Jakaya Kikwete: Rais muungwana anayelipa ubaya kwa wema...

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
Katika Tanzania huru naweza kusema kuwa serikali ya kikwete ndio iliyokumbana na misukosuko panda teremka nyingi na hata kuyumbisha uhai wake kwa wingi kuliko marais wote walotangulia.

Amekumbana na upinzani mkali wa ndani ya chama chake, ndani ya serikali na zaidi kutoka kwa wapinzani wake hasa CHADEMA huku bara na CUF kule Zanzibar.

Lakini ameendelea kula na kucheka nao kana kwamba hakuna kilichotokea... Wapo walosema hawamtambui kama ni rais halali, wengine wakasema wanamnyang'anya uenyekiti wa chama wengine wakasema wamemchoka tu kwa kuwa hajafanya lolote tangu aingie madarakani lakini ameendelea kucheka nao...

Kweli ukubwa ni jalala na daima usilipe ubaya kwa ubaya...
 
Kukaa kimya ni kwa sababu yanayosemwa dhidi yake ni kweli na wapinzani kutaka kuongea nae ni faraja kwake anajua atapata mbinu mpya za kuongoza baada ya kugota na kusalitiwa na wanamtandao wake. Ajipange upya ila mvuto kwa wananchi umekwisha kabisa.
 
Anhekima ya kukupambana na mihemko ya Kisiasa bravo mr president usimvue gamba EL na CHE .
 
Kukaa kimya ni kwa sababu yanayosemwa dhidi yake ni kweli na wapinzani kutaka kuongea nae ni faraja kwake anajua atapata mbinu mpya za kuongoza baada ya kugota na kusalitiwa na wanamtandao wake. Ajipange upya ila mvuto kwa wananchi umekwisha kabisa.

Wapinzani ndio wao wamemtafuta, sasa hapo unapata jibu gani ? ww mwanamke akikutafuta na ukamkaribisha chumbani na mkijifungia unategemea nn ?. Kwa hili ni sawa na cdm kupewa mimba !

Siku zote ukitaka kumuadhibu mtu anayekufanyia ubaya, usilipe kisasi. By the way kwa Rais kulipa kisasi ni hatari kwa amani ya nchi.
 
Time will tell....tusishangae baadae anaweza akaonekana mzuri maana kumbukumbu za wabongo ni fupi sijui tukoje!

Angalia Uganda ya Iddi Amin alivyoua watu hadi kuweka vichwa kwenye friji kwa ajili ya lunch! leo hii kuna watu eti wanammiss na wanamwona bora kuliko Museveni! Sijui uafrika wetu au sijui hali ya hewa inatufanya tuwe hivi...yaani mimi sielewi!
 
Kuna msemo unasema kila kukicha tunaona ni afadha ya jana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Join Date : 21st November 2011
Posts : 12
Rep Power : 0

Karibu jamvini.
Kuna kitu umesahau mkuu nacho ni kuwa inaelekea hajawahi kuanzisha hoja yoyote bali amekuwa akitawala kwa kufuata matukio na kujibu hoja zinazoelekea kwake, au sio?
Na hata hizo chache alizoanzisha zimemgeuka na hazijapata majibu, mfano 'kujivua gamba' na ile ya kusema kuwa 'muungano una matatizo'!
 
Nawaza sana hivi km wakati ule Mwandosya angeachwa kwenye Baraza la Mawaziri leo hii ingekuwaje?

Kdg nitoe machozi siku ile Mwandosya anaapishwa na kubakishwa kwenye Baraza. Ingekuwa Rais mwingine pengine angempuzisha ili aendelee na tiba.

Raisi Kikwete aliona tiba ya Mwandosya ni kumbakisha barazani. Ni ubinadamu wa hali ya juu kwa kweli!
 
Nawaza sana hivi km wakati ule Mwandosya angeachwa kwenye Baraza la Mawaziri leo hii ingekuwaje? Kdg nitoe machozi siku ile Mwandosya anaapishwa na kubakishwa kwenye Baraza. Ingekuwa Raisi mwingine pengine angempuzisha ili aendelee na tiba. Raisi Kikwete aliona tiba ya Mwandosya ni kumbakisha barazani. Ni ubinadamu wa hali ya juu kwa kweli!

Kama alivoamua kumpa Babu Seya na wanae msosi wa bure mpk ziraili awatenganishe na viwiliwili vyao?
 
Nilidhani unazungumzia sual la katiba kumbe mambo ya kupeana ulaji.? Ukoo wa panya huo
 
Nawaza sana hivi km wakati ule Mwandosya angeachwa kwenye Baraza la Mawaziri leo hii ingekuwaje? Kdg nitoe machozi siku ile Mwandosya anaapishwa na kubakishwa kwenye Baraza. Ingekuwa Raisi mwingine pengine angempuzisha ili aendelee na tiba. Raisi Kikwete aliona tiba ya Mwandosya ni kumbakisha barazani. Ni ubinadamu wa hali ya juu kwa kweli!
Wengine mnatutafutia BAN tu.....
 
Back
Top Bottom