mapema zaidi.

Mfuko wa rambo unachukua miaka wanadai 400 ili kuteketea kabisa
 
Suala sio kuwa biodegradable in that case, tunachoangalia ni 'reusability', yaani huo mfuko ukiununua una uwezo wa kuutumia mara nyingi bila kuutupa, na hicho ndicho kinaangaliwa hapa.
[/QUOTE
Samaki wa leo leo na nyama vinadondosha uchafu kwenye vyombo vya usafiri labda walete masufuria rafiki kwa kubebea hizo bidhaa.
 
Suala sio kuwa biodegradable in that case, tunachoangalia ni 'reusability', yaani huo mfuko ukiununua una uwezo wa kuutumia mara nyingi bila kuutupa, na hicho ndicho kinaangaliwa hapa.
Mhh unaweza kuwa sahihi ila hata ukiutumia mara nyingi baadae utautupa tu. Na hiyo ya kuutumia mara nyingi nayo inaweza ikawa kwa wachache labda vijijini. Sidhani kama mijini watu watatembea na mifuko hasa ukizingatia wengi manunuzi yao ya vitu si ya kupangwa mf. mtu anaona tikitimaji ananunua , zinapita boxer ananunua ....sasa uwezekano wa kuwa na mfuko haupo muda huo.

Tujuzane hii mifuko ni material gani imetumika, je inaoza haraka, na ikioza mabaki yake ni rafiki kimazingira ?
 
Back
Top Bottom