Je, Kabendera na Tito Magoti watafika mahakamani kama mashahidi wa utetezi? Kutajwa kwao kunalenga nini kwenye kesi ya Mbowe?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Ukifuatilia kesi inavyoendelea yapo Mambo makuu matatu unayabaini kuhusu shahidi wa Jamhuri SP Jumanne. Kwanza, swali kwamba anatoka kabila gani na kujibu kwamba ni Msukuma Lina maswali mengi hasa likiunganishwa na awamu iliyopita pamoja na ukweli kwamba kituo chake pamoja na kuwa Arusha alipewa kibali chakuzunguka nchi nzima tofauti hata na taratibu za jeshi la Polisi. Kwa maana nyingine aliamiwa kwamba zimwi likualo alikuli likakumaliza na aliwekwa kwenye mnyororo wa utawala unaoitwa Sukuma Gang. Yamkini huyu ipo siku angeteuliwa kuwa IGP.

Cha pili, swali kwamba alishirikiana na Makonda means wapo watu waliaminiwa na utawqla wa juu wakawa wanajifanyia mambo bila kudhibitiwa na mtu yeyote.

Tatu ameulizwa swali kuhusu kumfahamu Tito Magoti akasema amfahamu,in real sense huyu ni mwongo. Tito alikamatwa nchi na Dunia ikamfahamu huyu anasema amfahamu. Lakini pia anaulizwa kwa maana kwamba Kibatala anataarifa kwamba huyu alishiriki aidha kumkamata au kumhoji Tito Magoti, lakini shahidi huyu anakwepa kwa kusema hana taarifa. May be Tito anaweza kutueleza namna anavyomfahamu.

Nne anaulizwa swali kama alihusika na kesi ya Kabendera, anabisha. Kabendera kupitia ukurasa wake wa tweer anakiri kati ya sura ambazo hazijamtoka kichwani ni Jumanne. Maana yake huyu Jumanne pia kesi ya kabendera alihusika na wakati huo pia alikuwa Arusha kesi ipo Dar. Ni mtaalam pekee wa jeshi la polisi Hadi ahusike Kila kesi ya DSM?

Tano. Anaulizwa kuhusu kukamatwa na kupoteza kwa Ben saanane, anakana kufahamu. Kabendera kwenye tweer anamtaka MBOWE aeleze Kila kitu kuhusu Ben mambo Yawe adharani. Means wahusika wanafahamika.

Sita; huyu Jumanne alishiriki kuchukua Rushwa ya Milion mia Arusha na TAKUKURU wakawa wanamchunguza lakini amepandishwa cheo akiwa ndani ya uchunguzi tuhuma za rushwa ambazo TAKUKURU haijawahi kumsafisha au kutoa taarifa ya uchunguzi.

Kwa mifano hiyo na kwa kipengele Cha sita huyu Jumanne ni mtu mwenye network kubwa sana na yawezekana kwenye kundi hili na kwa promosheni hizi usishangae mmoja wao akawa IGP huko mbeleni tuendako.

Lakini pamoja na kibali walichopewa cha kufanya wanavyojisikia Je, walioumizwa na mfumo huu wakapiganiwa mitandaoni Hadi wakatoka watakuwa tayari kusimama kizimbani kueleza mahakama ukweli wa kile walichofanya akina Jumanne?

Mwisho, kama akina Jumanne wamepewa Promotion siku siyo nyingi Kingai atapata promotion ya President Kwa KAZI nzuri aliyofanya na hapo ndipo tutabaini Mimi na yeye ni kitu kimoja.
 
Shahidi: Miye ushawahi kuniona kwa Sabaya?

Kibatala: Si nyie Jeshi la Polisi

Shahidi: Aaah! Sawa hapo sawa, Kama Jeshi la Polisi sawa, Mwanzo Hukuwa specific

Huyu jamaa ni kubwa jinga damu za wengi tusiowafahamu zinamlilia.

Ipo siku atalipwa hapa hapa duniani.
 
Jumanne ni muuaji na mhalifu mkuu. Ni jitu lisilostahili kuwa huru. Siku tukipata kiongozi mwenye hekima, kiongozi wa haki, huyu hataishi uraiani kamwe.
 
Back
Top Bottom