Ndugu zangu mie nasikitikana sana mara kwa mara nikisikia mawaziri wakisema ooh serikali inatambua kuwa kuna uhaba wa vitendea kazi mashuleni?Sasa swali la kujiuliza kama kweli wanatambua hilo ni kitu gani kinawafanya wasinunue vitendea kazi hivyo?Pili nilimshangaa sana waziri wa Elimu anasema ati serikali imedhamiria kutumia hela ya chenji iliyorudishwa kutoka England ili itumike kununulia vitendea kazi kama vitabu nk.Swali lingine je kama kusingekuwa na chenji hizo wangefanyaje? Na je bajeti ya Elimu au ya kuboresha Elimu iko wapi?na kama wanatumia cheni hiyo zitakwenda wapi zile fedha ambazo zilishapitishwa kwenye bajeti???Naomba ushirikiano wa kudiscuss, hii ni kwa maendeleo ya nchi yetu tuweke siasa pembeni Ahsanteni:crying: