ITIKADI ni imani; Membe amepotoka na amefanya uamuzi wa kijinga

Labda usichokifahamu kuwa Mgombea mkuu wa Chama cha Upinzani kunakuja na umaarufu mkubwa wa ndani na nje ya nchi, na hicho ndicho wanachokitafuta, anajua hawezi kushinda na kuiondoa CCM ni kama Tundu Lisu tu, attention seeking, Lowasa sasa hivi ni maarufu sana nje na ndani ya nchi sababu hiyo, ...

Hii mada inahusu uchaguzi na umaarufu wa wagombea, au ni mambo ya itikadi? Kenge jike ww.
 
Naona dozi za CHADEMA zimeanza kukuingia vizuri na bado, peopleeeeeeeeessss!!!
 
wanaotaka kutimiza ndoto za kuwania urais, wanafaya hivyo upinzani.
 
'Itikadi ni imani' ... naamina imani hubadilika, watu hubadili imani wanapoona waliyokuwa wanayaamini hawayaishi, so huwez kuendelea kuamin kitu ambacho kiwez kukiishi.. conclusively kama unaweza kabadil imani it is easy kubadil itikadi!
 
Kinachotekea sasa hiv sio, sio itikadi bali ni ubinafsi, maslahi binafsi, unafki, all for personal benefits and not as a nation!!
 
Sijui hata kama unazo akili za kutosha kutafakari kwa usahihi. Wakati akiwa taabuni akinyanyaswa na wakuja hukutoka kumtetea. Polepole na Bashiru wamefanya yao mko kimya. Sasa kafukuzwa chamani abaki kufanya nini. Kama imani ataendelea kuwa nayo in exile.

Lowasa alishindwa wakati CCM ikiwa moja chini ya mwenyekiti muungwana hana kiburi wala majivuno hatukani watu wala hajui kutishia watu kama yeye ni Mungu. Kwa mazingira haya CCM hii ni dhaifu kuliko kawaida

Lowasa alishindwa kwasababu uongozi uliokuwapo ulijali wafanyakazi na kuwathamini. Leo miaka mitano wanapiga miayo. Mstaafu wa mwaka huu na ujao anapata sawa na na wa mwaka 2015 huku gharama za maisha Zikiwa zimepanda mara mbili zaidi ya ilivyokuwa 2015
Lowasa na Mrema walishindwa kwa sababu serikali ilikuwa haipendeleo kupeleka maendeleo kwa viongozi. Chato inalazimishwa iwe jiji kisa Rais ni wa huko.

Mwisho kabisa Membe ni tofauti na Mrema na Lowasa. Anao uwezo binasi wa kujieleza mambo yaliyowashinda Lowasa na Mrema wakawa wakisubiri wasemewe.

Kumchagua Membe wananchi hawatapoteza Kituo zaidi ya ufedhuri, kiswahili kibovu,matusi na ushamba
 
Every man has right to decide. Watu wanabaidili dini ambalo ndio Jambo zito zaidi itakuja kuwa chama hata muasisi wa chama cha mapinduzi hayati baba wa taifa mwalimu Julius K Nyerere kawambia wana ccm na taifa Kwa jumla kuwa ccm sio mama yake anaweza kuachana nacho kwa hiyo kama mh membe kaamua kutoka ccm sawa tu.

Heshima ya mtu haishuki Kwa sababu tu ya kuhama chama uongo, bali heshima ya mtu inashuka kutokana matendo yake maovu katika jamii na mwanadamu alivyoumbwa ni mtu wa kubadilika kutafakari na kuamua.

Kujengwa kiitikadi na kiimani sio sababu ya msingi Mungu kampa mwanadamu akili ya kupambanua mambo ndio maana leo tunapiga vita Imani potofu Kwanini tusikae kimya tukaacha watu na Imani zao mtu akifiwa na mumewe lazima atembee na wanakijiji ili apate utakaso nk. Bernard Membe kafanya maamumizi yake binafsi na wala sio dhambi ni jambo la kawaida na yeye si wa kwanza Kwa hiyo sio big issue tumuache ende akatekeleze dhamira yake.

Wewe umejitambulisha kuwa mwana ccm kwa hiyo kazi kubwa ilokuwepo mbele nikueleza jinsi gani mwenyekiti wetu na rais wetu wa jamhuri ya muungano Dk John Pombe Joseph Magufulu Kwa kiasi gan katekeleza ilani yetu ya uchaguzi ya 2015-2020 na Kwa nini watanzania wanatakiwa wampe ridhaa ya kuweza kutuongoza tena Kwa mustakbali wa taifa. Usijiadili Mambo madogo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom