Iran itajibu uchokozi wa maadui

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Naibu Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria hujuma ya ndege isiyo na rubani ya Marekani katika anga ya Iran na kusema Iran haitaacha uhasimu huo wa maadui bila jibu. Amesema maadui wataona athari za jibu litakalotolewa na Iran kufuatia vitendo vyao.
Brigedia Jenerali Hussein Salami, katika katika mahojiano na Kanali ya Pili ya Televisheni ya Iran, amesema ndege isiyo na rubani ya Marekani iliyohujumu anga ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliangushwa chini kwa kutumia teknolojia inayomilikiwa na vikosi vya anga vya Iran. Brigedia Jenerali Salami amesema Iran ni kati ya nchi chache duniani zenye kumiliki teknolojia ya utengenezaji ndege zisizo na rubani zenye vifaa vya kufanya upelelezi wa kina. Amedokeza kuwa hata kabla ya kuinasa ndege isiyo na rubani ya Marekani, Iran tayari ilikuwa inamiliki teknolojia ya kutengeneza ndege zisizo na rubani zisizoweza kuonekana kwenye rada au stealth.
Amesema maadui wa Iran bado hawajadiriki uwezo mkubwa ilionao Iran katika uga wa teknolojia na hivyo amewataka kutafakari zaidi kuhusu uwezo wa Iran. Itakumbukwa kuwa Jumapili wiki iliyopita jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lilitangaza kuwa kitengo chake cha ulinzi wa anga na vita vya kielektroniki kilifanikiwa kuiangusha kitaalamu ndege ya kijasusi isiyo na rubani ya Marekani aina ya RQ-170 Sentinel.
 
Back
Top Bottom