Inachekesha sana namna ambavyo wanaume tunageuzwa misukule na wanawake bila kujua

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Nipo tayari hata kuambiwa kuwa haya ni maneno ya mkosaji. Hali tuliyofikia, inachekesha sana aisee. Wanaume, wanaume, wanaume... Tupunguzeni kujishusha

Yaani unakuta mwanaume anajitutumua kurusha salamu za kila rangi kwa mwanamke, hata asipojibiwa, anasindikizia maneno ya unyenyekevu na kuomba japo ahurumiwe. Wacheni tu niwe mwanaume wa tofauti

Hivi hawa viumbe waliwapa nini kwani. Nina rafiki yangu, aliniazima Tsh 5k ili asukumie dinner. Ile time namkabidhi, inaingia simu ya kibinti. Binti anadai hela akaweke protector kwenye simu yake. Huyu mshenzi akaituma kisha kurejea home kwake kulala na njaa. Aisee. Wamewapa nini?

Yule binti niliewaomba ushauri wa kumla nilimsikia akimtukana mwamba kwenye simu siku ya jana usiku. Mwamba mpaka anaitwa Mpumbav, yeye yumo tu. Hivi mnajua kutukanwa kama mtoto!!? Jamaa aliyaoga ya kutosha

Dah! Mola anisaidie nisiwe mwanaume Jalala kwenye maisha yangu. Nitapiga niue
Nowdays, nikiona mtu anampiga mkewe huku akiwa hajalewa, huwa nakimbilia chupa la K Vant dukani pamoja na chapati mbili ili akimaliza kazi ajipongeze

Zamani nilidhani wanaonewa tu. Mwanamke mwema ni anayetokea Buhongwa pekee. Hawa wa Dsm ni pasua kichwa

Ila wanaume tuacheni kuwanyenyekea wanawake
 
Back
Top Bottom