Doctor Ngariba
JF-Expert Member
- Jan 28, 2020
- 481
- 766
Wakuu naamini muko buheri wa afya, pole kwa ambao wanapitia changamoto ya afya na Mungu awaponye.
Naombeni wanajukwaa munijibu swali langu kuhusu vita kati ya Hamas na jeshi la Serikali ya Israel. Nitashukuru iwapo jibu/majibu yataepuka yale maneno na misamiati ya "Wazee wa Makobazi", "migalatia" na mengine yenye kuashiria kuegemea upande flani ili kuweza kujifunza.
Japo nina imani yangu, lakini nauliza hili nikiwa neutral na dhamira kuu ni kupata maarifa kwa watu wenye utaalamu wa maswala ya kivita pamoja na siasa za kimataifa kwa hiyo naomba pia wenye kujibu wawe neutral.
Niende kwenye mada kama ilivyo kwenye kichwa cha habari hapo juu.
Hamas kwa uchache wao (kwa kuzingatia eneo la Kijiographia) sidhani kama wangekuwa bado wanapambana na jeshi la IDF takribani kwa miezi miwili bila kupata msaada wowote wa kijeshi iwe silaha,milltary personnel au hata upelelezi dhidi ya jeshi linaloaminika kuwa bora na lenye kupata back up kutoka kwa Marekani na washirika wake (kama wapo)
Kama wanasaidiwa, swali linakuja na nani na hiyo misaada inaingiaje kwenye eneo dogo na ambalo kwa kiasi kikubwa limezingirwa na linashambuliwa kwa makombora mazito ya kila siku na jeshi la Israel?
Kwa kuzingatia eneo dogo la ukanda wa Gaza na kuwa Palestina ni nchi (japo haina sovereignty) ambayo almost inazungukwa kila upande na Israel, nadhani siyo rahisi kuingiza silaha kutoka nje hasa kipindi hiki cha vita bila kufahamika na jeshi la IDF(niko tayari kurekebishwa kama nitakuwa nimekosea)
Rejea hapa 👇
"With around 2 million Palestinians on approximately 365 km2 (141 sq mi) of land, Gaza has one of the world's highest population densities. The Strip contains eight refugee camps."(WIKIPEDIA)
Na kama hawana msaada (hususani wa kijeshi ndani ya eneo la kivita) nguvu hii ya kupambana hadi leo wanaitoa wapi na silaha zao mfano wa manati dhidi ya vifaru na ndege vita bora kuwahi kutokea. Au kwamba walidunduliza kwa kipindi kirefu kabla ya vita?
Mwisho kwa ajili ya kujifunza, nini hatma ya vita hii iwapo Israel itafanikiwa kuwaondosha Hamas katika ukanda wa Gaza? Je, eneo hili litakuwa mali halali ya Israel au wataachiwa Wapalestina wenyewe chini ya uangalizi wa Serikali Jerusalem?
Nawasilisha na naomba kujifunza kutoka kwenu.