TandaleOne
JF-Expert Member
- Sep 4, 2010
- 1,644
- 709
Watu wameendelea kutoa maoni yao kuhusu uamuzi wa aliyekuwa Kada na Kiongozi mwandamizi wa Chama na Serikali, Mzee wangu Bernerd Membe kujitoa rasmi katika Chama cha Mapinduzi, nimeonelea kuwa ni jambo lenye manufaa nami nikaungana na watanzania wengine katika kutoa mtazamo wangu katika kadhia hiyo. Kwa ufupi sana.
Jambo la kwanza kubwa ni kuhusu ITIKADI, tumefundishwa na kuelewa kuwa itikadi ya Chama Cha Siasa ni imani, imani inayojengwa katika misingi, falsafa na nadharia ya namna bora na sahihi ya kuongoza watu na kuendesha nchi. Imani mahala pake ni moyoni, huko ndiko inakohifadhiwa. Aliyeamini huitwa MUUMINI na daima, katika siku zote za maisha yake muumini ataiishi, atailinda na kuifia imani yake. Uamuzi wa Mzee wangu unanirudisha katika fikra nzito nikiwaza Mzee MEMBE aliamini katika nini, je alikuwa mkweli katika imani yake..? imani iliyomlea, iliyomkuza, ikamjenga na kumuinua daraja akawa mtu katika watu.
Jambo la pili, kwa mtu wa taaluma yake, inatia mashaka juu ya ubobezi wake, upofu wa mipango yake na upoyoyo wa mikakati yake na ujinga wa maamuzi yake. Inawezekana vipi, mtu mwenye fikra zilizo sawa akapita katika njia ya waliopotea, akiwa anajua katika dhati ya moyo wake kuwa njia hiyo it's heading nowhere. Alijaribu Mrema mwaka 1995 akiwa anabebwa na makundi ya watu na watu wakisukuma gari yake, hakufanikiwa, Ameendelea kujaribu Seifu Sharif, hatofanikiwa, Alijitosa Mzee Lowasa 2015 akiungwa mkono na makundi ya Vijana na wabeba mikoba ya noti, hakufanikiwa...,how could he make it with a bunch of paid actors kijijini kwake chiponda..how..?
Mimi sio mtu wa kuyumba katika misimamo yangu, nimeiishi imani na itikadi yangu na hata ninapopambana huwa ninapambania imani ninayoiishi na si vinginevyo, sikuwahi kuwa adui wa mtu kwa kufuata mkumbo na sikuwahi kuwa rafiki wa mtu kwa kufuata mkumbo..ninapambana na yeyote kwa wakati wowote pale ninapoona MISINGI ya imani ninayoiamini inachezewa .
Kama vile tunapokuwa katika mafanikio katika carrier zetu, pale tunapopata majaribu, tuwe bold and strong enough kupambania yale tunayoamini hayako sawa katika kulinda, kujenga na kuendeleza Imani/Itikadi zetu. Mzee Membe kwa uamuzi wake amejivua hata ile heshima kidogo aliyobakiwa nayo katika jamii yake na hata kwa wale tuliomuamini na kudhani ni mtu jasiri, mwelevu na mwenye maono, amethibitisha kuwa ni mtu dhaifu, muoga, asiye na msimamo na mpotevu.
Natoa wito kwa wanachama wenzangu wa CCM na wananchi wenzangu. Tuendelee kuilinda Imani ya Chama Chetu kwa gharama yeyote.
Mpaka sasa CCM bado ni Chama bora kabisa na imani yake ni THABITI.