Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

Hata huko ambapo sheria hiyo ipo, sio kila nyaraka automatically inaikuwa chini ya sheria hiyo.

Ndio maana hadi sasa kuna nyaraka za wakati wa JFK hazijawekwa wazi.

Ni kweli ila nadhani kuna tatizo kidogo kwenye usimamiaji wa sheria hii!
 
Mutiner aki surrender 1964
104408099-an-english-navy-fusilier-disarming-a-rebel-gettyimages.jpg
 
Hata huko ambapo sheria hiyo ipo, sio kila nyaraka automatically inaikuwa chini ya sheria hiyo.

Ndio maana hadi sasa kuna nyaraka za wakati wa JFK hazijawekwa wazi.

Nyaraka gani za wakati wa JFK ambazo hazijawekwa wazi?
 
Yericko Nyerere,

..ur of the mark katika madai yako kwenye post # 4.

..mfano: Hans Pope hakuwahi kuwa Maj Gen. Pia alipatikana na hatia ya makosa ya uhaini na kufungwa jela.

..pia komandoo aliyeuawa alijulikana kwa jina la mohamed tamim, lakini hakuuawa ktk mapambano toka airport mpaka kinondoni.

..kumbukumbu zako ni sawa na zako kuhusu idadi ya majaribio kuwa ni matatu. jaribio la kwanza, na serious kupita yote kwa mtizamo wangu, ni la 1964. jaribio la pili ni la miaka ya 1970 ambalo lilihusisha wanajeshi, wanasiasa kama Kamaliza,Chipaka, etc inasemekana hawa walijaribu kuhusisha wapiganaji wa vyama za ukombozi. Inasemekana jaribio hili la pili lilikuwa na mkono wa Oscar Kambona. jaribio # 3, liliwahusisha wakina Lugangira,Hatibu Gandhi, Zacharia Hans Pope, etc etc.

@Mzee Mwanakijiji,

..serikali ya Mwalimu Nyerere ilichelewa ktk utekelezaji wa zoezi la Africanization kwa upande wa jeshi.

..hiyo ilipelekea askari wa ngazi za NCO kuanza vurugu za kuwakataa maofisa wa Kizungu waliokuwa wakiongoza jeshi.

..kiongozi wa maasi hayo alikuwa Sgt.Hingo Ilogi. sasa kuna wakati Sgt.Hingo Ilogi na wenzake walikwenda mpaka Ikulu kwa nia ya "kuonana" na Mwalimu Nyerere.

..inasemekana walipofika[Hingo Ilogi & Co] ikulu walikutana na aliyekuwa mkuu wa usalama wa taifa, Emilius Mzena, ambaye alitumia ujanja na kuwadanganya kwamba Mwalimu alikuwa hayuko Ikulu. kuna wanaodai kitendo cha Mzena ndiyo kilimuokoa Mwalimu kwasababu maana baada ya hapo alipelekwa mafichoni.

..kwa mtizamo wangu, askari toka Uingereza ndiyo waliookoa jahazi, vinginevyo tungekuwa tunaongea habari nyingine kabisa hapa.

NB:

..kuna mwana JF anaitwa Shwari, huyu huwa ni msaada mkubwa sana ktk masuala ya kihistoria kama haya.
 
Baadhi ya nyaraka kuhusu mauaji yake.

Nyaraka kuhusu Malcolm X na mauaji yake pia hazijawekwa zote wazi

Kwa uchache

I remember nilishawahi kuangalia documentary moja kuhusu oswald.., alleged JFK killer, walisema jamaa alikua socialist na alikua na link na cuba..,

nadhani wakumbuka JFK alikufa baada ya vuguvugu la "cuban missile crisis"
 
Baadhi ya nyaraka kuhusu mauaji yake.

Nyaraka kuhusu Malcolm X na mauaji yake pia hazijawekwa zote wazi

Kwa uchache

that is too general; kusema "baadhi ya naraka kuhusu mauaji yake" zina assume kuwa zipo. Kwa mfano nyaraka gani ambazo wametaka kuziona au zinajulikana kuwa zipo na hazijatolewa hadharani baada ya kipindi cha kisheria cha kuwa classified kupita?
 
Kuna nyaraka zinazohusiana na mazungumzo ya simu ya Malcolm X na watu wanaohusiana nae.

Zipo na hazijawekwa wazi licha ya watafiti kuziomba tena na tena.
 
Kuna nyaraka zinazohusiana na mazungumzo ya simu ya Malcolm X na watu wanaohusiana nae.

Zipo na hazijawekwa wazi licha ya watafiti kuziomba tena na tena.

terms za classification ya hizo documents ni nini? au ni sababu gani inatolewa ya kutoziweka hadharani?
 
Kuna nyaraka zinazohusiana na mazungumzo ya simu ya Malcolm X na watu wanaohusiana nae.

Zipo na hazijawekwa wazi licha ya watafiti kuziomba tena na tena.

Kina nani hao watu wanaohusiana naye na hayo mahusiano ni ya kivipi na ni watafiti gani wameziomba tena na tena hizo nyaraka na hawakuzipata? Bwana Marables ni mmoja wao?:)
 
Back
Top Bottom