Jaji Mihayo: Rais Magufuli sio Dikteta

Madikteta wote hutetewa na watu wao kabla hata kujitetea mwenyewe kama alivyofanya Magufuli.
 
Sijui kama hii ni JF au ni fb. Mkuu fungua dictionary usome maana ya dictator. Ku dictate ni kutoa amri na hiyo amri ndo sheria. Kiswahili wanaita utawala wa kiimla. Yaani hakuna sheria. Amri ya Mkuu wa nchi ndo sheria. Hatuna rais wa aina hiyo kwa sasa apa africa
 
Jaji Mihayo, usiingize siasa mahakamani.
Mkuu asante kwa kupanua mada na kuonesha idadi kubwa ya Madikteta wa Afrika ingawa Jaji Mihayo alisema Afrika Mashariki tu na aliyemtaja ni Iddi Amin.

Kuna madikteta wengi tu Afrika. Nashangaa msomi kama wewe unashindwa kujua hilo.

Hawa ni baadhi ya madikteta Afrika:



1. Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo

Nchi : Equatorial Guinea

Madarakani: Tangu August 1979

Kampindua mjomba wake Francisco Macías Nguema.

Equatorial Guinea ina utajiri wa mafuta lakini pesa yote anaiba yeye na familia yake. Wananchi wanakufa na njaa.


2. José Eduardo dos Santos

Nchi: Angola

Madarakani: Tangu September 1979 alipokufa Rais Agostinho Neto.

Binamu yake ni makamu wa Rais.
Mtoto wake wa kike, Isabel, ni bilionea wa kwanza wa kike Afrika.

Angola Ina utajiri wa mafuta na almasi lakini wananchi wake wanakufa na njaa. Ukiishi zaidi ya miaka 41, unabahati.

Familia ya Rais Dos Dantos, inamiliki makampuni mingi katika uchumi wao mpaka kuweza mtoto wake Isabel kununua share katika mabenki na makampuni ya magazeti makubwa ya Ureno.


3. Rais Robert Mugabe

Nchi: Zimbabwe

Madarakani: Tangu 1980 (Waziri Mkuu, Rais wa Nchi 1987)

Asilimia 60 ya wananchi hawana kazi, wengi wanakimbilia Afrika Kusini kutafuta kazi.

Baada ya kutaifisha ardhi iliyokuwa inalimwa na raia wa kizungu wa Zimbabwe, uchumi ukashuka. Wakulima Wazawa wakashindwa kuitumia ardhi vizuri kutokana na sababu za kifedha na kielimu.

Sasa nchi inaomba msaada wa chakula nje na vyakula ni adimu madukani.

Pia, wapinzani wake wamebanwa koo na serikali yake.


4. Mfalme Mswati III

Nchi: Swaziland

Madarakani: Tangu 1986

Wananchi wake wanaishi miaka 46, wengi wanakufa na ukimwi na njaa. Asilimia 40 hawana kazi.

Mfalme ndiyo Mkuu wa Nchi. Hamna kura ya kuchagua kiongozi.

Mswati anatumia fedha za Nchi kama za kwake. Anajulikana zaidi duniani kama mpenzi wa magari ya BMW na huowa karibu kila miaka michache. Ana wake 14.


5. Rais Omar Al-Bashir

Nchi : Sudan

Madarakani: Tangu 1989 baada ya kumpindua Sadiq al- Mahdi.

Vita nchini vimeua watu milioni moja na maonevu dhidi ya raia wa Kiafrika wa Kusini mwa Sudan imesababisha Sudan kugawanyika mwaka 2011 na kuwa Sudan na Sudan ya Kusini baada ya raia hao kupigana vita na serikali ili wapate haki zao.

Wananchi wa Sudan hawana haki yoyote chini ya serikali yake ya chama kimoja, National Islamic Front. Wabunge wake wote 500 ni wa kuteuliwa.

Bado sijaongeza kina Museveni, Kagame na Nkurunziza.

Listi ni ndefu mno.
 
Ama kweli Binadamu kiumbe wa ajabu. Hivi kweli watanzania tutaridhika lini? JK mmemlaumu wee kuwa hafai,ati mpole, anachekacheka tu, anauza sura, serikali ya kishkaji nk. Leo hii JPM anajaribu kuchukua mwelekeo mwingine malalamiko ndo kwanza yamejaa beseni. Jamani mungu hadhihakiwi...... endeleeni tu kulalamika, angalieni BBC na Aljazeera kinachotokea Syria, ni matokeo ya kutoridhika, haya yetu macho.
 
Nakubaliana na Jaji Mihayo. Hata kama Magufuli angekuwa Dikteta, nadhani kwa Tanzania ya sasa angetufaa sana. Watu wamekuwa wazembe, wezi, wavivu na kila aina ya Upuuzi. Rais Magufuli kaza buti. Hakuna kurudi nyuma

Kati ya wale 46
 
Siku tatu baada ya Rais John Magufuli kueleza kuwa yeye si kichaa, si dikteta wala mnyama, Jaji Thomas Mihayo ameungana na mkuu huyo wa nchi akisema hajauona udikteta wake.

Jaji Mihayo alikuwa akifafanua kauli alizotoa Rais Magufuli kwenye kilele cha Siku ya Sheria, wakati alipomuahidi Jaji Mkuu Othman Chande Sh12.3 bilioni za kuendeshea shughuli za mahakama na kumtaka aharakishe kushughulikia kesi za ufisadi ili Serikali iokoe Sh1 trilioni, ambazo kati ya hizo atatoa Sh250 bilioni kwa ajili ya Idara ya Mahakama.

Rais pia alitaka kesi ambazo watuhumiwa wanakamatwa na ushahidi, zifikishwe mahakamani mara moja na kuamuliwa, lakini akataka asichukuliwe kuwa ni dikteta kutokana na maamuzi yake.

“Ninapochukua hatua mimi si mnyama, si dikteta, si shetani. Ni mpole kweli, lakini inafika mahali lazima nifanye (uamuzi). Yanayofanyika serikalini ni mambo ya ajabu sana, nataka kutoa sadaka yangu, inawezekana hata nikifa naweza kuwa rais wa malaika,” alisema.

Kauli hiyo imeibua mjadala miongoni mwa wanasheria wanaodai Rais anaingilia uhuru wa mahakama kwa kutaka uamuzi wa kesi hizo ufanywe kwa utashi wa Serikali, huku baadhi ya hatua kali anazochukua zikielezewa kuwa zina harufu ya udikteta.

Lakini jana, mkuu huyo wa nchi alipata mtetezi wakati Jaji Mihayo alipoongea na waandishi kufafanua kauli hiyo ya Siku ya She ria, akisema Rais dikteta ni yule asiyefuata misingi ya sheria.

“Wanaosema Magufuli ni dikteta hawawajui madikteta. Hakuna kiongozi dikteta Afrika Mashariki isipokuwa Idi Amini tu,” alisema jaji huyo mstaafu ambaye alisema ameamua kutoa ufafanuzi huo baada ya kuona mjadala mkubwa kuhusu kauli hiyo ya Rais na kupata baraka kutoka kwa Jaji Mkuu, Othuman Chande.

Jaji Mihayo, ambaye ni mwenyekiti wa majaji wastaafu, alihoji inawezekanaje kiongozi ambaye mataifa mengine wanatamani akaongoze nchi yao angalau kwa miezi miwili, aonekane kuwa ni dikteta.

“Magufuli anafuata sheria kwa sababu hajafanya jambo lolote ambalo linamfanya awe juu ya sheria. Sijawahi kusikia kasema mfunge huyu au kusema sheria hii isitumike na hii itumike” alisema.

Alisema ni kawaida kwa viongozi wanaokemea uovu kuonekana kama madikteta kwa sababu wanataka kuondoa rushwa.

Kadhalika, Jaji Mihayo alisema anaupenda utendaji kazi wa Magufuli ili wanaokiuka sheria wawajibishwe na walalahoi wapate haki yao.

Magufuli na Mahakama
Kuhusu ahadi yake ya kuipa Idara ya Mahakama Sh12.3 bilioni ili izitumie kwenye shughuli zake na agizo la kuharakisha uamuzi wa kesi 442 ili Serikali iokoe Sh1 trilioni, Jaji Mihayo alisema kitendo hicho hakiingilii uhuru wa mahakama bali ni katika kuhakikisha kesi zinamalizwa kwa wakati na serikali inakusanya mapato ya kutosha.

“Maneno ya Rais ya kuwataka majaji wamalize kesi kwa haraka na kuwaahidi kiasi kile cha fedha, si kuwahonga bali ni motisha na mbinu ya kukusanya mapato,” alisema.

Alisema kauli ya Rais isitafisriwe kuwa ni lazima Serikali ishinde kesi dhidi ya rufaa ya kodi, bali alitaka majaji wafanye kazi zao kwa wepesi zaidi.

Akifafanua kesi za rufaa za kodi, Jaji Mihayo alisema mashauri hayo yatakusanya fedha nyingi kwa hata kama wanaodaiwa watashinda, kisheria ni lazima watoe theluthi ya kodi wanayodaiwa.

Jaji Mihayo pia alisema maneno ya Magufuli yasichukuliwe kuwa yatawavuruga majaji kwa sababu wanafanya kazi yao kwa kufuata kanuni na sheria.

“Uhuru wa mahakama upo ‘guaranteed (umehakikishwa)’ na katika kifungu namba 107 (a) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano.Hata kama Rais akiamrisha vipi, kama ni kitu ambacho ni kinyume na utaratibu, hakiwezi kutekelezwa” alisema.

Kuhusu Magufuli kuwachukulia hatua majaji na mahakimu 502 ambao hawajafikia malengo ya kumaliza kati ya kesi 250 na 260 kwa mwaka, Jaji Mihayo alisema JPM alionyesha kukerwa na ucheleweshaji wa kesi na wala si kuingilia uhuru wa mahakama.

Alisema hata Jaji Mkuu Othman Chande alishachukua hatua kwa kuwataka mahakimu hao watoe maelezo kabla sheria haijachukua mkondo wake.

“Tatizo la ucheleweshaji wa kesi ni kubwa, si dogo kama unavyofikiria ndiyo maana linamkera JPM,” alisema.

Utendaji wa mawaziri, wakuu wa mikoa
Kadhalika Jaji Mihayo pia alizungumzia pia jinsi mawaziri wa JPM wanavyotoa kauli za kuwafukuza kazi au kuwasimamisha watendaji wa Serikali, akisema siasa inatawala kuliko sheria.

Alisema kisheria kiongozi wa Serikali hawezi kusimamishwa kazi au kufukuzwa bila maandishi.

“Watendaji hawatachukuliwa hatua bila kauli ya waziri kuwa katika maandishi, hilo jambo halichukuliwi kijumla tu,” alisema.

Alisema Katibu Mkuu Kiongozi akimsimamisha au kumfukuza mtu kazi, hilo linakuwa limeshafanyiwa kazi kwa kina.

“Vinginevyo, huwezi kumfukuza mtu kazi bila mchakato na uchunguzi wa kuhakiki kama ni kweli ana haki ya kusimamishwa au kufukuzwa,” alisema.
Naona Jaji Mihayo yuko katika harakati za kuomba ateuliwe awe mwenyekiti wa tume fulani ndani ya serikali!!
 
Mtandao wa maivii. Ndio unaleta shida kwa sasa. Wala Sio UKAWA . Wanataka KIKI ya 2020 kwa kulaumu na kukosea kila kinafanywa na JPM. WATANZANIA WAONA. MAFISADI, WEZI WA MALI ZA UMAA. Mtaangaika sana
 
Amesema EAC akuna dikteta. Alikuwepo Idi Am in I ndivyo alivyosema na Sio AFRICA


Definition of a Dictator:

noun

A ruler who is not effectively restricted by a constitution, laws, recognized opposition, etc

An absolute, esp tyrannical, ruler
(in ancient Rome) a person appointed during a crisis to exercise supreme authority

A person who makes pronouncements, as on conduct, fashion, etc, which are regarded as authoritative

A person who behaves in an authoritarian or tyrannical manner

source: collinsdictionary.com

Sasa hapo Uganda na Rwanda, kuna demokrasia? Hapo siyo Afrika Mashariki?

Marais Museveni, Nkurunziza na Kagame ni madikteta. Wameshikilia uongozi kwa nguvu, wanawaua na kuwafunga wapinzani wao. Wengine wamebadilisha katiba ili wakae ikulu baada ya muda kwisha kikatiba. Wameshika madaraka kwa nguvu. Serikali na chama ni kitu kimoja.

Huo ndiyo uongozi wa kidikteta.
 
Sijui kama hii ni JF au ni fb. Mkuu fungua dictionary usome maana ya dictator. Ku dictate ni kutoa amri na hiyo amri ndo sheria. Kiswahili wanaita utawala wa kiimla. Yaani hakuna sheria. Amri ya Mkuu wa nchi ndo sheria. Hatuna rais wa aina hiyo kwa sasa apa africa


Definition of a Dictator:

noun

A ruler who is not effectively restricted by a constitution, laws, recognized opposition, etc
an absolute, esp tyrannical, ruler
(in ancient Rome) a person appointed during a crisis to exercise supreme authority.

A person who makes pronouncements, as on conduct, fashion, etc, which are regarded as authoritative.

A person who behaves in an authoritarian or tyrannical manner.

source: collinsdictionary.com
 
Tafsiri za ulaya. Wananchi wanaudumiwa safi sana na uchumi mzuri. Elimu, afya zao mzuri. Rwanda na Uganda. MTU wa maendeleo na kuongoza ndio tunamtaka Africa. Sio mwizi kama mliotaka kutuletea Tanzania
 
Tafsiri za ulaya. Wananchi wanaudumiwa safi sana na uchumi mzuri. Elimu, afya zao mzuri. Rwanda na Uganda. MTU wa maendeleo na kuongoza ndio tunamtaka Africa. Sio mwizi kama mliotaka kutuletea Tanzania

Mkuu,

Hapa tunaongekea udikteta wa viongozi. Wewe unaongelea kutaka kiongozi Dikteta.

Ni vitu viwili tofauti.

Chagua.

Hamna maana ya kizungu na Kiafrika. Hizo ni porojo za vijiweni.
 
Anayesema magufuli dikteta atakuwa chizi au yupo kwenye kundi la mafisadi wanaochukia uongozi wa magufuli kwa hofu ya kupelekwa kwenye mahakama ya mafisadi.
 
Kwanza magufuli angekuwa dikteta mimi ningefurahi sana ili akomeshe ujinga mwingi wa baadhi ya watu uliokithiri.
 
Nakubaliana na Jaji Mihayo. Hata kama Magufuli angekuwa Dikteta, nadhani kwa Tanzania ya sasa angetufaa sana. Watu wamekuwa wazembe, wezi, wavivu na kila aina ya Upuuzi. Rais Magufuli kaza buti. Hakuna kurudi nyuma
Tena magufuli angekuwa dikteta mimi ningefurahi sana maana wajinga kama kundi la mafisadi ndiyo kiboko yao.
 
Sidhani kama kukaa madarakani muda mrefu ni kigezo cha udikteta. Wapo wanaokaa muda mrefu kwa mujibu wa sheria ya nchi zao husika. Udikteta ni matendo yanayokiuka sheria katika muda mtawala aliopo madarakani, hata kama ni miaka mitatu

Katiba ya nchi inasema Raisi lazima anga'atuke baada ya muda wake kuisha.

Marais wa Rwanda na Burundi na wengine wanabadili katiba ili waongoze zaidi bila idhini ya wananchi.

Kama wangefanya referendum, ingekubalika. Lakini wanatumia nguvu kuganda katika uongozi.

Huu siyo mfano wa uongozi wa Kidikteta?
 
Back
Top Bottom