Je, itakuwaje kama ukiacha kulala usingizi?

Josevic

Member
Apr 30, 2013
19
11
Inashauriwa kulala masaa 6-8 kwa siku. Lakini itakuaje kama ukiacha kusinzia kabisa?

Kwa kawaida binadamu hutumia theluthi moja (⅓) ya maisha yake akisinzia. Hii ina maana mtu aliyeishia miaka 60, basi ametumia miaka 20 kulala. Kama tusipolala ni wazi tutapata muda wa kutosha kufanya mambo mengi iwe kazi, kujifurahisha na kujifunza vitu vipya.

Pamoja na faida hizo za nje ya mwili, miili yetu hufaidika sana pale tunapisinzia. Unaposinzia mwili huachilia homoni ambazo huenda kutengeneza tishu za mwili. Mfano unaponyanyua vyuma, unapolala ndio muda mwili unapotengeneza seli na tishu ili ujazie.

Sasa usipolala yafuatayo yatakutokea.

Baada ya masaa 24: Utakuwa sawa kabisa na utakuwa mwenye furaha na nguvu zaidi . Hii ni baada ya ubongo kuachia homoni ya dopamaini kupitia mfumo wa kimesolombiki.

Ila usidanganyike na furaha hii maana haidumu.

Baada ya masaa 24: mwili wako utapunguza kasi ya kufanya vitu. Utaanza kusahau ulichokuwa unafanya na utaonekana kama umelewa pombe .

Baada ya siku mbili bila kusinzia, mwili huanza kuzima na kuacha kujitengenezea sukari (hivyo hukosa nguvu). Ngozi huanza kupauka, macho kuwa mekundu, na makunyanzi kuongezeka usoni.

Baada ya siku 3: Utaanza kuona na kusikia vitu visivyo halisi. Hii ni baada ya ubongo kuanza kuleta ndoto katika maisha ya kawaida. Pia mwili huanza kuvunja protini, sukari, mafuta na misuli ili kutengeneza nishati. Kama ulikuwa baunsa basi utaanza kuisha.

Baada ya wiki mbili: Kinga ya mwili wako itapungua sana na katika hatua hii unaweza kufariki hata kwa mafua ya kawaida . Ikitokea hujapata magonjwa ya kuambukiza... Tuendelee...

Baada ya wiki ya tatu: unaweza kupata shambulio la moyo na kupoteza maisha. Kama mwili wako uko vizuri basi unaweza kuzidi hapa kidogo.

Ni muhimu sana kuhakikisha unapata usingizi wa kutosha wa masaa 6 hadi 8 kwa siku. Lakini ITAKUWAJE KAMA ukilala kichwa chini miguu juu...?
 
Mie nikisinzia 2hrs tu siku inayofuata ni majanga sana. Kusinzia ni muhimu sana.
 
Back
Top Bottom