Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,634
- 46,277
Huwa naona wachezaji mpira wakisali kabla ya kuanza kucheza, pia katika nchi kama yetu huwa nasikia wadau, viongozi wa serikali, timu na mpira kwa ujumla wakihamasisha raia waiombee timu ya taifa au vilabu vyao pendwa vishinde mechi.
Ikiwa upande wa pili wa timu pinzani nao itafanya au unafanya hivyo haya si yatakuwa mashindano ya kusikilizwa kwa sala au dua?
Je hii inakuwa na mashiko yoyote katika timu kushinda au kushindwa?
Mungu anakubali maombi ya aina hii ya kuiombea timu nyingine ishindwe?