Jana nimekatwa shilingi 1500 nikinunua umeme baada ya shilingi 1ooo hii 500 imeongezeka lini?

SAUTI YAKO

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
2,923
2,003
Tangu zoezi lianze miaka michache iliyopita nimekuwa nikikatwa elfu moja,lakini jana ikakusanywa 1500 bila maelezo hiyo 500 imeongezekaje.

Sijajua kwenu wakuu imekuaje pia kama mmekutana na ongezeko hilo.Mamlaka husika imeshawahi ongelea ongezeko hilo na hiyo tsh 500 inaenda kumfanyia nini mwananchi,je imekaaje kisheria kuchukua hela ya mtu bila kumfahamisha kuwa kuna hilo ongezeko?

Wajuzi wa mambo wenye uelewa mkubwa ninaomba msaada wenu,maana nilitaka kama mwenezi angekuwa hajapita huku niliko ningetokea kwenye mkutano hawaite wahusika wajieleze maana yeye ndiye anao uwezo wa kufumbua mafumbo now days
 
Utaratibu wameweka wao,kwa sababu wanazojua wao. Mara ya kwanza ya kununua umeme kila mwezi,lazima 1500 wachukue.
Hapo ukinunua tena,utapata units zako safi. Ila mwezi wa 3 tena, mara ya kwanza utakayonunua,hivyo hivyo.
Ngoja wa usafi nae aje
Subiri wa ulinzi nae apite.

Hiyo pesa kulitakiwa kuwepo utaratibu au mfumo,wa wenye nyumba kulipa,kuliko kulipiwa na wapangaji
 
Hata mimi nimeona mkuu; debt collected: 1500
Nilijua niko mwenyewe mkuu,je hatuwezi pata msaada wa kisheria kwa hili walolifanya bila kuutangazia umma kwanza.Watanzania tunapelekwa tu watu wanavyojisikia wakiamka leo tufanye hivi wanafanya.Ninaomba itv waliweke hili kwenye kipima joto sauti zipazwe.tuna mizigo mingi sana sasa hivi mifumuko ya bei bado tunazidishiwa tu mizigo
 
mbona mwigulu toka mwaka jana alitangazaa bungeni na makofii yakapigwaa ya kutosha na wabunge wotee
...!!
Mkuu tuwekee kumbukumbu ya tangazo hilo inawezekana taarifa ilitangazwa lakini haikufanyika juhudi ya kutosha kuwafikia watumiaji wengi .mwanzo walivyotangaza tutaanza kukatwa elimu ilitolewa sana tukaridhika
 
Nilijua niko mwenyewe mkuu,je hatuwezi pata msaada wa kisheria kwa hili walolifanya bila kuutangazia umma kwanza.Watanzania tunapelekwa tu watu wanavyojisikia wakiamka leo tufanye hivi wanafanya.Ninaomba itv waliweke hili kwenye kipima joto sauti zipazwe.tuna mizigo mingi sana sasa hivi mifumuko ya bei bado tunazidishiwa tu mizigo
Haukuwa makini tu ila zoezi lilianza toka mwaka jana, wanakata 1,500 na jumla ni 18,000 badala ya 12,000 kwa mwaka. Ndio mmasema kodi ya ardhi/pango(?)
 
Wewe Ni mgeni hapa mjini? Walipoambiwa wale kwa kamba zao kila mwezi wanarefusha kamba.
Kwa taarifa yako juzi juzi wameongeza urefu wa kamba kwenye nauli.
Wanakamua Hadi ng'ombe atoe damu.
 
Tangu zoezi lianze miaka michache iliyopita nimekuwa nikikatwa elfu moja,lakini jana ikakusanywa 1500 bila maelezo hiyo 500 imeongezekaje.
Sijajua kwenu wakuu imekuaje pia kama mmekutana na ongezeko hilo.Mamlaka husika imeshawahi ongelea ongezeko hilo na hiyo tsh 500 inaenda kumfanyia nini mwananchi,je imekaaje kisheria kuchukua hela ya mtu bila kumfahamisha kuwa kuna hilo ongezeko?
Wajuzi wa mambo wenye uelewa mkubwa ninaomba msaada wenu,maana nilitaka kama mwenezi angekuwa hajapita huku niliko ningetokea kwenye mkutano hawaite wahusika wajieleze maana yeye ndiye anao uwezo wa kufumbua mafumbo now days
maisha yamepanda kwa viongoz wameona waongeze wakabiliane na ugumu wa maisha. mkuu hupendi watawala waish kwa raha mustarehe?
 
Haukuwa makini tu ila zoezi lilianza toka mwaka jana, wanakata 1,500 na jumla ni 18,000 badala ya 12,000 kwa mwaka. Ndio mmasema kodi ya ardhi/pango(?)
Hapo nimeelewa mkuu kweli nakiri sikuwahi kuipata hii maana ni mwezi huu ndio nimeanza kukatwa 1500 mwaka jana ililkuwa tsh 1000
 
Back
Top Bottom