Jaribio la kuiba silaha JWTZ Bohari kuu Gongo la Mboto

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
JWTZ v/s Polisi:

Nimefahamishwa kuwa, askari walioavalia sare za JWTZ walishuka kwenye lori lao na ‘kumlabua' askari aliyekuwa akiongoza magari kwenye eneo la Ubungo, Dar es Salaam kwa kuwachelewesha kwenye foleni kwa muda mrefu.

Taarifa kutoka chanzo kingine cha habari zikaongeza kusema kuwa Wanajeshi waliohusika ‘kulabua' walikamatwa baadaye katika eneo la Ilala na sasa wapo rumande.

Jaribio la kupora silaha:

Kwa mujibu wa GPL, mtu mmoja anaedaiwa kuwa ni jambazi wakiwa na wenzake waliingia katika kambi ya JWTZ 511 KJ bohari kuu ya kijeshi iliyopo Gongo-la-Mboto jijini Dar es Salaam kwa lengo la kupora silaha. Kulizuka purukushani baina ya majambazi hayo, askari waliokuwa ulinzi ndani ya kambi hiyo na raia, purukushani ambayo ilimtoa uhai jambazi mmoja.
 
Sio vizuri kuwapiga, lakini kusema ya ukweli polisi trafiki wanaboa sana mida ya jioni katika mataa ya ubungo! wala hawako fear kabisa kwa watumiaji wa barabara za Mandela na Sam Nujoma wao akili zao ni Morogoro road tu ndio kuna magari mengi, I really hate this!!!
 
nngu007 wafuasi wa ponda wakisikia kuwa wajeda wamewekwa rumande itawapa morari wa kupambana nao siku yoyote wakiletwa mtaani kudhibiti "program" yao.
kama vipi akamatwe na ighondu wa ikulu. ova!
 
Last edited by a moderator:
Sio vizuri kuwapiga, lakini kusema ya ukweli polisi trafiki wanaboa sana mida ya jioni katika mataa ya ubungo! wala hawako fear kabisa kwa watumiaji wa barabara za Mandela na Sam Nujoma wao akili zao ni Morogoro road tu ndio kuna magari mengi, I really hate this!!!

Jamani hebu angalia na upande wa pili. Ile kazi ya kuongoza magari si ndogo na rahisi kama tunavyodhani. Makosa ya kujisahau na kuruhusu upande mmoja kwa muda mrefu si sababu ya kuwachukia hawa askari waongozaji ni kiasi cha kuwaelimisha tu! Kwa pale ubungo wanaokoa sana jahazi, hebu jaribu kuwaambia siku moja waache kuongoza magari tutegemee taa tu utaona balaa lake.
 
hao ni majambazi au uamsho?semeni jamani ,duniani yanatokea sana haya.Hata askari wa afghanistani na pakistani wenye mapenzi na talibani huwa imani yao huwatuma kufanya kazi ya magaidi ndani ya vituo vya kijeshi.kama kuna viongozi wa serikali la zenj wana mapenzi na uamsho kwanini askari nao wasiopo wanaompenda sana Ponda na iamni yake?
 
Jamani hebu angalia na upande wa pili. Ile kazi ya kuongoza magari si ndogo na rahisi kama tunavyodhani. Makosa ya kujisahau na kuruhusu upande mmoja kwa muda mrefu si sababu ya kuwachukia hawa askari waongozaji ni kiasi cha kuwaelimisha tu! Kwa pale ubungo wanaokoa sana jahazi, hebu jaribu kuwaambia siku moja waache kuongoza magari tutegemee taa tu utaona balaa lake.

Wabongo, wabongo, wabongo!!! Teknolojia ya kisasa ya mataa ya kuongoza magari ipo tele - mataa yanakuwa programmed kufuatana na hali halisi ya trafiki kwa wakati husika. Haya ya kusema askari wanaokoa sana jahazi ni fikra za karne ya ishirini kam sio karne ya 19. Serikali ya jiji au hata ya taifa (kwa vile Dar inaonekana kama ndio Tanzania yote) inao uwezo wa kifedha wa kuinunua teknolojia hiyo kama wahusika wangekuwa wanatumia vichwa vyao badala ya kutumia 'meya wa jiji'!!:sad:
 
Tatizo kubwa viongozi wetu,ni watawala wasiotaka kusikiliza ushauri wa wataalam,na kufanya maamuzi kwa wakati sahihi !
 
Jamani hebu angalia na upande wa pili. Ile kazi ya kuongoza magari si ndogo na rahisi kama tunavyodhani. Makosa ya kujisahau na kuruhusu upande mmoja kwa muda mrefu si sababu ya kuwachukia hawa askari waongozaji ni kiasi cha kuwaelimisha tu! Kwa pale ubungo wanaokoa sana jahazi, hebu jaribu kuwaambia siku moja waache kuongoza magari tutegemee taa tu utaona balaa lake.

wajibu wao ni nini hasa!!!! wao ndo askari wa usalama barabarani lazima watekeleze wajibu wao kwa uweredi wa hali ya juu, siyo fear kuruhusu tu magari ya upande mmoja na kuacha magari ya pande nyingine yakisota kwenye foleni kwa muda mrefu; tutawaelimisha mpaka lini??? hiyo ndiyo kazi waliyochagua lazima waifanye kwa weredi kabisa....inatia hasira kuona Afande mzima anafanya upuuzi kwenye mataa wakati watu wote nia yao ni moja ya kuwahi.
 
JWTZ v/s Polisi: Nimefahamishwa kuwa, askari walioavalia sare za JWTZ walishuka kwenye lori lao na ‘kumlabua’ askari aliyekuwa akiongoza magari kwenye eneo la Ubungo, Dar es Salaam kwa kuwachelewesha kwenye foleni kwa muda mrefu. Taarifa kutoka chanzo kingine cha habari zikaongeza kusema kuwa Wanajeshi waliohusika ‘kulabua’ walikamatwa baadaye katika eneo la Ilala na sasa wapo rumande. Jaribio la kupora silaha: Kwa mujibu wa GPL, mtu mmoja anaedaiwa kuwa ni jambazi wakiwa na wenzake waliingia katika kambi ya JWTZ 511 KJ bohari kuu ya kijeshi iliyopo Gongo-la-Mboto jijini Dar es Salaam kwa lengo la kupora silaha. Kulizuka purukushani baina ya majambazi hayo, askari waliokuwa ulinzi ndani ya kambi hiyo na raia, purukushani ambayo ilimtoa uhai jambazi mmoja.
Hilo la kwanza la askari trafiki kupigwa na JWTZ nililiona kwa macho yangu nikiwa ndani ya bus mita chache kutoka kwenye mataa. Plikuwa na malori ya jeshi na la kwanza lilikuwa na askari lakini mengine matano au sita yalifunikwa na turabai. Palikuwa na magari mengine mawilimatatu kati ya gari la kwanza na la pili la jeshi na gari la kwanza lilipèita na kusimama mbele kidogo ya askari,inaelekea walikuwa hawajapata ruhusa ya kupita.Tulishuhudia wakishuka kwa kasi na kuanza majibishano na trafiki na mara mtama mara ngumi.Trafiki Yule aliokolewa na askari wenzie na raia (au askari kanzu).Baada ya pale lori lao lilianza kuondoka mwendo mdogo na wao wakiwa wakimbilia na kuruka huku wakishangiliwa.Malori yaliyofuata yalitulia na kufuata muongozo wa trafiki kabla ya kuelekea buguruni. Nilishanga nikiwa ndani ya bus hata kabla ya kufika Kibaha watu walishap post hapa JF
 
Wabongo, wabongo, wabongo!!! Teknolojia ya kisasa ya mataa ya kuongoza magari ipo tele - mataa yanakuwa programmed kufuatana na hali halisi ya trafiki kwa wakati husika. Haya ya kusema askari wanaokoa sana jahazi ni fikra za karne ya ishirini kam sio karne ya 19. Serikali ya jiji au hata ya taifa (kwa vile Dar inaonekana kama ndio Tanzania yote) inao uwezo wa kifedha wa kuinunua teknolojia hiyo kama wahusika wangekuwa wanatumia vichwa vyao badala ya kutumia 'meya wa jiji'!!:sad:

Meanwhile kabla serikali haijaamua kutumia akili waheshimu na uwape ushirikiano wako askari hao...
Natanguliza shukrani.
 
Majambazi wameenda kuiba silaha kwenye bohari ya jeshi?
Labda walikuwa wanajeshi!
 
Hii habari hata sieelewi!mbona ki kashfa kubwa sana kwa majambazi kuvamia armoury?haiwezekani wataingiaje kambini na kutaka kuiba!
 
JWTZ v/s Polisi:

Nimefahamishwa kuwa, askari walioavalia sare za JWTZ walishuka kwenye lori lao na ‘kumlabua' askari aliyekuwa akiongoza magari kwenye eneo la Ubungo, Dar es Salaam kwa kuwachelewesha kwenye foleni kwa muda mrefu.

Taarifa kutoka chanzo kingine cha habari zikaongeza kusema kuwa Wanajeshi waliohusika ‘kulabua' walikamatwa baadaye katika eneo la Ilala na sasa wapo rumande.

Jaribio la kupora silaha:

Kwa mujibu wa
GPL, mtu mmoja anaedaiwa kuwa ni jambazi wakiwa na wenzake waliingia katika kambi ya JWTZ 511 KJ bohari kuu ya kijeshi iliyopo Gongo-la-Mboto jijini Dar es Salaam kwa lengo la kupora silaha. Kulizuka purukushani baina ya majambazi hayo, askari waliokuwa ulinzi ndani ya kambi hiyo na raia, purukushani ambayo ilimtoa uhai jambazi mmoja.

Tusijidanganye,kama mabomu yalipigwa NAIROBI NA DAR,kwa wakati mmoja mwaka 1998,sasa TUJUFUNNZE kuwa unapoona mwenzako ananyolewa wewe tia maji[mombasa kuna matitizo na vurugu muda sasa,lakini Tanzania Serikali ilkuwa inapuuza dalili zote zenye kuashiria machafuko]

Inawezekana Tanzania tayari vikundi vya hatari vipo[kwani hata Pakstani,huwa vikundi hivi huvamia hata gwaride lajeshi na kufanya hujuma].makini

TUKIO LA KUVAMIA KAMBI YA JESHI LISIPUUZWE,jeshi na Taasisi za serikali zianze kuchukua TAHADHARI.!!!!!
 
Sio vizuri kuwapiga, lakini kusema ya ukweli polisi trafiki wanaboa sana mida ya jioni katika mataa ya ubungo! wala hawako fear kabisa kwa watumiaji wa barabara za Mandela na Sam Nujoma wao akili zao ni Morogoro road tu ndio kuna magari mengi, I really hate this!!!

Solution hapo ni kufunga smart traffic light basi,toa hao traffic police
 
Back
Top Bottom