Isumbwile
JF-Expert Member
- Dec 12, 2012
- 801
- 359
Najua kwamba wengi wetu hukimbilia kupima ukimwi kabla ya kufunga ndoa na wenzi wao, lakini sijawahi kusikia wapenzi wakipima genes za magonjwa ya kurithi kipimo ambacho nadhani kinafanywa kwa kutumia DNA Test.
Nakumbuka baba yangu aliwahi kunisimuli kwamba zamani wao ilikuwa kabla ya posa kupelekwa ni lazima kila upande ujiridhishe kama familia husika ilikuwa haina magonjwa ya kurithi kama vile sickle cell, kifafa nk.
Tofauti na zamani siku hizi watu wengi wamehamia mijini kutokana na mabadiliko ya kiuchumi ambapo kuna muingiliano wa makabila. Siku hizi watu wamekuwa wakioana kwa kukutana mijini tu na hakuna hata mmoja anajua kuhusu familia ya mwenzake, hivyo watu wamekuwa kama vile wanacheza bahati nasibu.
Lakini pia mababu zetu walikuwa wakichunguza tabia mbaya zinazotembea katika familia husika inayotaka kuoa binti yao au familia kijana wao anapotaka kuoa, tabia mbaya zilizokuwa zikichunguzwa ni ulevi kupindukia, wizi, mkono wa kupiga kwa wanaume, uzinzi, ushirikina nk. Haya hayahitaji vipimo vya kitabibu, kwa sababu mara nyingi historia inahukumu.
Kwa kuwa siku hizi ni vigumu kwa baadhi ya wapenzi wanaotaka kuoana wanatoka katika makabila tofauti au mikoa tofauti, je kuna umuhimu sasa wa wanandoa kufanya vipimo vya maradhi ya kurithi (genotype) ili kuepuka kupata watoto wenye matatizo hayo?
Naomba changamoto zenu wadau:
snowhite, Paloma, Fixed Point, Kongosho, gfsonwin, Preta, DEMBA, Heaven on Earth, Lisa, Nivea, Teamo, miss chagga, miss neddy, lara 1, King'ast, AshaDii, Munkari, MankaM, mayenga, Mwita Maranya, Jiwe Linaloishi, Kiranga, Nyani Ngabu, The Boss, Asprin, Arushaone, Mzee wa Rula, Filipo, Erickb52, charminglady
Am just curious Mkuu@Mtambuzi , ingekuwaje kama mama ngina enzi zile mmekolea kwenye uchumba mkaenda kupima then mkajikuta carriers wa wagonjwa fulani,vp mngeachana???