Je, hii 'Media Blackout' ya leo juu ya tukio zima la uchukuaji fomu wa Tundu Lissu ndiko kumuenzi vyema Mwanahabari Hayati Rais Mkapa?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,689
109,119
Nichukieni mtakavyonichukia GENTAMYCINE ila pamoja na kwamba nakipenda Chama changu Tawala ambacho ndicho Kimeshika Dola ya Kiserikali cha CCM, ila kama 'Mwanataaluma' kitendo kilichofanyika leo hasa cha 'Media Blackout' dhidi ya Tukio zima la Uchukuaji Fomu wa Tundu Lissu wa CHADEMA na ambayo nayasikia yameendelea huko katika Newsrooms ni 'Upumbavu' mtupu

Sijaona sababu yoyote ile ya Vyombo Vikubwa vya Habari nchini Kupigiwa Simu na hata Waandishi wake 'Kutishwa' hasa kama wakipeleka Hewani ( kama haya Madai ni ya kweli kwani sijayathibitisha bado ) Habari za hili Tukio zima, lakini kinachonisikitisha tu ni kwamba Serikali yangu ya CCM imefanya mengi na makubwa kwa miaka hii Mitano sasa iweje leo hii imuogope Tundu Lissu hivi?

Najua kuwa Tundu Lissu ( Mtani wangu huyu kutoka Mkoani Singida nae ana Changamoto zake ) ila binafsi nilidhani njia pekee ya 'Kummaliza' Kisiasa ni Sisi wana CCM na Serikali yetu Kumuonyesha kwa Vitendo 'Maendeleo' tuliyoyafanya na siyo 'Kumuogopa' hivi hadi kumfanyia 'Mizengwe' ili Tukio zima la leo lisiwe Masikioni mwa Watu ( Watanzania ) tukidhani kuwa labda ndiyo tutamuweza.

Wala haiitaji 'Akili' kubwa kujua ya kwamba kadri Mamlaka husika iliyo chini ya Chama changu Tawala cha CCM kinavyopambana kutaka 'Kumzima' Kisiasa na Kiumaarufu hivi Tundu Lissu kwa 'Kuwatishia' Wanahabari na Vyombo vyao basi ijue ya kwamba ndiyo inasaidia mno Kumuongezea 'Umaarufu' wako na hapa kuna 'Athari' nyingi tu kwa upande wa Kura CCM yangu itazipata.

Halafu Wiki iliyoisha tulikuwa tunamsifu na kumpamba kweli kweli Nguli wa Habari nchini na Mwandamizi kabisa Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin William Mkapa kwamba alipenda 'Demokrasia' na hakuwa na 'Mabavu' dhidi ya Wapinzani. Je, huu 'Upumbavu' uliofanywa leo wa 'Kuvitishia' Vyomba vya Habari Vikubwa nchini 'Visiripoti' Tukio la Lissu ndiyo Kumuenzi Mkapa?

CCM yangu naipenda, Rais na Mwenyekiti wangu Dkt. Magufuli namkubali sana hata Mwenyezi Mungu anajua ila huu 'Upuuzi' mkubwa sijaupenda.
 
Wapinzani kuweni na youtube channel zenu. Nunueni vifaa vya kurusha matangazo kama blackmagic, teradek,cerevo,liveUsolo,vidiu,mevo,gopro, roland livestream,dji drone livestream. Share link kupitia mitandao waambieni watu wasubscribe wafike 5m. Kulalamika hakutasaidia kitu.

Muda wa kampeni hakuna chombo chochote cha habari kitakacho onesha hata picha yenu.

Nunueni vifaa.
 
Licha ya media kuzuiwa chadema ilishindwa Nini kuanzisha online media, page zao na kutoa habari, maana jinsi wanavobanwa na ccm kuachwa wanapigwa gape, atleast wangerusha tukio kwenye account za CDM kusubiria huruma tu watasanda, CCM imechokwa ni vile inajipa promo
 
Uko sahihi Sasa kipindi kina ruzuku walishindwa kuwekexa Mambo muhimu ka haya, CDM inabidi kutafta vichwa vipya vya kuwapa ushauri, hii kulia Lia faulo za ccm hazisaidii
 
Wapinzani kuweni na youtube channel zenu. Nunueni vifaa vya kurusha matangazo kama blackmagic, teradek,cerevo,liveUsolo,vidiu,mevo,gopro, roland livestream,dji drone livestream. Share link kupitia mitandao waambieni watu wasubscribe wafike 5m. Kulalamika hakutasaidia kitu.

Muda wa kampeni hakuna chombo chochote cha habari kitakacho onesha hata picha yenu.

Nunueni vifaa.
Kumbe chadema digital nisawa na kitochi changu 'it has proved failure , it is a big shame. If they invested alot of money then it is a waste of'
 
Licha ya media kuzuiwa chadema ilishindwa Nini kuanzisha online media, page zao na kutoa habari, maana jinsi wanavobanwa na ccm kuachwa wanapigwa gape, atleast wangerusha tukio kwenye account za CDM kusubiria huruma tu watasanda, CCM imechokwa ni vile inajipa promo

Hapa ndiyo utajua kwa nini zilitakiwa kusajiliwa na kulipiwa! Lengo ndiyo hili sasa mdogo wangu

Hata gazeti lao likafungiwa 😂😂😂
 
Genta my brother, I’m sorry to tell you that this year is the LAST YEAR FOR CCM to lead Tanzania.

Mark my words. Huu ndo mwaka wa mwisho kuongoza Tanzania. From October nchi inaenda kuwa chini ya Chadema.

Nimesikiliza kwa Makini sana hotuba ya Mzee Butiku jana kwenye mkutano wa NCCR. Kuna ujumbe aliutuma kwa TISS, Polisi, JWTZ na NEC . Kwa nilivyomsikia nimejiridhisha kuwa wazee wenye maamuzi yao waneridhia nchi kwenda upinzani mwaka huu.

Tukutane October ndugu yangu Genta!!
 
Kumbe chadema digital nisawa na kitochi changu '
Yaani hawako serious. Yaani kununua vifaa wameshindwa?
Vifaa vinavyohitajika ni
-camera yenye sdi out
-wireless microphone ya camera
-sdi cable
-liveUsolo
-modem ya 4G
-line ya 4g yenye bando.

Wakipata hiyo setup wanaweza kuenda live wakiwa popote kwenye mtandao kupitia youtube, facebook. Inabidi wanunue haraka kabla ya kampeni kuanza. Hakuna chombo chochote cha habari kitakacho onesha hata picha ya wapinzani.

NB: wale wazoefu wa kuagiza vitu mtafanya bajeti ya vifaa.
 
Sumaye kapewa nafasi ya kusalimia hapa.. Si akaanza kufunguka. MaTBC yakamzima.

Kama taifa tulipofika hapavumiliki tena.

Ni nani hao wanaotaka kuona na kusikia yanayowapendeza tu.?!?.

Hii ni kinyaa kikubwa ktk muhimili wa Habari.
 
Wapinzani kuweni na youtube channel zenu. Nunueni vifaa vya kurusha matangazo kama blackmagic, teradek,cerevo,liveUsolo,vidiu,mevo,gopro, roland livestream,dji drone livestream. Share link kupitia mitandao waambieni watu wasubscribe wafike 5m. Kulalamika hakutasaidia kitu.

Muda wa kampeni hakuna chombo chochote cha habari kitakacho onesha hata picha yenu.

Nunueni vifaa.
Hili naunga mkono
 
Back
Top Bottom