Je, Mbowe amefanikiwa kutimiza lengo alilokusudia?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Kwa waliomsikiliza Mbowe jana alikuwa na malengo makuu matatu
Kwanza, kuonyesha jamii wazi kwamba Chadema walitimiza wajibu wao kama walivyoombwa na viongozi na jamii kwa ujumla kwamba wakae kwenye maridhiano na CCM kwa maslahi mapana. Ameonyesha walitekeleza lakini Chama cha Mapinduzi kimekataa maridhiano

Pili, alitaka kuliambia Taifa kwamba hakuna uchaguzi wa haki 2025 badala yake CCM wanataka kurudia mchezo wa 2020 na hivyo 4R hazina mantiki.

Tatu, chadema kama chama cha siasa baada ya kudharaulika kwa nguvu ya mazungumzo na hata maoni ya tume mbalimbali zilizounda kimeamua kurudi kwenye harakati. Hapa kuna matumizi ya dola yatakayokwamisha mahusiano ya kimataifa hivyo hoja ya kufungua nchi inakwenda kutiwa doa.

Kwa maeneo haya matatu Mbowe amefanikiwa kwa sababu tayari watu wameonekana kuandamana kwa hoja kabla hata ya maandamano ya miguu. Mjadala unaoendelea kwa kiasi kikubwa ni kama serikali imeshindwa kupangua hoja zake. Means wataanza upya kumwita kwa mazungumzo kutuliza upepo.

Kama nchi inapotokea tamko la wazi la kukiukwa kwa maridhiano siyo picha nzuri na inaleta kutokuaminiana na mwisho wa siku mashirikiano yanakwenda kuondoka baina ya wababe hawa wawili wa siasa nchini.

Mbowe ametimiza wajibu na ameibuka kidedea, je tunatokaje hapa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom