Iran haitosita kutoa msaada kwa Wairaq kwa ajili ya kupambana na Israel

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,045
18,014
Msemaji wa serikali ya Iran: Utawala wa Kizayuni wa Israel ukubali taathira mbaya za uchokozi wake
Aug 26, 2019 12:01 UTC
Msemaji wa Serikali ya Iran amelaani mashambulizi yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika nchi za Lebanon, Iraq na Syria na kusema kuwa, utawala huo unapaswa ukubali taathira mbaya za uchokozi huo.
Ali Rabi'e amewaambia waandishi wa habari leo kwamba, Israel haipasi kutumia vibaya subira ya watu wa kanda ya magharibi mwa Asia na kuongeza kuwa: Iran inaunga mkono haki halali ya kujihami ya mataifa ya Iraq, Syria na Lebanon. Rabi'e amesema tahadhari iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah kwa utawala wa Kizayuni wa Israel ni ujumbe mkali na wa jaddi kwa wachokozi na kuongeza kuwa: Katika miezi ya hivi karibuni utawala wa Kizayuni wa Israel umezidisha ukiukaji wa sheria za kimataifa.
Kuhusu shambulizi la ndege isiyo na rubani ya Israel dhidi ya kambi ya harakati ya wananchi ya al Hashdu al Shaabi nchini Iraq, msemaji wa serikali ya Iran amesema: Jamhuri ya Kiislamu haitasita kutoa msaada wa aina yoyote kwa Wairaqi kwa ajili ya kukabiliana na uchokozi wa utawala wa Kizayuni.
Vilevile ameashiria hali ya meli ya mafuta ya Iran Grace-1 na kusema Iran imeuza mafuta yaliyomo kwenye meli hiyo na sasa mmiliki wa mafuta hayo anapaswa kuchukua uamuzi mzigo huo utapelekwa wapi.
Msemaji wa serikali ya Iran amezungumzia pia safari iliyofanywa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran nchini Ufaransa na kusema: Safari ya Muhammad Javad Zarif haikuwa na mfungamano na kikao cha G7 na imefanyika kwa mwaliko wa Ufaransa. Amesisitiza kuwa Iran haina hamu ya kufanya mazungumzo na maafisa wa Marekani.
 
Hawana ubavu
 
Back
Top Bottom