Mazoezi ya kijeshi ya JWTZ yazua taharuki Dar

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,079
Milio mizito ya mizinga, ngurumo za vifaruv yatikisa
headline_bullet.jpg
Msemaji wa jeshi : Ni mazoezi ya kawaida kabisa



membe(7).jpg

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe


Mazoezi ya kijeshi yaliyofanywa usiku wa manane kuamkia jana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), yalizua taharuki kubwa miongoni mwa wananchi wanaoishi jirani na kambi ya Vifaru ya Kiluvya nje kidogo ya jiji la Dar e s Salaam.

Mazoezi hayo yanayoonekana kufanywa kwa udharura, yameleta wasiwasi mkubwa kwa wananchi kutokana na vishindo vikubwa vilivyo kuwa vikisikika mithili ya radi huku mingurumo ya vifaru ikisikika kwa nguvu.

Wakati mazoezi hayo yakifanyika, mvua ilikuwa ikinyesha na umeme katika makazi ya watu ulikatika na kuzidi kusababisha hofu kubwa.

Askari wa kambi hiyo walifanya mazoezi ya kushitukiza usiku wa kuamkia jana ikiwa ni pamoja na kuzijaribu zana zao nzito kama vile mabomu na mizinga ya kurushwa kwa vifaru huku ikitoa milio mizito.

Vishindo hivyo vya majaribio ya silaha hizo nzito vilisababisha wananchi wanaoishi jirani na kambi hiyo wakiwemo wa Kiluvya, Kibamba na maeneo ya Mbezi, kupatwa na taharuki huku wakikumbushwa milipuko ya mabomu ya kambi za Mbagala na Gongo la Mboto yaliyosababisha vifo vya watu wengi na uharibifu mkubwa wa mali.

Wakazi wengi wa maeneo hayo walilazimika kutoka nje ya nyumba zao na familia zao huku wakiwa hawajui hatma yao huku wengine wakizungumza kwa tahadhari wakiwa wamefunga nyumba zao na kukaa maeneo ya wazi huku wakifanya mawasiliano na ndugu zao walio nje ya maeneo hayo.

Akizungumza na gazeti hili jana, Msemaji wa JWTZ , Kanali Kapambala Mgawe, alisema mazoezi hayo ni ya kawaida kabisa.

“Huwa yakifanyika tunatoa taarifa, haya ya jana taarifa zilitolewa kwa wananchi wale wa jirani sana lakini kwa kuwa mazoezi yenyewe yalifanyika usiku, kelele zilisikika mbali sana tofauti kama mazoezi yangefanyika mchana,” alisema.

Wasiwasi mkubwa uliwakumba wananchi kufuatia kauli za serikali bungeni dhidi ya chokochoko zinazofanywa na nchi jirani ya Malawi ya kugombea mpaka katika ziwa Nyasa.

Pamoja na serikali kusisitiza kuwa jeshi limejiandaa kwa lolote litakalotokea nchini Malawi, Kanali Mgawe alisema mazoezi hayo hayahusiani na chokochoko za Malawi.

Mwanzoni mwa wiki hii, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, aliionya Serikali ya Malawi juu ya utata wa mpaka uliopo katika Ziwa Nyasa kati ya Tanzania na nchi hiyo na kusisitiza kuwa Serikali ya Malawi hairuhusiwi kutumia eneo la mpaka unaogombaniwa hadi mwafaka utakapopatikana.

Alisema tatizo hilo ni la muda mrefu ambapo Malawi wanadai Ziwa lote Kaskazini ya Msumbiji kuelekea Ruvuma na Mbeya ni mali yao kwa mujibu wa Mkataba wa Heligoland uliowekwa saini Julai mwaka 1890.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, Edward Lowassa, naye alitoa msimamo wa kamati yake na kusisitiza kuwa JWTZ wako tayari kwa lolote ingawa aliomba Mungu kuepusha kutokea kwa vita na badala yake suala hilo liamuliwe kwa njia ya kidiplomasia.

Msimamo huo wa serikali umekuja baada Serikali ya Malawi kutoa kandarasi kwa kampuni kadhaa za kigeni zinazoendesha utafiti wa mafuta na gesi katika eneo la ziwa Nyasa linalogombaniwa na pande hizo mbili.

Ndege za kuangaza katika mipaka ya baharini zimeripotiwa kuzunguka mara kwa mara katika eneo la ziwa hilo kwa kile Tanzania inachokiita ukiukwaji wa makubaliano ya pande zote mbili.

Wakati Serikali ya Tanzania ikiweka tishio hilo, serikali ya Malawi kupitia Waziri wake wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Ndani, Uladi Mussa alisema Watanzania hawana mamlaka ya kuzuia utafiti wa mafuta uliokuwa ukiendelea katika ziwa hilo na kwamba shinikizo la Tanzania likiendelea watalazimika kwenda katika mahakama ya kimataifa.






CHANZO: NIPASHE

 
Hivi kwanini hizi kambi za kijeshi zijengwe karibu kabisa na maeneo ya makazi ya raia? Anyway yawezekana kwa upande mwingine raia kujenga karibu na kambi hizo kwa maana ya kambi kutangulia kujengwa. Nafikiri serikali yetu ingeweka mikakati ya kambi za jeshi kuwa mbali kabisa na raia ili kuepusha usumbufu.
 
Ni wananchi wanazifuata kambi za jeshi, nyingi ziko zilipo tangu 1970 au kabla, ni strategic areas in case of anything.
 
Hiyo ni jamba jamba ya kutisha Malawi nini? Angalia hiyo mibomu isijelipuka hata kabla ya kutupwa Malawi ikamaliza watu wetu kama ilivyotokea kule Mbagala na Gongo la Mboto. Mikambi ya kijeshi katikati ya jiji ya nini? Si muipeleke mipakani hasa Musoma kule wanapomalizana wenyewe kwa wenyewe wakigombea bangi. Wanchale na Wanchoka wanafaa kupelekewa mikambi ya kijeshi ili isaidie kurejesha amani baina yao.
 
Hivi kwanini hizi kambi za kijeshi zijengwe karibu kabisa na maeneo ya makazi ya raia? Anyway yawezekana kwa upande mwingine raia kujenga karibu na kambi hizo kwa maana ya kambi kutangulia kujengwa. Nafikiri serikali yetu ingeweka mikakati ya kambi za jeshi kuwa mbali kabisa na raia ili kuepusha usumbufu.



hakuna kambi ya jeshi iliyojengwa eneo la raia . ni raia ndio wamezifuata kambi za jeshi. na wengi wao ni ndugu za wanajeshi au wanajeshi wastaafu. utafutwe ufumbuzi makini ......
 
mimi sioni ubaya wa kuwepo hizi kambi za jeshi hapa mjini ila sehemu za kufanyia mafunzo kama haya na maghala ya silaha yawe mbali na mjini, ukiangalia kipindi cha mbagala mabomu yalifika hadi kiwalani na gongo la mboto yalifika hadi mbezi shamba. Namalizia kwa kusema hapa mjini si mahali pazuri kwa haya mnayoyafanya sasa.
 
wakafanye mazoezi mpakani na ziwa nyasa ili mkwara wao usikike vizuri au wanawaogopa wanyasa ndo maana wanafanyia mbali.
 
mimi sioni ubaya wa kuwepo hizi kambi za jeshi hapa mjini ila sehemu za kufanyia mafunzo kama haya na maghala ya silaha yawe mbali na mjini, ukiangalia kipindi cha mbagala mabomu yalifika hadi kiwalani na gongo la mboto yalifika hadi mbezi shamba. Namalizia kwa kusema hapa mjini si mahali pazuri kwa haya mnayoyafanya sasa.

Kila kambi ya jeshi ina kitu tunaita armourer(ghala la silaha) na la mabomu.., haya ni kwa ajili ya ulinzi wa kambi husika na eneo husika wakati wa hali ya hatari, kama hostility(war) inakua more violent silaha nzito na mabomu husika yatasafirishwa kutoka mahali yanapofichwa na kusogezwa karibu na eneo la vita.., yale mabomu ya mbagala ni kamzigo tu ka kuilinda ile kambi na sehemu ya dar es salaam, maana kambi huwa zinawekwa strategically.., dar na mkoa wa pwani inalindwa kutoka pande nne, kaskazini, kusini, mashariki na magharbi.., kwhy kambi zimekaa namna hyo na silaha zilizopo hapo ni justified kuwepo hapo..,

Exceptionally, 511kj(gongo la mboto) pale ni entry point ya baadhi ya silaha, kwhy sometimes silaha (mizinga, mabomu, makombora) pale zinakua nyingi na nzito zaidi zikisubiri kwenda zinapohitajika kufichwa..,

Kambi zote za jeshi zinajengewa uwezo wa kuhimili shambulizi la adui hata kama la ghafla kwa muda wa kutosha ili ikisubiriwa nguvu ya ziada kusaidia.., kwhy huwezi kukwepa kuwa na mabomu na silaha nyepesi, za kati na nzito kwa baadhi ya kambi za mijini eg dar
 
Back
Top Bottom