Inatutafuna kimya kimya..itatumaliza..

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Naishi maeneo ya Ubungo nikaona itanigharimu kidogo ikiwa watoto wangu nitawaandikisha shule za chekechea maeneo ya Mbezi (Kimara). Tulipoanza uongozi wa shule walikubali kuwa ikiwa mtu ana watoto zaidi ya mmoja, nafuu itatolewa kwa usafiri..leo ni mwaka mmoja tu tokea tukubaliane hayo..sasa yule inataka wazazi tulipie kila kichwa cha mtoto gharama halisi za usafiri bila punguzo ambazo kwa muhura zinakaribia laki mbili kwa mtoto mmoja (haijalishi ukaribu wa eneo ambapo mtoto anatoke)..

Changamoto ambayo binafsi nimepata sambamba na kushuka kwa matokeo ya mitihani ya shule za msingi na sekondari mwisho ya vijana wetu katika shule za sekondari na hata vyuo, ni kukosekana kwa mfumo mzuri wa kwa Serikali kuthibiti utitiri wa watoa huduma katika sekta binafsi..Hivi leo, kuna shule kibao za Chekeche mpaka kidato cha sita na pia vyuo ambavyo vinatoa elimu na kumilikiwa na watu binafsi. Ukifuatilia kwa makini, kumekuwa na tofauti kubwa sana na gharama na huduma zinazotolewa na shule hizo...Wakati Serikali imeruhusu haya kwa upande mwingine hakuna utaratibu wowote wa kisheria wa kudhibiti utendaji na huduma zinazotelewa na sekta binafsi. Hii imechainga kwa kiasi kikubwa sana watoa huduma kujiamuria wayatakayo, kujipangia viwango vya huduma, gharama nk. Hivi sasa ukifuatilia kwa makini utabaini kuwa shule nyingi zinapata faida kubwa sana kupitia gharama za usafiri, malazi na chakula. Kwa kuwa shule hizo nyingine zimeanzishwa kama mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) hazitozwi kodi yeyote hivyo kujineemesha vilivyo.

Chakusikitisha zaidi, kwa kuwa watoa huduma hizi katika sekta binafsi wengi ni watumishi wa Umma na wananyazifa tofauti, kupitia nyazifa walizonazo, wameweza kuishawishi Serikali kuweka utartaibu mbovu ambao hautawabana.

Mtakumbuka enzi za Mhe. Joseph Mungai akiwa ni Wziri wa Elimu na wakati huo huo anamiliki sekondari binafsi..na kwa taarifa za uhakika, hata Naibu Waziri wa sasa wa Elimu Mhe. Philipo Augustino Mulugo nae ni mmiliki wa Sekondari kule Mkoani Mbeya!!!..Katika Hali kama hii, inawezekanaje kwa Mtendaji Mkuu wa Serikali kuwa mwadilifu katika kusimamia maamuzi ya Serikali ambayo pengine yanaenda kinyume na maslahi binfasi ???...

Leo hii, karibia kila mtumishi wa umma anamiliki ofisi/ Kampuni binafsi ambayo pangine anaitumia kuchota fedha za umma..kwa mfano wadaktari wengi wanamiliki zahanati au maduka ya madawa na wemgine mbele ya Hospitali kubwa za Umma. Wahasibu wanakampuni zao binafsi za ukaguzi, wagavi (procurement officers) wanamakapuni ya Ugavi; wakandarasi au mawaziri wenye dhamana ya ujenzi wanamiliki makapuni ya ujenzi; Mfanyakazi wa Shirika la Bima la Taifa anakampuni ya Bima, Afisa Mkubwa wa Polisi, anamiliki kampuni ya Ulinzi, Mkurugenzi, Mtendaji Mkuu, Jaji, Hakimu au Balozi ambaye anatumika Serikalini kwa taaluma ya sheria huko mtaani anamiliki kampuni kubwa ya Uwakili nk nk.

Katika mfumo huu, Serikali imejikuta ikifikia maamuzi ambayo yanawaumiza kwa kiasi kikubwa wanyonge kwa mfano mahospitali kukosa huduma kwa kuwa daktari yupo katika hospitali yake wakati wa muda wa umma; Serikali kupoteza kesi nyeti kwa kuwa wakili wa Serikali aliamua kuuza kesi hiyo kwa wakili wa upande wa pili ambaye ni mbia wenzie katika Biashara; baadhi ya shule kufanya vizuri na nyingine kufelisha vibaya sana kwa kuwa mtendaji anaesimamia mitihani kavujisha mitihani katika shule yake au mwalimu wa shule ya umma anamilii shule binafsi na muda mwwingi yupo shule kwake nk nk.

Tumefikia katika zama mbaya sana ambayo hatuwezi kukwepa ufisadi wa wazi...na hili litatutfauna iwapo Serikali yetu haitaiwekea utaratibu wenye sura ya "AZIMIO LA ARUSHA".....
 
Uongozi wa mafisadi na Hatima ya Tanzania,mwisho wa haya ni wizi,umaskin,uzandiki,mauaji na kuchapana makonde
 
Watabadilishaje utaratibu wakati watakaopata hasara ni wao??Hio ndio Tanzania yetu....either tubadilishe mfumo mzima wa uongozi ili tuanze upya au tuzoee hali ilivyo!
 
Back
Top Bottom