Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 18,678
- 22,267
Habari za Dodoma Paskal, Kozi fupi Dom. ilikufundisha kuwa maoni binafsi ni uchochezi, okay safi sana.Wanabodi,
Leo taifa limetangaziwa huku tukishuhudia live kupitia matangazo ya moja kwa moja, live kupitia kwenye TV, rais akatutangazia kuwa fedha hizo ni gawio la serikali, na muda mfupi baada ya tukio hilo, Mhe. Zitto akaibuka na taarifa yake kuwa fedha hizo sio gawio, ni maduhuli.
Nimepandisha uzi huu kufuatia hoja za mwana jf huyu
Mkuu ZZK, nimezisoma hoja zako na kuzielewa ila ni za uchochezi kutaka kumfanys rais wetu aonekane muongo na tukio lile ni usanii!.
Hata kama fedha hizo ni za maduhuli na sio gawio, jee kuna tatizo gani zikiitwa gawio?!. Sote tulioangalia live, tumeshuhudia hundi za gawio zikitolewa, sasa iweje mtu tuu ajiibukie na kuita ni maduhuli?.
- Kwa sisi ambao sio wachumi, any income ni profits, hivyo chochote ambacho serikali imepata mgao wake kutokana na income ya taasisi zake hivyo ni sahihi kabisa kuita gawio la mapato yao!.
- Maana ya gawio ni mgao na sio lazima dividends.
- Faida ni fedha yoyote unayoipata extra, hivyo kwa mgao huo, serikali imepata faida.
- Sii ulaghai, bali huo ndio ukweli wenyewe, gawio hilo ni faida kwa serikali.
- Hata kama hakuna faida, then gawio hilo ni mgao halali wa 15% ya serikali.
- Maadamu yameishawekwa kisheria, neno gawio hapa linamaanisha kile unachogawa, iwe ni mchango, mgawo, gawio, call it what you may, serikali imegaiwa, hivyo kilichopokelewa ni gawio la mgao wa serikali.
- Amewaleta ili Watanzania tuone, jinsi serikali yetu inavyofanya kazi, na amini usiamini, kuanzia mwaka huu wa fedha, kutakuwa na tukio la TRA kwa walipa kodi wakubwa nao pia watatangazwa na vyeti vya recognition wapewe!.
- Zitto usipotoshe, Watanzania hatuja danganywa, zile hundi ni za ukweli, ni gawio halali kwa serikali yetu na fedha hizo zote zimeingia mfuko mkuu hazina na nchi imepata pesa!.
Nauliza jee mnaonaje tukishauri Mhe. Zitto akamatwe na kushitakiwa kwa uchochezi wa kumdhalilisha rais wa JMT na kuidhalilisha taasisi ya urais?.
Rais wa nchi ni kama baba kwenye familia, sio mtu, huyu ni an institution, na kwa mujibu wa katiba yetu, rais wetu hawezi kukosea ndio maana hashitakiwi. Hata kama Zitto ni mkweli na hayo ni maduhuli na sio gawio, kama rais kasema ni gawio, then ni gawio!. The boss is always right!.
Haiwezekani rais wetu aseme kitu hiki halafu atokee mtu mwingine, ambishie rais!. Huu ni utovu wa nidhamu!.
Hii sii mara ya kwanza kwa Mhe. Zitto kutoa kauli za kichochezi, tulipotangaziwa na rais wetu kuwa tumenunua ndege mpya , Zitto aliibuka na kudai ndege sio mpya, ni chakavu na kudai kuwa ni ndege za mtumba. Mimi nilishauri
Zitto Zuberi Kabwe Ni Mchochezi, Akamatwe, Ashitakiwe Kwa Uchochezi, Adai Rais Magufuli ni...
P.