Mtanzania Huru
Member
- Apr 20, 2011
- 28
- 29
January, Maharage, Yakubu: Mapacha watatu na dada yao waliojimilikisha sekta ya nishati ya Tanzania
Na Mwandishi Maalumu
January Makamba, Maharage Chande na Saidi Yakubu ni maswahiba wa karibu sana, kiasi ambacho unaweza kuwaita ni mapacha watatu.
Mapacha hawa watatu wamekuwa pamoja kwenye shida na raha kwa miaka mingi sasa.
Wamekuwa pamoja kwenye shida wakati wa awamu iliyopita walipokuwa nje ya mfumo.
Na sasa hivi wako pamoja kwenye raha kwenye awamu hii wakiwa ndani ya mfumo.
Kwa sasa January ni Waziri wa Nishati, Yakubu ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Maharage ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO.
Alipoteuliwa tu kuwa Waziri wa Nishati, January alihakikisha kuwa anawaweka karibu mapacha wenzake Maharage na Yakubu.
Jambo la kwanza alilofanya January ni kupendekeza kwa mamlaka ya uteuzi kuwa rafiki yake wa karibu Maharage ateuliwe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO.
Mapacha hao watatu wanashiikiana na dada wa January, Mwamvita, kupanga madili yote kwenye taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati.
Yakubu husafiri kwenda Afrika ya Kusini mara kwa mara kukutana na Mwamvita Makamba kupanga namna ya kuchota pesa zaidi kwenye sekta ya Nishati ya Tanzania.
MGODI WA TANESCO
TANESCO ni taasisi kubwa kuliko zote nchini, yenye maelfu ya wafanyakazi na mapato ya zaidi ya shilingi trilioni 1 kwa mwezi.
Kwa kumweka rafiki yake wa karibu Maharage kama Mkurugenzi Mkuu, January ni kama vile amejimilikisha MGODI unaotema Shilingi trilioni 1 kwa mwezi.
Kandarasi, tena na manunuzi yote makubwa ya TANESCO sasa hivi lazima yapite kwa January kwa kuwapa kazi watu anaowachagua yeye.
Taasisi nyingine kubwa chini ya Wizara ya Nishati, ikiwemo TPDC, EWURA na REA nazo zimekuwa zinatumiwa kama migodi binafsi na mapacha hao watatu kujichotea pesa za umma.
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali seeikalimi zinasema kuwa kwa hakika mapacha hao watatu sasa wameiteka sekta yote ya nishati.
Mapacha hao watatu pia wameingiza makuvha yao kwenye miradi mikubwa nchini ikiwemo mradi wa JNHPP na mradi wa LNG.
January na Maharage wanahakikisha kuwa mapacha mwenzao, Yakubu, anapewa tenda kubwa za kisheria kupitia kwa kampuni yake binafsi ya uwakili ya Yakubu & Associates Chambers.
January na Maharage wamehakikisha kuwa TANESCO wanatoa tenda kadhaa kubwa za huduma za kisheria kwa kampuni ya Yakubu kwa mabilioni ya shilingi ambazo mapacha hao watatu wanagawana.
Bodi ya TANESCO chini ya Mwenyekiti Omar Issa ambayo ina wajumbe vigogo ikiwemo mtoto wa Mzee Bakhresa, Aboubakar Bakhresa, imegeuka kuwa boya kwani maamuzi yote hufanywa na January na Maharage.
Bodi ipo kama haipo kutokana na kila mtu kujua kuhusu urafiki wa karibu wa January na Maharage na hao wawili ndiyo hufanya maamuzi yote yanayohusu shirika.