Je, bado kuna umuhimu wa kuhamisha makao makuu ya nchi Dodoma?

Karibia nchi zote afrika,ofisi za serikali zao zipo makao makuu ya nchi husika,Ni lini serikali ya Tanzania ofisi zake zitahamia Dodoma?
 
Kuita makao makuu Dodoma na serikali kuwa DSM ni mradi. Unajua ni kiasi gani cha fedha kinachotumika kama masurufu kwa watumishi wa serikali kuu kuja Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge? mawaziri je? madereva je? Hata machangudoa wanafaidika. Natamani kukutupia hii chupa ya bia niliyoshika, usilete mkosi.

Hilo jambo hata serikali ya awamu ya nne imeamua kupotezea....haimo kwenye ilani na hakuna anayezungumzia. Sijui vyama vya upinzani vina maoni gani
 
Kuna mahali nimesoma, sijui ni humu JF au wapi. Watu wa Nigeria baada ya kupata picha kamili ya mpango huu walikopi na kwenda kufanya kweli kwao, na wamefanikiwa kuhama toka Lagos kwenda Abuja, hivi karibuni walirudi kuja kukopi tena ule mpango kabambe, walichokiona ...walichoka.
 
Halafu haya ma-mansion yetu utakuja kukodi wewe? Thubutiii, huo mpango umekufa nani atakubali asipigwe na upepo wa bahari
 
Enginner Mtolera sisi bado tunakuamini hebu waeleze hao viongozi na Mainjinia ni kitu gani kinawasibu wasiende Dodoma km ni Makao Makuu mbona Kenya miaka ya 1922 waliamua Nairobi iwe makao makuu na yakawa?
Ila kwa Abuja nakumbuka waliokuwa Viongozi wa CDA enzi zile ndio waliokwenda Abuja kujionea na wakaja bna majibu, sasa sijui ni siasa au fedha hakuna?
 
Mimi kwangu kuhamia dom sioni kama ni priority ..kama 90% wanafunzi wamefali hili ndo la kushughurikia kwanza sahvi
 
Ndio maana majengo yanaporomoka dar kwa ajili ya kulazimisha kuyalundika yote dar.
 
Ndg wanaJF

Natamani sana kuishtaki serikali kwa kutulaghai na kuchukua michango mingi sana hasa miaka ya 1980 kwa minajili ya kujenga makao makao makuu ya nchi.

Nakumbuka walikuwa wanachukua kwa lazima na risiti tunazo.
Kumbe uongo. Wapi MTIKILA?
 
Hata kituo cha kimataifa cha mikutano si mmeona kimejengwa hapa Dar na mchina? Sasa mmeanza maswali yenu yasiyo na tija.
 
Tupo na Bagamoyo Corridor kwa sasa

Kwa vile wanahaha kutafuta wapi pa kuwekeza pesa zao, kama mimi ningekuwa Bwana Maendeleo aka Fastjet ningewakabidhi Wachina mji wa Dodoma waujenge na kuumiliki kwa miaka 100 ili kurejesha mkopo wao na baada ya hapo sisi wenyewe (wakati huo vitukuu vyetu) ndo tuanze kuumiliki.
 
tumechoshwa na maneno ya kanga ambayo yamesemwa sana tangu enzi za mwalimu..kama kweli kuna mpango wa kuhamia DOM nilitarajia majengo ya taasisi mbalimbali yangekuwa yanajengwa Dodoma na siyo Dar..kila nchi ina mji mkuu na mji wa kibiashara...ni wakati sasa dar ibaki kuwa mji wa kibiashara na Dodoma iwe mji mkuu kwa dhati..
 
Back
Top Bottom