Elections 2010 Je, huu ni ulaghai wa CCM kuhusu hospitali ya rufaa?

babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
5,221
3,167
Jakaya Kikwete wakati akifanya kampeni mkoa wa Kilimanjaro aliahidi kuboresha hospitali ya Mawenzi kama inavyoelezea kwenye nyekundu hapo chini
JK wants to know candidate financing Mawenzi Hospital
By Patrick Kisembo
17th September 2010


CCM presidential candidate Jakaya Kikwete
CCM presidential candidate Jakaya Kikwete has directed leaders in Kilimanjaro Region to find out and inform members of the public, the person financing the construction of Mawenzi hospital in Moshi District.
Addressing a campaign rally yesterday, Kikwete said there were rumours that the hospital was being funded by one of the opposition party candidates and he wanted him or her known publicly.
“I have heard that there is a person funding the construction of Mawenzi hospital, while it is normally funded by the government,” he said.
He said there was no reason for a contestant to lie to the people in order to be voted for in the forthcoming October general election.
The CCM national chairman said the government was undertaking the project and had set aside a total of 1.6bn/- to upgrade the hospital to a referral status, explaining that a four-storey building would be added to the infrastructure.
While in Bomang’ombe area, Hai District, Kikwete called on the people to vote for the outgoing legislator, Eng Fuya Kimbita. He said Kimbita had considerably contributed to the development of the people in Hai constituency.
He promised to provide Hai residents with improved coffee seedlings to ensure quality yields. He said the government was consulting a US-based coffee company to find the market for Tanzanian coffee.
Kikwete also promised to improve social services including education, health care, infrastructure and water.
SOURCE: THE GUARDIAN

Siku mbili baadae akiwa anafanya kampeni mkoani Manyara alitoa ahadi ya kuzipandisha hospitali saba kuwa za rufaa lakini hospitali ya Mawenzi haikuwa kwenye list kama alivyoahidi mkoani Kilimanjaro.
JK aahidi hospitali saba za rufaa
By Hellen Mwango
19th September 2010



Mgombea urais kwa tiketi CCM, Dk. Jakaya Kikwete

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Jakaya Kikwete amesema serikali yake ijayo itazipandisha hadhi hospitali saba maalum nchini na kuwa za rufaa, ili kuipa nafasi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kutoa huduma ya magonjwa yaliyoshindikana badala ya wananchi kwenda kutibiwa nje.
Dk. Kikwete aliahidi hayo jana alipokuwa akiwahutubia maelfu ya wakazi wa Tarafa ya Hydom, katika mkutano wa kampeni za kutetea kiti chake cha urais wilayani Mbulu, Mkoani Manyara.
Aidha, alizitaja hospitali hizo kuwa ni, Hydom, Arusha ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheli (KKKT), St Gasper ya Itigi, St Francis ya Ifakara, mkoani Morogoro, Ndanda ya mkoani Mtwara, Peramiho na hospitali ya Ilembula iliyopo mkoani Iringa.
Alisema kuwa baada ya hospitali hizo kupandishwa hadhi hivi karibuni, zitakuwa na uwezo wa kuhudumia wananchi wengi na kutoa mfano kuwa hospitali ya Haydom ikipadishwa hadhi itaweza kuhudumia wakazi wa Singida na Shinyanga.
"Tutataka kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ili iweze kushughulikia magonjwa makubwa yaliyoshindikana badala ya wananchi kwenda kutibiwa nje ya nchi. Hospitali hizi maalum tutakazozipandisha hadhi na kuwa za rufaa, zitahudumia wagonjwa ya kawaida," alisema.
Aidha, alisema kuwa mbali na kuzipandisha hadhi hospitali hizo, pia wataboresha mazingira ya kazi katika hospitali hizo ili madaktari waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.
Akisalimia wananchi katika Kata ya Muslur, wakazi hao walilalamikia tatizo la mimba kwa watoto wao wa kike, hivyo kumwomba awasaidie wapate hosteli, ili watoto wao wasikatishe masomo kutokana na tatizo hilo.
"Mheshimiwa hapa tuna tatizo la watoto wetu kupata mimba, kwani wanaishi kwenye magheto, tunaomba utusaidie tupate hosteli, ili tuwaokoe watoto wetu," alisema mkazi mmoja wa eneo hilo.
Akihoji kero hiyo, mgombea huyo wa urais aliwataka wakazi hao kukusanya nguvu na kuchangia ujenzi wa hosteli na kwamba naye atawasaidia katika kukamilisha.
Mbali na kero hiyo, kero nyingine za wakazi wa kata mbalimbali katika wilaya ya Mbulu ni ukosefu wa mtandao wa simu za mkononi, umeme, zahanati na maji safi na salama.
SOURCE: NIPASHE JUMAPILI

Mwezi uliopita nilisoma ufafanuzi wa kamanda wa vijana wa UVCCM Moshi Mjini Aggrey Marealle kuhusu maneno aliyoyasema wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM mkoani Kilimanjaro. Katika utetezi wake niliguswa na sehemu moja, nina mnukuu “Nawahisi wasifanye hivyo na badala yake wamchague Bw Justin Salakana kwa kumpa kura ili aweze kufanya kazi na serikali ya Chama tawala kinachoongozwa na Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Niliwasihi wananchi wa Moshi kuwa wasipofanya hivyo, BASI LA MAENDELEO HALITASIMAMA MOSHI NA BADALA YAKE LITAENDA KATIKA MIKOA JIRANI KAMA VILE ARUSHA,TANGA, MANYARA NA MIKOA MINGINE JIRANI”.

Kauli hiyo ya kamanda wa vijana ilifanya niifananishe ccm sawa na baba ambaye ana mtoto wa kambo na watoto wengine wa kuwazaa, wote kwa pamoja wanalitumikia shamba la familia lakini mazao yanapovunwa baba anawagawia watoto wake wa kuwazaa na kunyima mtoto wa kambo.


Asilimia kubwa ya pesa zinazotumika kuleta maendeleo zinatokana na kodi tunayotozwa sisi wananchi wakiwemo wana Chadema pia.Kutumia pesa za kodi hizo kuleta maendeleo kwenye majimbo ya ccm tu na kubagua ya upinzani ni UFISADI WA HALI YA JUU.


Kutokana na hizo ahadi za Mwenyekiti wa CCM taifa na kamanda wa vijana UVCCM Moshi Mjini. Je, Kikwete baada ya kumaliza kampeni zake mkoani Kilimanjaro aligundua washabiki wa upinzania ni wengi na baadhi ya majimbo ya ccm yatachukuliwa na wapinzani akaamua BASI LA MAENDELEO LISISIMAME MKOANI KILIMANJARO?

Au alidanganya kwa ajili ya kura huku akiwa hana mpango wowote wa kuipandisha hadhi?
 
Usalama wa taifa ndio wanamwandalia taarifa aseme nini, afanye nini na kwa wakati gani, wamekuwa wakijishughulisha sana kumbomoa bwana mkubwa kwa taarifa za udanganyifu, kuanzia leo tutasikia makubwa tena mikoa ya kusini.

Hospitali ya mawenzi inatakiwa kujengwa upya kabisa na shilingi 1.6 bilioni ni pesa za kutosha kujenga vyoo peke yake, kwa taratibu za serikali ya ccm.

 
Kwa sasa JK anafanya usanii tu, anaahidi tu ili mradi apate kura, ikumbukwe kwamba hiki ni kipindi chake cha mwisho hivyo hatakuwa na wa kumuuliza. Akiwa mkoani Mbeya aliwaahidi wakulima serikali kupitia wakala wa ununuzi wa mazao ya chakula itanunua mazao ya wakulima, wakulima wakapeleka mazao yao kwenye maghala ya serikali, sasa mwezi umeisha bado zzziiiiiiiii! ni usanii tu wa JK na genge lake la wahalifu
 
Usalama wa taifa ndio wanamwandalia taarifa aseme nini, afanye nini na kwa wakati gani, wamekuwa wakijishughulisha sana kumbomoa bwana mkubwa kwa taarifa za udanganyifu, kuanzia leo tutasikia makubwa tena mikoa ya kusini.

Hospitali ya mawenzi inatakiwa kujengwa upya kabisa na shilingi 1.6 bilioni ni pesa za kutosha kujenga vyoo peke yake, kwa taratibu za serikali ya ccm.
Ni kweli kabisa Hospitali ya Mawenzi inaitaji ukarabati mkubwa kama sio kuanza from scratch.Juzi nimeingia baadhi ya wards zimechakaa kupita kiasi ni risk sana kufanyiwa upasuwaji kwenye hospitali iliyoko kwenye mazingira kama yale,unaweza kwenda kutafuta matibabu ukaondoka na magonjwa mengine.

Niliposoma ahadi ya Kikwete kuipandisha hadhi, ilinipa moyo kiasi fulani na serikali kwa sababu nilijua wataifanyia ukarabati wa hali ya juu, vile vile niliamini CCM imeamuwa kuondokana na ile dhana "ukitaka mambo yako ya kunyooke jiunge na sisi" baada ya siku mbili unapojua ilikuwa ni ulaghai inatia kichefu chefu kweli.
 
Safi sana! Wana Kilimanjaro ni sawa na "maskini jeuri".Bado wapo baada ya kuambiwa wakiendelea kushabikia upinzani BASI LA MAENDELEO HALITASIMAMA MOSHI.Ni vizuri kuona baadhi ya wapiga kura wanasimamia Principles.
 
Back
Top Bottom