Artificial intelligence
JF-Expert Member
- Jan 28, 2021
- 1,262
- 2,192
Kiukweli nilibahatika kutembelea jumla ya plants za madini 9, tatu kahama Shinyanga na 6 wiliya ya Bukombe Geita. Nilichokiona na kukishuhudia kwenye plants hizo ni cha kuhuzunisha na kusitikisha sana haswa kuhusu afya za watu walioajiriwa kwenye hizo plants na wanaoishi kuzunguka hizo plants.
Plants hizo ambazo zinajihusisha na uchenjuaji wa dhahabu kutoka kwenye mchanga au mawe ni za watu wenye kipato cha kati na cha juu, ili kuendesha plants hizo, wataalamu mbalimbali wa kusimamia na kuendesha shughuli hiyo uhitajika.
Jinsi gani zinahatarisha afya za watu, niligundua baadhi ya mambo kama ifuatavyo
Kwanza
Wataalamu walioajiriwa ni unprofessional, hawana taaluma ya kile wanachokifanyia kazi. Hapa nitatolea mfano wakemia wanaotumika kupima na kuandaa kemikali zinazohitajika Kwa ajili ya uchenjuaji, cha kwanza kabisa katika plants zote hizo ni plant moja tu iliyokuwa na mkemia ambaye ni professional (na huyo anasema ndiye anaye wafundisha vijana), zilizobaki ni vijana wanachukuliwa mtaani na kufundishwa jinsi ya kupima na kuandaa hizo kemikali, vijana hawa kwa sababu hawana ujuzi zaidi kuhusu hiyo taaluma wanajikuta wakifanya kazi katika mazingira magumu sana.
Vijana wanaingia maabara bila vifaa maalumu vya kujikinga na kumwagikiwa au kudondokewa na sumu hizo za kemikali, katika hali ya kustahajabisha vijana hawa ushika kemikali kwa mikono na vifaa vya kemikali bila kujali, hapa ndipo wanajikuta katika matatizo ya kiafya kwani nilishuhudia baadhi yao wakikohoa damu, kucha kuchomoka, nywele kuungua, ngozi kubabuka n.k, baada ya kuwauliza Kwa nini jibu lilikuwa ni sisi "tumeshazoea haya ndiyo maisha yetu, tunajua tutakufa". Hii ni kwa sababu maabara hazikizi viwanga na ukosefu wa maarifa kuhusu good laboratory practices na laboratory safety.
Wakati nikiwa Bukombe, sehemu moja inaitwa namba moja, kuna plant moja kijana alikuwa anachanganya conc. Sulfuric acid kwa bahati mbaya sijuhi alikosea nini, kutokana na kuvuta hewa yake kwa sababu moshi ulitanda chumba kizima, alipiga kelele na kuomba msaada, wakati anatolewa kupelekwa kituo cha afya alisema hivi "siwezi kuona", kituoni aliambiwa sumu aliyovuta hawaiwezi ikabidi apelekwe hospitali ya wilaya Bukombe, kiukweli mpaka natoka kule kijana niliacha hajaweza kuona tena.
Pili
Uchafuzi wa vyanzo vya maji vinavyozunguka plants hizo, hapa ndipo kuna hatari kubwa sana ya watu wa kanda ya ziwa kupata cancer, kwani plants hizo hazina wataalamu wenye utaalamu wowote kuhusu "chemical speciation" na "waste management", hivyo hawajuhi chochote kuhusu bio-concentration, bio-accumulation concepts, hivyo kemikali hizo baada ya kuzifanyia treatment uzitoa kwenye mantenki na kwenda kuzitupa bila utaratibu, kwahiyo kemikali hizo utiririka hadi kwenye vyanzo vya maji kama mito na visima ,hali hii inapelekea maji wanayotumia kutoka kwenye visima na samaki kutoka kwenye mabwawa na hiyo mito kuwa na kiasi kikubwa cha kemikali hizo zenye sumu.
Pamoja na kwamba ni uchimbaji mdogo, lakini unahitaji utaalamu na usimamizi pia, wamiliki wa plants wanapata pesa nyingi, lakini hawajali kabisa kuhusu afya za watu, NEMC pamoja na ofisi ya mkemia mkuu mkuu wa serikali (GCLA) kwa kushirikiana na wizara ya madini chini ya serikali mnao wajibu wa kusimamia hili ili kuwanusuru watu kutokana na hizo sumu za kemikali.
Najua kuna rushwa kubwa sana kule, Ila wekeni nguvu, vijana mikono, miguu inatoboka tu, huku wenye plants wakivuna pesa.