Ina maana hili Taifa limekosa watu waliofanya makubwa katika mpira wa Tanzania mpaka watu wa hamasa wanachaguliwa Mwijaku na Baba levo?!

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,288
12,789
"Suala la mpira wapewe watu wa mpira na suala la uchawa wapewe watu wa uchawa."

Wizara ya Sanaa na michezo ijitafakari sana katika hili.

Hili Taifa Lina watu (Legends) waliofanya makubwa katika taifa hili Tena kwa kuichezea Timu Yao ya Taifa na walikua na mvuto mkubwa sana uwanjani lakini taifa Leo hii haliwatambui kabisa.

TFF imelala tu na kufunika majina ya malegend waliofanya makubwa Tena wapo hai na nguvu wanazo Wanaweza KUPEWA ubalozi wa Hamasa na wakahamasisha vizuri tu.

Mwijaku na Baba levo Hawa wanjua Nini kuhusu??

Na kwa Nini wapewe wao kigezo gani kimeangaliwa??

Kwa nini wachezaji Pendwa Kama wakina Mrisho Ngasa, Juma kaseja Amri kiemba n.k wasiingizwe /KUPEWA hiyo kazi ya Kuhamasisha Mashabiki kuipenda timu ya Taifa kuelekea kwenye michuano ya AFCON??

Mambo ya kimpira mpira tuweke watu wa mpira hii itapendeza sana kuliko kuleta watu/machawa ni sawa na kushusha hadhi ya mpira wetu.

Kuelekea Dabi ya kariakoo huwa naona Malegend waliocheza Simba sc na Yanga Sc huwa wanahojiwa na kusimulia yaliyopita kipindi wapo uwanjani, Sunday Manara na wengine huwa wanahojiwa.

Maoni Yangu: Mambo ya mpira yaende kimpira na Mambo ya kichawa yaende kichawa chawa,

Legends wahusishwe wenye hamasa ya Timu ya Taifa siyo kuwatafuta kipindi Cha Kariakoo Dabi tu na kwenye Mambo mengine mnawapa Baba levo na Mwijaku.

Nawasilisha hoja.
 
Sijui kwanini nakujibu ila wacha tu nikujibu.

Nadhani wamelenga kijiditali zaidi. Mwijaku, bb levo na joti wanafollowers mamilioni huko kwenye udaku wa soshomedia. So kuwatumia hawa kutaleta impact kuliko hao malejendali wa soka ambao wanafahamika na wachache. Hao wapuuzi wanaowafatilia kina mwijaku na upuuzi wao ndio target ya hamasa.
 
HIYO SIYO SABABU MZEE TFF WANAKWENDA KIMICHONGO MICHONGO TU MZEE.
 
Sijui kwanini nakujibu ila wacha tu nikujibu.

Nadhani wamelenga kijiditali zaidi. Mwijaku, bb levo na joti wanafollowers mamilioni huko kwenye udaku wa soshomedia. So kuwatumia hawa kutaleta impact kuliko hao malejendali wa soka ambao wanafahamika na wachache. Hao wapuuzi wanaowafatilia kina mwijaku na upuuzi wao ndio target ya hamasa.
Sababu mfu
 
Hebu tusaidie sisi tusioelewa soka la bongo vizuri, wanahamasisha Nini kati ya hivi; Wanahamisha wachezaji wakacheze vizuri tushinde au washabiki twende uwanjani tukatoe hamasa. Then nina swali nikipata jibu
 
Sijui kwanini nakujibu ila wacha tu nikujibu.

Nadhani wamelenga kijiditali zaidi. Mwijaku, bb levo na joti wanafollowers mamilioni huko kwenye udaku wa soshomedia. So kuwatumia hawa kutaleta impact kuliko hao malejendali wa soka ambao wanafahamika na wachache. Hao wapuuzi wanaowafatilia kina mwijaku na upuuzi wao ndio target ya hamasa.
Kwahiyo, hao kina Mwijaku na wajinga wenzao wanahamasisha Mashabiki na sio Hamasa kwa Timu ya Taifa, kwa maana ya Morali kwa Wachezaji Ili wacheze kwa Ari na kujituma Ili timu ipate matokeo...!

Hii Hamasa imekaa kimchongo...na inafanyika Tanzania pekee nadhani.

Ujinga sana
 
Kwani hii hamasa ya nini?
Kama pesa si wanapewa za michuano?
Au kuna nini cha zaidi?
 
Back
Top Bottom