Jamani rorya, rorya, rorya na hatima yake!!!

JACADUOGO2.

JF-Expert Member
Dec 13, 2010
930
217
Inasikitisha, inashangaza, inahuzunisha na kutia huruma katika nchi ambayo inadaiwa kuwa ni ya kidemokrasia kama Tanzania kufanya mambo ya aibu chini ya uongozi wa CCM bila ya kiongozi wa taifa la Jamhuri ya Muungano rais Jakaya Mrisho Kikwete kukemea! Kwa kweli inasikitisha na inapunguza imani ya wananchi kwa viongozi wao na suala la ufisadi linazidi kudhihirika wazi miongoni mwa viongozi wetu. Tunawaomba mtambue wazi kuwa watanzania tuna akili timamu na tunatambua kila kitu ndani ya taifa hili. Sisi ni watanzania tunatambua wakati uliopita, tunatambua wakati uliopo na tunatazama kwa upeo wa juu wakati ujao. Ifike mahali viongozi wajue umuhimu wa utu wa watanzania au wananchi wao kwa ujumla wake. (Leaders must know the importance of the Tanzanians’ dignity).

RORYA ni miongoni mwa majimbo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yanayosifka kwa mambo mazuri mengi pamoja na mambo mengine mabaya machache kama ilivyoada. RORYA ikiwa ni miongoni mwa majimbo machache yenye maliasili nyingi ikiwa ni pamoja na ziwa Victoria, madini (maeneo ya Kamot karibu na mlima Rorya) na nyingine nyingi. Pamoja na hayo yote RORYA ni miongoni mwa majimbo yaliyo nyuma sana kimaendeleo kwani barabara za jimbo la RORYA hazina kiwango chochote kizuri ikiwa ni pamoja na ukosefu wa lami kwani ndani ya jimbo zima la RORYA hamna barabara ya lami. Ni aibu!!

Mbaya zaidi kuliko yote ni kwamba RORYA inatawaliwa kimabavu, kwa maslahi ya watu wachache (LAMECK AIRO na CHARLES OCHELE) na bila kujali maslahi ya wanarorya. Hii Ni aibu, Ni fedhea, Ni dharau, Ni ujuha, Ni uroho na ni ukosefu wa hekima na busara katika uongozi.

Ni dharau pale ambapo maamuzi ya jimbo la RORYA yanapofanywa na kutawaliwa na mfanyabiasha LAMECK AIRO ambaye amesababisha migogoro mingi na uhasama miongoni mwa Wanarorya kuanzia kipindi alipokuwa diwani wa kata ya Koryo hasa katika harakati ya kutangaza makao makuu ya wilaya ya RORYA ambapo alidiriki kutoa rushwa na kubadilisha sehemu ambapo ilitakiwa iwe ni makao makuu ya wilaya ya RORYA yaani makao makuu kutoka SHIRATI na kwenda kuwekwa porini (Ingri juu) pasipo na kigezo chochote cha ubora katika eneo hilo la Ingri juu tofauti na SHIRATI iliyokuwa na kila kigezo ikiwa ni pamoja na maji (ziwa Victoria), umeme na hata barabara zinazopitika tofauti na Ingri juu ambapo kila kitu kinaanza mwanzo na fedha nyingi kutumika katika ujenzi bila tija wala sababu ya msingi.

Vile vile ni chini ya uwenyekiti wa CHARLES OCHELE wa halmashauri ya wilaya ya RORYA (2005 – 2010) na ushauri wa rafiki yake wa karibu LAMECK AIRO iliyopelekea halmashauri ya RORYA kupata hati chafu kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili.

Hii yote ni shauri ya LAMECK AIRO kukosa elimu, upeo na mtazamo wowote katika fani yoyote katika maisha kwani ni darasa la saba na hajui maana ya elimu kwani katika kampeni zake alidiriki katamka katika kampeni ya kuomba kura ya maoni kuwa “ ELIMU NI KELELE” alipoulizwa kuhusu umuhimu wa elimu kwake.

Katika harakati za kuwania nafasi ya uwenyekiti wa halmashauri ya wilaya RORYA (2010 – 2015) miongoni mwa wana CCM waliochukua fomu ya kuwania nafasi hiyo walikuwa madiwani watano ikiwa ni pamoja na Yamo Odemba Kagose kata ya Rabuor, Ongujo Wakibar kata ya Mkoma, Okeya Ogigo kata ya Nyamtinga, Lukio Ambogo kata ya Nyahongo na Charles Ochele kata ya Roche. Majina hayo yalichujwa hadi makao makuu CCM kama ilivyo kawaida ili kupata majina mawili yatakayopigiwa kura na madiwani wa CCM RORYA ili kupata jina moja litakalopambanishwa na mpinzani. Hata hivyo majina mawili yaliyotoka taifani yalikuwa ni ya Okeya Ogigo kata ya Nyamtinga na Lukio Ambogo kata ya Nyahongo, lakini cha kushangaza ni pale ambapo LAMECK AIRO (Mbunge) alipotoa tamko kwamba yuko tayari kujiuzulu ubunge kutokana na sababu kwamba jina la Ochele halimo miongoni mwa yale majina mawili yaliyotoka taifani na kwamba atarudisha kadi ya CCM na kuwa mwanachama wa kawaida wa CCM. Aibu kwa mbunge wa RORYA, Lameck Airo! Utarudishaje kadi ya chama halafu uwe mwanachama wa kawaida? Ajabu!

Kimsingi mbunge huyu hajui kwamba ukisharudisha kadi ya chama huwezi tena kuwa mwanachama wa kawaida na huwezi kuwa mwanachama wa chama hicho. Je, wananchi wa kawaida ambao wengi wao hata hawajui maana ya uanachama, wao wangesemaje? Na kwa nini ajiuzulu ubunge na kurudisha kadi kama hamna jina la Ochele? Kwani Ochele ni nani na ana nini? Kwani Lameck ni nani na ana nini akijiuzulu? Kwani RORYA ni ya Lameck na Ochele?

Cha kushangaza zaidi na kusikitisha zaidi na hili ni kwa taifa zima, ni pale ambapo katika mazingira ya kutatanisha na kufedhesha taifa la jamhuri ya muungano wa Tanzania ni pale ambapo bila kutarajia jina CHARLES OCHELE lilipokuja tena kuonekana kwamba ni miongoni mwa wanaoenda kupigiwa kura na madiwani wa CCM kuwania nafasi ya uwenyekiti wa halmashauri ya wilaya RORYA wakati majina yaliyotoka taifani jina lake halikuwepo. Hii ikiwa ni pamoja na msimamo wa LAMECK AIRO kuwa jina la Ochele lisipopitishwa anajiuzulu ubunge na kurudisha kadi ya CCM. Swali ni kwamba kwa nini kama jina la Ochele lilishatolewa na kamati kuu kwa nini jina hilo lirudishwe tena na kamati kuu?

ü Kama siyo rushwa na ufisadi ni nini?
ü Kama siyo ukosefu wa uelewa ni nini?
ü Kama siyo kudharau wanarorya ni nini?
ü Kama siyo utawala wa kimabavu ni nini?
ü Kama siyo kupora watu haki yao ni nini?
ü Kama siyo madharau ni nini?
ü Je, kiongozi mkuu wa nchi anasemaje kuhusu haya mazingira ya kifisadi?

Naamini kwamba kila anayefuatilia vyombo vya habari hapa nchini Tanzania anajua wazi madhara ya hayo matukio yaliyotokea RORYA na yaliyosababishwa na LAMECK AIRO. Ikiwa ni pamoja na baadhi ya madiwani wa CCM RORYA kujiuzulu ikiwa ni pamoja na mwenyekiti wa CCM wilaya ndugu, Leonard Yoda. Miongoni mwa madiwani watatu wa jimbo la RORYA waliojiuzulu ni Ongujo Wakibara wa kata ya Mkoma, Lukio Ambogo wa kata ya Nyahongo na Okeya Ogigo wa kata ya Nyamtinga. Wanarorya tunasema Lameck hana sifa yoyote ya kuwa mbunge wa RORYA.

LAMECK AIRO ni miongoni mwa wagombea ubunge waliotumia hela nyingi sana katika kampeni zake kwani hakuwa na uwezo wowote wa kujinadi wala hakuwa na sera, hivyo aliamua kutumia pesa (Rushwa) katika kampeni hadi alipofanikiwa kuwarubuni wananchi na kupata kura za kuchakachuliwa. Alijitahidi kutuma vibaraka wake katika baadhi ya kata za RORYA ili kuwania udiwani lakini kwa bahati mbaya kwake na kwa hao vibaraka wake na bahati nzuri kwetu hao vibaraka wake walishindwa kuhimili mikikimikiki na hatimaye walibwagwa chini. Miongoni mwa hao vibaraka ni pamoja na aliyemuweka kugombea udiwani katika kata ya TAI, ndugu, LAZARO ROJA AKUKU aliyemjengea nyumba na kupewa gari na pesa nyingi zilizotumika kuhonga wapiga kura ndani ya kipindi cha kampeni. Mwingine ni TOPA aliyegombea katika kata ya BUKURA aliyepewa pikipiki na hela. Wote walibwagwa!

Tunawashauri Wanarorya kuwa na tabia ya kusikiliza hoja na sera za wagombea na kuwauliza maswali juu ya mustakabali wa RORYA na Tanzania kwa ujumla, hasa kuwahoji wababaishaji wa sera kama AIRO. Waache tabia ya kumchagua mtu kwa sababu ya pesa zake na kuachana kabisa na ile tabia ya “GONYA” (nifungue). Wajiulize kwamba huo mlungula wanaopewa umetoka wapi na mtoaji (AIRO) ataurudishaje? Wanarorya tubadilike, tuachane na ukale, ukanda na tujali maendeleo ya RORYA

Madhara ya LAMECK AIRO kwa Wanarorya:
1. RORYA kupata hati chafu kwa zaidi ya miaka miwili.
2. Makao makuu kuwa porini(Ingri juu) badala ya Shirati.
3. Madiwani waliochaguliwa na wananchi kujiuzulu kwa sababu yake.
4. Kutotambua umuhimu wa elimu kwa kusema kwamba “elimu ni kelele”
5. Kutoa rushwa ili Ochele awe mwenyekiti wa halmashauri.

Hata hivyo ieleweke kuwa RORYA ni ya Wanarorya na siyo mali ya mtu binafsi kuitumia kama mradi binafsi. Hivyo tunataka mabadiliko ya haraka sana.
.
NB:
Tunaomba kujua kuwa uchaguzi katika zile kata tatu (3) zilizoachwa wazi utafanyika lini? Wananchi tumechoka kusubiri kuanzia DECEMBER 2010 mpaka leo!!!!! Jamani RORYA.

JACADUOGO
WUOD RORYA
 
Katiba ya Tanzania ina mpe kila Mwananchi kuwa na uhuru wa kutoa mawazo yake pasipo kuvunja sheria,na ndicho alichokifanya ndugu yetu..sasa wewe mamlaka ya kumziba mdomo umeyatoa wapi?

Na kama nani? Na unamaslahi gani juu ya Mbunge wa sasa wa Rorya...Mosi tambua kuwa uadilifu na uongozi ulio tukuka aupimwi kwa kiwango cha elimu tu.Pili kuteuliwa kwa makao makuu ya Rorya yamefanyika kiushawishi wa makundi (kundi la Utegi vs Shirati)..hilo pia utaki lisemwe wakati watu walitoleana bastola.

JK ni mtu wa kufata upepo ya wenye nacho hana maamuzi sahahi kwa wakati sahahii na kwa watu sahihii..Hilo alifichiki atauipake rangi ya njano itabaki kuwa nyekundu...Mbunge wetu (Lamek) ameingia kwenye hiyo nafasi potelea mbali ELIMU yake lakini hana sifa ya kuwa kiongozi muadilifu..namaanisha MWADILIFU..Soma, dadisi, tafakari na fatilia.
 
Katiba ya Tanzania ina mpe kila Mwananchi kuwa na uhuru wa kutoa mawazo yake pasipo kuvunja sheria,na ndicho alichokifanya ndugu yetu..sasa wewe mamlaka ya kumziba mdomo umeyatoa wapi?

Na kama nani? Na unamaslahi gani juu ya Mbunge wa sasa wa Rorya...Mosi tambua kuwa uadilifu na uongozi ulio tukuka aupimwi kwa kiwango cha elimu tu.Pili kuteuliwa kwa makao makuu ya Rorya yamefanyika kiushawishi wa makundi (kundi la Utegi vs Shirati)..hilo pia utaki lisemwe wakati watu walitoleana bastola.

JK ni mtu wa kufata upepo ya wenye nacho hana maamuzi sahahi kwa wakati sahahii na kwa watu sahihii..Hilo alifichiki atauipake rangi ya njano itabaki kuwa nyekundu...Mbunge wetu (Lamek) ameingia kwenye hiyo nafasi potelea mbali ELIMU yake lakini hana sifa ya kuwa kiongozi muadilifu..namaanisha MWADILIFU..Soma, dadisi, tafakari na fatilia.

Wana Rorya, wala msilie. Mimi nimo ndani ya CCM uongozi wa juu sana. huyu Airo ameshajadiliwa, ashukuru mungu alipata ubunge. 2015 out.
kuna kijana mdogo msomi ambaye nadhani anaishi marekani, ndiye chaguo la CCM 2015. hachaneni na hawa majambazi, wezi wa ng'ombe weye mitandao ya majambazi. mungu keshasikia kilio chenu
 
Wanatumia Fedha wanazopata kwa Kuwadhulumu wavuvi kwa mikopo ya nyavu za samaki ya kumasikinisha!
 
Wana Rorya, wala msilie. Mimi nimo ndani ya CCM uongozi wa juu sana. huyu Airo ameshajadiliwa, ashukuru mungu alipata ubunge. 2015 out.<br />
kuna kijana mdogo msomi ambaye nadhani anaishi marekani, ndiye chaguo la CCM 2015. hachaneni na hawa majambazi, wezi wa ng'ombe weye mitandao ya majambazi. mungu keshasikia kilio chenu
<br />
<br />
Anasubiriwa anayeishi marekani hakuna vijana wa Rorya wengine zaidi ya huyo? Ha ha ha! Amkeni usingizini andaeni vijana.
 
Back
Top Bottom