Jamani tuna standard price kwenye hii bidhaa au kila mtu anajipangia tu

Optimistic Soul

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
204
21
Nimeshawahi kunywa soda mitaa tofauti tofauti nikapata bei tofauti, pengine wanauza Tsh.500, sehemu nyingine nlikuta Tsh.600 japokua kwenye kizibo imeandikwa Tsh.450 nikashindwa kuelewa kabisa hawa jamaa wa hivi viwanda (cocacola na pepsi) wanatupa bei gani, na wanajua soda zao mtaani zinauzwa bei gani? wachukue mfano wa sigara zilipandishwa bei ila kampuni ya sigara ilibandika mabadiliko ya bei kila kona.
Au wanaJF hamjakumbana na jambo hili? nazungumzia mtaani sio zile sehemu ambazo wanauza soda 1,000 au 2,000 makusudi wakijumuisha pamoja na bei za furniture kwenye soda.
 
Back
Top Bottom