Je kwa mwanamke ndoa ndiyo kila kitu?

Thamani ya mwanamke haiongezeki wala kupungua aolewe ama asipoolewa.
Thamani ya mwanamke inapatikana siku anapozaliwa.

Ndoa ni muhimu kweli na hilo halipingiki,issue ni mafundisho yasiyo sahihi wanayopewa mabint yakiwaandaa kuwa wake na si kusimama wao kama wao. Ni kweli thamani ya mwanamke inakamilika kwa yeye kuwa na mume? Mama anapomwambia bint yake siku ya kitchen party kuwa umenitunzia heshima yangu kama mama anatuma ujumbe gani kwa bint zake ambao hawajapata wa kuwaoa?
Vipi huyo aliyeolewa ndoa yake iki fail au mume akafariki atasimama mwenyewe kama aliaminishwa mguu wake wa pili ni mume?
Wanawake wengi wanavumilia ndoa za manyanyaso kwa kuogopa jamii kuwaona hawajiheshimu kama watatoka na kuishi wenyewe!!
 
Mambo ya kuamka umekumbatia blanketi chapa simba, wakati kuna uwezekano wa kuwa na blanketi chapa mtu, lina joto kutoka kwa manufakchara, linapiga story na kukuchekesha, ya nini?

Hata kama una mihela, kuna saa unataka walau mtu wa kupanga naye, hivi lile 'orofa' la keko nilitoe msaada ama nilibonde bonde tu. Unavaa unapendezaaaa, huna hata mtu wa kukusifia tokea home, aisee mke wangu umetokelezea kinoma. Ya nini?

Umuhimu wa ndoa haupimwi kwa monetary value tu, kuna mengi zaidi ya hayo.

Lakini, usiolewe sababu unatafuta pa kufia na kuzikwa, olewa sababu unahisi huyo njagu anakufaa.
 
Zinduna wazazi wanafanya hvyo ili kujarib kufuata mising na sheria za dini na mila. unapoolewa ile dhambi ya uzinz haitakuepo unles otherwiz unapenda michepuko. pia hakuna mzazi anaependa azae nje ya ndoa na huwa wanapatwa na aibu na stress ikitokea hvy. so wana sababu za mcng ila tu madhara yake ni km hy wanawake kuwork hard kutfrta ndoa hatimae kupata ndoano badala ya ndoa. nicchokubaliana nacho mimi ni perception za watu mwanamke asipoolewa atasemwa weeeee!! mwanamke tofaut na mwanaume yy anasubiria proposal sasa zispokuja hafanyaje?
 
Last edited by a moderator:
Mi nadhani kama mtu anaweza kumudu kuishi peke yake bila kujihusisha na zinaa kabisa na moyoni mwake ameamua hivyo SIYO DHAMBI na hakika ndoa kwa mtu kama huyu sio jambo la lazima ila sitaweza kumuelewa mtu anayesema ndoa kwake sio lazima halafu wakati huo huo amejihalalishia zinaa.Cha msingi hapo ni kuchagua moja ama KUINGIA KWENYE NDOA au KUISHI PEKE YAKO BILA KUJIHUSISHA KABISA NA ZINAA,Otherwise...
 
Sio kama najaribu kujiliwaza or anything ila nachoelewa mm ndoa sio lazima. Hata kwenye bible ipo;

1 Corinthians 7:1-16
Now to the unmarried and the widows I say: It is good for them to stay unmarried, as I am. But if they cannot control themselves, they should marry, for it is better to marry than to burn with passion.

If am not mistaken hii phrase imetoka kwa apostle Paul; am not so sure kama mantiki yake ya kustay unmarried na unayoiongelea wewe zinafanana kiuhalisia.

Himself he stays unmarried and he meant it (no kids no that mchezo) mnaotaka kuiga sasa mnastay unmarried and yet u get pregancy for men they get busy making babes here and there!!

If u aint a nun/padri.... ndoa bora ni muhimu aisee labda tu oppose hapo kwamba si bora ndoa
 
Fanyeni ya kuweza kuwapa heshima kwanza na kuwawezesha kuishi dada zangu!!!!!!!
Ndoa kama itatokea well and good lakini pia ikitokea na ukawa ni wa kuteseka usikae hapo hata dakika moja eti sababu utaonekana hivi na vile ndio maana nasisitiza hayo hapo juu!!!!!!

Ndoa yapaswa kuwa na furaha kama furaha haipo basi hakika ndoa sio kila kitu!!!!!!!!

Nashukuru kuona at least kuna wanaume wako positive kiasi hiki. Wengine hapa naona wanajaribu kutuaminisha hapa kuwa bila wao heshima haiwezi kupatikana.
 
If am not mistaken hii phrase imetoka kwa apostle Paul; am not so sure kama mantiki yake ya kustay unmarried na unayoiongelea wewe zinafanana kiuhalisia.

Himself he stays unmarried and he meant it (no kids no that mchezo) mnaotaka kuiga sasa mnastay unmarried and yet u get pregancy for men they get busy making babes here and there!!

If u aint a nun/padri.... ndoa bora ni muhimu aisee labda tu oppose hapo kwamba si bora ndoa

Yes that came from Paul and no it wasn't just meant for nuns and priests. Marriage should be a personal choice and whether i decide to have babies or not that's my decision to make, not society's. Tatizo bana "ndoa" imekua so idealized to the extent that it has actually lost it's meaning. Watu wanaoa na kuolewa kutimiza wajibu not realising that marriage is a lifetime commitment to one partner and one partner alone! Sasa hebu nionyeshe couples ambazo zipo 100% faithful to their vows? I am not trying to say that people should stay unmarried but what i am saying is very simple; Do Not get married just because it is the thing to do or because you are trying to fit in the society. Get married because that is what you really want & stay committed to your partner.
 
Daaah hii thread kwa nini sikuiona tangu jana? Hongera sana mtoa mada ila nasikitika ujumbe huu haujawafikia wale haswa wanaotakiwa kufikishiwa.. Kwangu mimi siamini kuwa ndoa ndo kila kitu achilia mbali kwa mwanamke,kwa binadamu awaye yote. Hizi imani zetu za kiafrika ndio zinazosababisha watu wengi wanaingia kwenye mahusiano hatimaye ndoa na watu ambao sio sahihi simply bcoz 'umri unakwenda....' Hell...I say no...mtu aingie kwenye ndoa kwa sababu amempata wa kuingia nae kwenye ndoa na sio kwa sababu ana uhitaji wa kuingia kwenye ndoa. Ifike wakati jamii zetu zibadilike.....mtoto wa kike alelewe na aandaliwe kisaikolojia kuishi maisha ya aina zote mbili.
 
Vibibi na wenye tabia chafu ambao hawajawai tamkiwa neno NDOA vinaliwazana hapa!!
Ukweli utabaki pale pale safar ya mwanadamu aliyekamili atapitia hatua hizi
i/KUZALIWA
ii/NDOA
iii/KIFO
sasa nyie munaojiita mabinti wa kileo kalaga bao.

Pole mkuu inawezekana hujui unachozungumza.....kutamkiwa ndoa ni nini? Hata kichaa anaweza kukutamkia ndoa..utafurahi kwamba nimetamkiwa ndoa? Suala linaloleta ugumu ni kwamba je huyu anayetamka ndoa ndiye hasa ninayemtaka? Siwezi..narudia tena siwezi kuingia kwenye ndoa kwa sababu nalazimika kuolewa or someone is there to marry me....matokeo ya ndoa za kujilazimisha ni majuto na maumivu yasiyokwisha.
 
Ndo akili yako ilipoishia?
 
Zinduna wazazi wanafanya hvyo ili kujarib kufuata mising na sheria za dini na mila. unapoolewa ile dhambi ya uzinz haitakuepo unles otherwiz unapenda michepuko. pia hakuna mzazi anaependa azae nje ya ndoa na huwa wanapatwa na aibu na stress ikitokea hvy. so wana sababu za mcng ila tu madhara yake ni km hy wanawake kuwork hard kutfrta ndoa hatimae kupata ndoano badala ya ndoa. nicchokubaliana nacho mimi ni perception za watu mwanamke asipoolewa atasemwa weeeee!! mwanamke tofaut na mwanaume yy anasubiria proposal sasa zispokuja hafanyaje?

Kutokuolewa sio guarantee ya kuwa malaya...kwani sex ni chakula kwamba usiposex utakufa? Unaweza usiolewe ukashika imani yako na ukaishi maisha safi ya kumpendeza Mungu
 
Last edited by a moderator:
Kitu nilichogundua TZ ubinafsi ni mwingi sana, mtu kwake akishajenga ghorofa na pembeni yake kuna vijumba vya udongo bado atakuambia bongo kama ulaya maghorofa tunayo vile vile.

Mimi binafsi naona badala ya kuanzisha somo la kichina, labda tungeanzisha somo linaloitwa rushwa adui wa maendeleo, ambapo watoto wetu wepigwe brain wash kubwa kwamba rushwa ndio cancer iliyotuletea umasikini huu na ikiendelea itatumaliza kabisa, then within 30 years tutakuwa tumeingiza kizazi kipya chenye kasi mpya ya kuleta maendeleo. Hii itakuwa one of the long term strategies ya kuua huyu adui wa maendeleo.

Ingia nchi kama scandinavia huko yaani jamaa mentality yao yenyewe ni mtaji, mtu ukisahau wallet yako sehemu, kesho ukirudi jamaa wamekuwekea unaipata, sasa hawa ukiwakabidhi sehemu yoyote ile shughuli zinakwenda shwari, imagine wafanyakazi wote wa pale ardhi wangekuwa na hii mentality unafikiri kuna mtu angeweza kugawa viwanja viwili kwa mtu mmoja? yaani nafsi yake isingemruhusu kabisa, na tu-create such people is possible, kamaa jamii ishaoza basi tuwafikirie atleast the future generation.

China inapaa kwa sababu moja ya sababu ni kwamba watu wengi na viongozi wengi wanaiogopa rushwa kishenzi, hata kutoa tipp tu kwenye restaurant wengine huikataa kabisa, wanataka umpe hela ile kamili tu (although tipp sio rushwa)

Uarabuni unaambiwa yale mafuta yakichimbwa kila muarabu pale anafaidika, wote wako fiti hamna omba omba pale, na mashirika pia yanatajirika na wafalme pia wanatajirika kila mtu anapata chake, lakini kwetu ni viongozi na investors tu, sisi tunaachwa tulie.

Amen....
 
Nashukuru kuona at least kuna wanaume wako positive kiasi hiki. Wengine hapa naona wanajaribu kutuaminisha hapa kuwa bila wao heshima haiwezi kupatikana.

Heshima ni mtu kwanza mapokeo baadae sasa kama huyo anayetakiwa kuheshimiwa haoni sababu wala maana ya heshima hiyo isipokuwa manyanyaso na majuto, juu ya nini kukaa na kulia kila siku!!!!!!

Jiandae vizuri sana kwa maisha akitokea partner poa tu ila isiwe ndio kama pumzi ukikosa utakufa!!!!!
 
Hakika...mtu yuko tayari kuumia maisha yake yote ili kuwaridhisha watu...hawa ndio wanaofanya watu kuogopa kuingia kwenye ndoa kwa kuona ndoa ni kama jela wakati ndoa ni paradiso ndogo...inahitaji upate mtu wako mwenyewe haswaaa....kama hayupo usilazimishe p.chu kuwa suruali utaumia
 
If am not mistaken hii phrase imetoka kwa apostle Paul; am not so sure kama mantiki yake ya kustay unmarried na unayoiongelea wewe zinafanana kiuhalisia.

Himself he stays unmarried and he meant it (no kids no that mchezo) mnaotaka kuiga sasa mnastay unmarried and yet u get pregancy for men they get busy making babes here and there!!

If u aint a nun/padri.... ndoa bora ni muhimu aisee labda tu oppose hapo kwamba si bora ndoa

Yes...kitumia maandiko kudefend msimamo wako hakikisha unaishi kimaandiko haswaaa
 
Kutokuolewa sio guarantee ya kuwa malaya...kwani sex ni chakula kwamba usiposex utakufa? Unaweza usiolewe ukashika imani yako na ukaishi maisha safi ya kumpendeza Mungu

Mkuu kama chakula kilivyo one of the basic needs kwakweli nionavyo mimi even sex is one big basic need....unaishije miaka miaka 30,40 50 onwards without sex???? kwa mdomo utasema inawezekana lakini ukiwa kama binadam uliyekamilika mwenye vichocheo active ni ngumu na mwisho wa siku mnaishiga kabaka

Hao matoashi wenyewe wanatengwa ila wanaishia kuchepuka tu do not underestimate the power of nature bana
 
Back
Top Bottom