Iron Dome :Marekani kununua mfumo wa Israel wa kujilinda dhidi ya makombora

Pistol

Senior Member
Oct 13, 2015
194
86
Jeshi la Marekani limetangaza mipango ya kutaka kununua na kujaribu mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora wa Israel kwa jina Iron Dome.

Mfumo huo unaotumia rada na kutungua makombora kwa lengo la kukabiliana na tishio lolote umekuwepo tangu 2011.

Idara ya ulinzi nchini Marekani imesema kuwa mfumo huo utatumika kufanya majaribio huku ikitafuta mahitaji ya muda mrefu ya jeshi lake.

''Hili ni dhihirisho jingine la kuimarika kwa ushirikiano wetu thabiti na Marekani, na onyesho kwamba Israel inazidi kupandisha hadi yake duniani, "taarifa yake iliendelea.

Ufanisi wake
Mfumo huo wa Iron Dome hufanya kazi kwa kufuatilia tishio lolote la shambulio kwa muda mfupi kupitia rada yake , kisha inachambua data kuhusu eneo litakaloathirika - kabla ya kuamua kurusha kombora litakalotungua shambulio hilo.

Maafisa wa Israel wanasema kuwa mfumo huo wa makombora unaoweza kufanya kazi katika mazingira yoyote mbali na kusafirishwa kutoka eneo moja hadi jingine una mafanikio ya hadi asilimia 90.

Unasemekana kuwa na uwezo wa kulinda mji mzima dhidi ya tisho lolote la angani na umetumiwa sana kutungua makombora yaliorushwa na wapiganaji wa Kipalestina katika ukanda wa Gaza.

Utengenezaji wa mfumo huo
Ilichukua miaka kadhaa kuunda mfumo huo na ulitengezwa na kampuni ya ulinzi nchini Israel Rafael Advanced Defence Systems.

Marekani ilichangia sana katika uundaji wa mfumo huo, na baadhi ya vifaa vyake vinatoka kwa makampuni ya Marekani.

Katika taarifa, idara ya ulinzi nchini Israel ilisema kuwa ununuzi huo ulifanyika kutokana na mahitaji yake ya dharura ya jeshi la Marekani.

Ripoti zilivuja kuhusu ununuzi huo mwezi uliopita.

Kanali Patrick Seiber wa jeshi la Marekani amesema kuwa mfumo huo unachunguzwa na kujaribiwa ili kuwalinda wanajeshi wa Marekani waliotumwa katika mataifa ya kigeni.

Huku mfumo huo wa Iron Dome ukiwa umetumika na wanahewa wa Israel tangu 2011 na kuthibitisha uwezo wake katika vita, ilazima ibainike kuwa jeshi la Marekani litauchunguza kwa lengo la kuimarisha uwezo wake wa siku zijazo wa kujilinda , taarifa iliotolewa siku ya Jumatano ilisema.


BBC

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo machuma ya 300,400 na 500 uactive wake upo mdomoni na kwenye makaratasi?

Sent using Jamii Forums mobile app
300,400 na 500 za mrusi kwa Kweli Hazipo busy kupangua makombora ukilinganisha na iron dome ya Israeli na utaona pindi mashambulizi yanapotekelezwa pale Syria sometime inaelemewa.
Kuna watu humu jf hufikiri kuwa huenda walizima au hawajui kuzioparate lakini si Kweli kwani mikataba yao ni kuhakikishiana ulinzi. So 2 me iron dome is the best.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa watu wanatuzuga hasa USA kama alishiriki kuuunda inakuaje sasa atumie hela kuununua?? Anataka kuzuga kua mifumo yake iko imara ila kashaona mapungufu anataka kuyaziba!!
Kiuhalisia ni vigumu kununua kitu kilicho nadni ya uwezo wako kukitengeneza hasa masuala ya zana za kijeshi!
 
Hawa watu wanatuzuga hasa USA kama alishiriki kuuunda inakuaje sasa atumie hela kuununua?? Anataka kuzuga kua mifumo yake iko imara ila kashaona mapungufu anataka kuyaziba!!
Kiuhalisia ni vigumu kununua kitu kilicho nadni ya uwezo wako kukitengeneza hasa masuala ya zana za kijeshi!
So Kweli coz Uturuki imeshiriki kufadhiri mradi wa uundwaji wa ndegevita Aina ya F35 lakini mbona anauziwa?

Isitoshe Israeli yenyewe kauziwa ndegevita F18 na Hata hiyo F35 lakini bado kauziwa na msharti kibao.
Hiyo Ni Kawaida tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mada haisemi alifadhili inasema. Alishiriki it means anaijua tech iliyotumika!! Kwa nn asitengeneze yake kupunguza garama. Na hayo masharti?
So Kweli coz Uturuki imeshiriki kufadhiri mradi wa uundwaji wa ndegevita Aina ya F35 lakini mbona anauziwa?

Isitoshe Israeli yenyewe kauziwa ndegevita F18 na Hata hiyo F35 lakini bado kauziwa na msharti kibao.
Hiyo Ni Kawaida tu

Sent using Jamii Forums mobile app
anaijuia
 
Hivi karibuni iran ilisema marekani ataondoka syria ama kwa kupenda yeye au kuondolewa,na kwa msisitizo kuna maroketi yalikutwa yamelenga ngome ya marekani,iraq iitwayo al assad airbase,hiyo ilikuwa ni message,kwahiyo wananunua ili kulinda maeneo kama hayo,marekani hana short range air defence sababu haina nchi adui inayopakana nayo,ila marekani walisaidia kuunda iron dome kwa ajili ya israel kupambana na maroketi ya hamas
 
Exclusive: Iraq discovers
three Iranian rockets
ready to fire at US base
Feb 2, 2019 @ 18:30
Iraqi security forces Saturday
discovered three Iranian-made missiles
ready to fire and aimed at the US Ain Al
Assad Air Base in the northwestern
province of Anbar near the Syrian
border, DEBKAfile can exclusively
report. This discovery provides further
evidence of Iran’s ruthless
determination to force US forces to
leave Iraq, not just Syria – by whatever
means it takes. Ain Al Assad was the
base in Iraq which President Donald
Trump and the first lady visited on
Christmas with greetings for the US
troops serving there
 
Back
Top Bottom