Je, Kichwa Hiki Cha Habari Ni Tata?!

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
Napenda niseme kabisaa hapa mwanzo kuwa miye siyo mwanataaluma wa uandishi, ila niliposoma tu kichwa cha habari cha ifuatayo nikajisikia vibaya kinamna fulani hivi. Naomba uisome kwanza:

Tanzania kulamba zaidi ya Sh. Bilioni 250 za kukomesha malaria, TB

2007-10-12 16:32:50
Na Moris Lyimo, Jijini


Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoendelea zitakazofaidika na pesa kiasi cha Euro Milioni 200 ambazo ni zaidi ya Sh. Bilioni 250 za Kibongo, zitakazotolewa kama msaada katika Mfuko wa Dunia wa kutokomeza kifua kikuu, ukimwi na malaria kusaidia miradi ya afya katika nchi masikini.

Mratibu wa taasisi binafsi ya udhibiti wa malaria ya Alliance Against Malaria (TANAAM), tawi la Tanzania, Bi. Beatrice Minja, aliiambia Alasiri kuwa Serikali ya Ujerumani imeahidi kutoa fedha hizo katika Mkutano uliomalizika wiki iliyopita katika mji Mkuu wa nchi hiyo Berlin.

Amesema fedha hizo zitatolewa katika awamu ya pili ya mpango huo unaotambulika kama `Debt 2 Health Initiative` utakaoanza katika kipindi cha zaidi ya miaka minne ijayo kuanzia mwaka huu unaohusu kusaidia miradi ya afya katika nchi masikini.

Awamu ya kwanza ya mpango huo ilizinduliwa katika mkutano huo wiki iliyopita ambapo Serikali ya Ujerumani na Indonesia zilisaini mkataba wa Euro milioni 50 kusaidia miradi ya afya nchini Indonesia.

``Indonesia ilisaini mkataba huo kwa masharti kwamba itawekeza nusu kiasi hicho katika miradi yake ya afya kupitia mfuko wa dunia wa ukimwi, kifua kikuu na malaria,`` alisema Bi.Minja.

Alisema Ujerumani ni nchi ya kwanza kufadhili miradi ya afya ya mfuko huo na imekuwa karibu zaidi na mfuko wa dunia kuendeleza programu ya Debt2 Health Initiative ambapo Indonesia ni eneo lengwa na mpango huo.

Mwezi Aprili mwaka huu Bodi ya Mfuko wa Dunia ilipitisha azimio la awamu mbili za programu hiyo na kuhusisha nchi nne ambapo Indonesia ilikuwa ya kwanza wakati Kenya, Pakistani na Peru zilitajwa kuanza kufaidika na mpango huo.
Source link: IppMedia.

Najua ni kweli kuwa nchi yetu inategemea misaada, lakini katika kichwa hicho cha habari misaada inaonekana kuhalalishwa kama njia mojawapo ya kuendesha maisha, na pia kichwa cha habari nakiona kinapamba picha moja ya wananchi ambao hawana njia nyinginezo tena za kujikomboa ila misaada ndiyo ya kufurahia. Je ndiyo hivi?!

Hilo neno 'kulamba' ndiyo linalonitatiza. Miye naona aliyeweka hicho kichwa cha habari anasahau kuwa Tanzania ina 'masikini jeuri' ndani yake. Nikimaanisha kuwa maneno kama hayo juu yanahalalisha misaada lakini pia kudharilisha kinamna fulani hapo hapo. Sijui kwa kweli, labda ndiyo maana rafiki zangu wananiita masikini jeuri...

Nakubali hizo pesa ni za matumizi muhimu sana kama zitafanya kazi yake ipasavyo, ila ni hicho kichwa cha habari ndiyo nina utata nacho miye. Sasa Je, wenzangu JF mnaweza kuniweka sawa katika hili au ni hisia zangu tu hazijakaa vizuri katika hili.

SteveD.
 
Back
Top Bottom