Japo Hakuna Kazi za Kike na za Kiume, Lakini Utangazaji Mpira Redioni, Ni Mwanamke Mmoja Tu Tanzania, Halima Mchuka.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,507
113,629
Wanabodi
Kuna huu msemo, "Everything a man can do, a woman can do", kumaanisha hakuna kazi za kike na za kiume, kila kazi inayofanywa na mwanaume, inaweza kufanywa na mwanamke.

Moja ya kazi rahisi sana ni kazi ya utangazaji, ila inahitaji kipaji. lakini kwa upande wa utangazaji wa mpira wa miguu redioni, mpaka sasa kwa hapa nchini Tanzania, tumewahi kuwa na mtangazaji mwanamke mmoja tu aliyetangaza Mpira.

Mtangazaji huyu, the one and only ni, Halima Mchuka, aliyefariki miaka 10 iliyopita na viatu vyake havijapata mrithi hadi leo!.

Leo ni kumbukumbu ya miaka 10 ya kifo cha Halima Mchuka.

RIP Halima Mchuka, Shujaa wa kwanza wa Utangazaji Mpira kwa Mtangazaji Mwanamke Tanzania.
P.
 
Nakubaliana na wewe, hakutatokea sports lady kama Halima Mchuka!! Those days RTD was🔥🔥🔥
 
Kwanini hukuweka kwenye jukwaa la michezo, anyway umeeleweka pia.

Binafsi naanza kuamini hawa mamazetu wakubali tu kwamba kuna baadhi ya kazi wangetuachia wanaume tu, maana hata wanapopata hizo kazi bado wanahitaji support kutoka kwa mwanaume.

Mungu ni fundi sana once akitengeneza kitu humans can't fabricate.

late me end up over here!.
 
Domina Kinyaiya wa Bomba FM ni analyst mzuri sana wa mpira nadhani pia anaweza kuja kuwa mtangazaji mzuri.
Uchambuzi wake ni mzuri kuliko wa wapiga kelele wa Clouds.
 
Huku Halima Mchuka, huku Ezekiel Marongo hahaaa. Hapo nimekaa pembeni na mze tunasikiliza akina Ally Mayai wakifanya yao uwanjani.

Shit, nimezeeka sasa!
Binafsi Si Halima Mchuka wala Ezekiel Marongo niliwahi mkubali kwenye utangazaji wa Kandanda, Marongo huyu ndo alikuwa debe tupu, zaidi alikinogesha mno Kipindi cha michezo ile saa moja na Nusu Jionii utasikia Fundi mitambo ni Joseph Kambangwa

Kwa kizazi changu kipindi Azam Tv hawajaja niliwapenda mno na kuwakubali wafuataoo:-

1. Jesse John

2. Sued Mwinyi (ule msauti wake Dah)

3. Juma Nkamia

Zamani hukoo tuliambiwaa walikuwepo wakina...

Salim Mbonde
Ahmed Jongo
Nazir Mayoka
Dominic Chilambo
(Mechi za Pamba aiseee)
Charles Hillary

Apumzkee kwa Amaniii Halima Mchuka Sauti yakee ilikuwaaa Nzurii mnoooo
 
Back
Top Bottom