Inasemekana Waafrika wawili akiwemo Mtanzania Nemes waliofariki vitani wakipigania upande wa Urusi walikuwa wanafunzi

Tuachane na maelezo yako yaliyo pita sababu nilitegemea utanipa ushahidi ulikuwa frontline unapigana hiyo vita hivyo una ushahidi.
Turejee kuhusu Wagner kule CAR. Wagner ni raia wa nchi gani?
Je unajua kwamba wengi kati ya askari wananchama wa Wagner walikuwa veteran wa sehemu ya jeshi la
Wagner PMC ni private military company kama ilivyo Black waters kule Marekani. Wao wapo kikazi zaidi. Hata wewe ukiwahitaji unawapa pesa wanakufanyia kazi yako.
 
Now that he is dead for a war that benefits white people and yet you say there are benefits! What benefits
Wagner are somehow like mercenaries, so their soldiers are getting mtonyo wa maana sana. Wagner group haijakaa kizalendo sana.

Sasa tunajuaje labda jamaa alipiga hesabu akaona akienda akarudi anaondoka na pesa ndefu ya mtaji.......... Mcha. .... no mtu yeyote tu haingii sehemu kichwakichwa na hamna hela au faida
 
Wagner are somehow like mercenaries, so their soldiers are getting mtonyo wa maana sana. Wagner group haijakaa kizalendo sana.

Sasa tunajuaje labda jamaa alipiga hesabu akaona akienda akarudi anaondoka na pesa ndefu ya mtaji.......... Mcha. .... no mtu yeyote tu haingii sehemu kichwakichwa na hamna hela au faida
Wagner Group wanalipa Rubbles 240,000 kwa mwezi, ambayo Ni Kama Tsh. 8mil kwa mwezi na bado Kuna benefit nyingine Kama Health Insurance na mengineyo.
 
Taifa kama Tanzania ili liwe salama lazima liwe na vijana kama huyo na yumkini wapo wengi "undercover" vitani sehemu nyingine duniani.

Kama ubalozi umesema utatoa taarifa kwa familia mwili ukifika inatosha. Familia nayo iwe sikivu kwa ubalozi kijana azikwe na nishani ya ushujaa. Pumzika kwa amani mzalendo wetu.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Wagner PMC ni private military company kama ilivyo Black waters kule Marekani. Wao wapo kikazi zaidi. Hata wewe ukiwahitaji unawapa pesa wanakufanyia kazi yako.
Nafahamu lakini sijakupata umekusudia kuniambia nini.
Sijaipata mantiki ya post yako.
 
Kuhusu swala la jeshi la soviet russia kupigana front line hilo ni uongo, wao walikuwa wanaleta wataalamu wa vita (technical advisors) kidogo na marubani katika strategic positions tu

Ndio maana katika wanajeshi 11k angola 54 tu ndio walipoteza maisha na wote sio katika direct kombati bali magonjwa mengine tofauti katika hiyo miaka minne ya vita Angola

Hawa wa siku hizi Wagner group ndio wanakichafua kokote yani ni wapiganaji wa kulipwa kwa lugha fasaha ni majasusi na ni watu wa mataifa mbalimbali kote duniani
Ni mamluki siyo majasusi.
Kuhusu kufa kwa ajili ya waafrika naona umethibitisha 54 walikufa wakiwa mazingira ya kazini huku Afrika aijalishi walikuda kwa namna ipi ilimradi awakufia nchini kwao au hawakufia Afrika kama watalii.
 
Kuna wanafunzi wanasoma na huku wanajishughulisha na kazi za muda. Bora kufia kazini kwa heshima, kuliko kufia kifuani kwa UKIMWI.
 
Nilikuwa nimeshakomaa wakati wa harakati za uhuru wa kusini mwa Afrika. Wakati Eduardo Mondlane anauwawa tulifunga shule na kwenda kuandamana kupinga ugaidi huo. Siyo mtu wa kusimuliwa ukizingatia kuwa tulikuwa bado ndani ya ujamaa tukiwa tunapinga ubeberu. Tuishafukuza Ubalozi wa Marekani nchini kwetu; kwa hiyo hakukuwa na siri ya majeshi ya Urusi kuwapo nchini yasijulikane.

Ni jeshi la Cuba tu ndilo lilikwenda kumsaidia Neto kupigana na UNITA ambayo ilikuwa inasaidiwa na Marekani. Urusi haijawai kuwa na jeshi lake Afrika. Hata huko Afrika ya Kati miaka ya hivi karibuni walipeleka jeshi la Wagner, siyo jeshi la Urusi lenyewe!
Right. Tena ilikuwa ni Soviet Union sio Russia kama ilivyo leo. Jeshi lake lilikuwa na askari na wataalamu wengi toka Ukraine ambayo ndiyo ilikuwa kitovu cha teknolojia (centre of excellence) cha USSR.
 
It’s my dream, nafikaje huko namimi nikapigane vita- sio kwenda kufa vita za kiafrica za Alshababa vita mbaaya vita hata hazinogi hata ukifa hautambuliki kama umekufa. Jokes

By the way

Kuna jamaa yetu mtaani hapa aliendaga kujiunga na alishababa na tukasikia kutoka kwa ndugu zake kuwa ameuwawa katika shambulio la sheri ambalo walienda kuvamia na hao alshababa katika kutafuta habari kweli tukapata habari kwenye vyombo vya habari kuwa kweli ni yeye.

Jamaa alikuwa na mke na mtoto kazi yake ilikuwa ana kibanda cha kukodisha CD na dzain kama kutengeneza sim hivi na alikuwa mtu wa swala sana na msikiti aliokuwa anafanya ibada ni ulee wa itikadi kali yaani huo msikiti ukijichanganya hata umevaa kishati hakieleweki unakula mitama,

Jamaa alikuwaga mkimia sanaa nafikiri palee msikitini walimshawishi ndio akashawishika akaingia chaka kenya huko kwa wazee wa kazi baada kama ya mwaka na nusu ndio tunasikia amefariki na ndugu hata mwili hawakuupata nomaa sana aisee unaenda kupigana vita hata havikuhusu et mmh watu wana mambo yao unaenda kujiingiza ufe tu na wanaoongoza hayo mambo wapo salama- tujiongezeni jamani hayaa kaacha mke na mtoto alaf kwa kigezo yeye kaingia peponi uongo tu hata M/Mungu mwenyewe hawezi furahia huo unazi pambana vita inayo kuhusu jombaa ufaidike.

Watu kuona kibandani yupo mke wake mara kikafungwa kwa mda mrefu sana baada ya kupapasa papasa taarifa kwa ndugu zake ndio kuambiwa nyie kumbe hamna habari jamaa yenu amefariki kenya kwenye shambulio la alshababa alienda kujiunga na fisabillah, banah jamaa aliishia hivyo.

Inasemekana ukikubali kwenda huko wazazi wako wanaingiziwa dollar 15,000 hizi pesa anazitoa nani? Yaani kuna watu wanashinda kwenye vita ya fikra yaani tunashindwa kufikiria kuwa kuna mkono wa mjinga unatugombanisha wa Africa kwa faida zao binafsi, zinduka

Asante
Inasikitisha, ucha Mungu unapokuwa chanzo cha kukosa utu badala ya kukuzidishia maarifa.
 
Kuhusu swala la jeshi la soviet russia kupigana front line hilo ni uongo, wao walikuwa wanaleta wataalamu wa vita (technical advisors) kidogo na marubani katika strategic positions tu

Ndio maana katika wanajeshi 11k angola 54 tu ndio walipoteza maisha na wote sio katika direct kombati bali magonjwa mengine tofauti katika hiyo miaka minne ya vita Angola

Hawa wa siku hizi Wagner group ndio wanakichafua kokote yani ni wapiganaji wa kulipwa kwa lugha fasaha ni majasusi na ni watu wa mataifa mbalimbali kote duniani
Sio majasusi, askari wa kukodi "mamluki" aka "mercenaries"
 
Familia ya Mtanzania Nemes Raymond Tarimo (34) ambaye ameripotiwa kufariki wakati akipigana upande wa Jeshi binafsi la Urusi la Wagner Group dhidi ya Ukraine, imesema haifahamu ni nini kimempata Kijana wao hadi kufariki kwakuwa wanachokifahamu wao ni kwamba Nemes alikuwa anasoma Urusi na wameshangaa kuona akiagwa kijeshi.

Video ambayo imesambaa mitandaoni inawaonesha Wapiganaji wanaominika ni kutoka Wagner Group wakimuaga Nemes Tarimo ambapo amepewa pia nishani baada ya kudaiwa kufariki vitani katika shambulio la Bakhmut Mkoa wa Donbas mashariki mwa Ukraine.

Mjomba wa Nemes, Andrew Mwandenuka akiongea nyumbani kwa Familia ya Nemes Dar es salaam leo, amesema Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi umeiambia Familia kuwa mwili wa Nemes utakapofikishwa Tanzania wataelezwa ni nini kimempata Kijana wao.

Jitihada za kuupata Ubalozi wa Tanzania katika Shirikisho la Urusi ili kupata taarifa za tukio hili hazijafanikiwa huku Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukisema unalifanyia kazi suala hilo.

Yapo madai ambayo hayajathibitishwa yanayodai Nemes alifungwa Jela na baadaye alipewa nafasi ya kutoka jela kwa sharti la kujiunga na Jeshi hilo lakini Familia inasema haina taarifa za kwamba Nemes alifungwa wala kujiunga na Jeshi na inachokifahamu ni kwamba alikuwa Mwanafunzi.

chanzo
#MillardAyoUPDATES
Kijana alikuwa mzalendo wa Urusi
Anampigania Putin
Ataletwa na mshahara wake wa jeshi la kukodiwa
 
Back
Top Bottom