Jaribio la nchi za magharibi kuharibu uhusiano kati ya nchi za BRICS litashindikana

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111445542478.jpg


Mkutano wa 15 wa wakuu wa nchi za BRICS utafanyika kuanzia Agosti 22 hadi 24 mjini Johannesburg, Afrika Kusini. Hii sio tu itakuwa shughuli kubwa kwa nchi za BRICS, bali pia itatoa fursa zaidi za maendeleo kwa nchi za Kusini duniani. Hata hivyo, nchi za magharibi na vyombo vya habari vimetoa makala mbaya mfululizo kabla ya kufanyika kwa mkutano huo.



Shirika la habari la Reuters limesema nchi za BRICS zina maoni tofauti kuhusu "kupanuka kwa nchi wanachama." China, Russia na Afrika Kusini zinaunga mkono upanuzi, lakini Brazil na India zinapinga. Hata hivyo haikutarajiwa kwamba saa chache tu baada ya kutolewa kwa makala hiyo, Rais wa Brazil Lula alieleza hadharani kuwa nchi yake inaunga mkono nchi nyingine kujiunga na kundi la BRICS, na hata alipendekeza kubuniwa kwa “sarafu ya pamoja". Wakati huohuo wizara ya mambo ya nje ya India pia ilikanusha ripoti hiyo kupitia msemaji wake. Baada ya kuona kwamba jaribio hili halikufaulu, siku hizi, baadhi ya wasomi wa nchi za magharibi wanadai tena kuwa nchi za BRICS "huenda zikawa vibaraka wa China", na kwamba ushawishi wa wanachama wengine wa kundi hilo unadhibitiwa kikamilifu na China. Lakini kauli hii ilikejeliwa tena na wataalamu wa Russia—"Inawezekana kwamba dai kama hilo linatokana na kushindwa kufahamu vya kutosha uhusiano kati ya nchi za BRICS na madhumuni ya kuanzishwa kwa kundi hilo."



Neno BRICS lilipendekezwa kwa mara ya kwanza na benki ya Goldman Sachs mwaka 2001, wakati msukosuko wa fedha ulipoikumba dunia, na mataifa yaliyoibukia kiuchumi yalitarajiwa kuongoza kufufuka kwa uchumi wa dunia. Hata hivyo, baada ya miaka 20 sasa, nchi za BRICS zilipochangia zaidi ya 50% ya ukuaji wa uchumi wa dunia na kuongoza nchi nyingine za Kusini kuinuka pamoja, nchi za magharibi ziliingiwa na hofu na kuyachukulia maendeleo hayo kuwa tishio, hivyo zikajaribu kuleta uharibifu. Je, ni kwa nini mitazamo ya nchi za Magharibi kwa nchi zinazoendelea imebadilika sana?



Kwa muda mrefu huko nyuma, mitaji na masoko ya kimataifa ilidhibitiwa na nchi za magharibi. Walidumisha hadhi yao kupitia unyonyaji na ukiritimba, na kuruhusu nchi nyingine kupata utajiri tu hadi wao wapate faida kwanza. Hii ina maana kwamba nchi zinazoendelea haziwezi kujiendeleza isipokuwa zijisalimishe kwa kanuni zilizowekwa na nchi za kimagharibi. Lakini sasa, hali imebadilika. China na nchi nyingine zimejitokeza kinguvu na kutengeneza nafasi zaidi kwa nchi za Kusini kutafuta maendeleo yao ya kiuchumi nje ya muundo wa dunia unaotawaliwa na Magharibi. Kwa hivyo, nchi za magharibi kama vile Marekani zinajaribu kuzuia mabadiliko haya kwa kuchukua hatua kama ya kukandamiza China na kuonyesha nini kitatokea ikiwa nchi yoyote inayoendelea itajaribu kujiendeleza kwa njia yake yenyewe. Katika mazingira haya, kama jukwaa muhimu linalowakilisha maslahi ya masoko yaliyoibukia na nchi zinazoendelea, umuhimu wa ushirikiano wa BRICS unaongezeka zaidi.



Kwa mujibu wa serikali ya Afrika Kusini, wakuu wa nchi na serikali 40 wamethibitisha kuhudhuria mkutano wa kilele wa BRICS utakaofanyika wiki ijayo, na huenda idadi hii ikaongezeka hadi kufikia karibu 50. Ni wazi kuwa juhudi zinazofanywa na nchi za BRICS za kukuza utaratibu wa pande nyingi, utandawazi na uhusiano wa kimataifa ulio wa kidemokrasia zimetambuliwa kabisa na nchi za Kusini, ambazo nazo pia zinapenda kuchangia nguvu zao kwenye mchakato huo wa kihistoria.
 
Back
Top Bottom