Imani katika Sheria kama chombo cha kupambana na ufisadi

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,457
956
Mpaka sasa wananchi wameweza kuona ni kwa jinsi gani matatizo yanayoikumba nchi yetu yanazidi kuongeza licha ya kuwepo sheria, vyombo na taasisi mbalimbali za kisheria zenye nguvu na mamlaka ya kuyashughulikia.Wapo wenye kuamini kwamba maadam kuna sheria na vyombo hivyo, basi mafisadi watakiona cha moto.Kwani Sheria ni nini, ni za nani na kwa manufaa ya nani?
 
sheria zinatungwa na matajiri kuwazuia maskini kuwasogelea matajiri na kuhakikisha matajiri wanaendelea kuwakandamiza maskini. Zinatungwa ili kuwapa maskini kiinimacho cha utajiri! Mara zote sheria zinatungwa kuwafurahisha matajiri na kuwaridhisha maskini lakini wakati wote kuwanufaisha watawala!
 
ha ha ha... i guess vita vya ukombozi vitajirudia, maana tunaishi katika maudhui ya zile riwaya za kusadikika, kuli, duka la walaji etc
 
Mpaka sasa wananchi wameweza kuona ni kwa jinsi gani matatizo yanayoikumba nchi yetu yanazidi kuongeza licha ya kuwepo sheria, vyombo na taasisi mbalimbali za kisheria zenye nguvu na mamlaka ya kuyashughulikia.Wapo wenye kuamini kwamba maadam kuna sheria na vyombo hivyo, basi mafisadi watakiona cha moto.Kwani Sheria ni nini, ni za nani na kwa manufaa ya nani?

Mimi si mwanasheria lakini nitajaribu kuyajibu maswali yako kwa kutumia uwezo wangu binafsi wa kuelewa.

Sheria ni mfumo wa utaratibu ambao jamii fulani imejiwekea ili kudumisha utulivu na kuwalinda watu au vitu.

Katika kujibu swali lako la pili la sheria ni za nani, kama ambavyo nimeeleza kwenye jibu langu lililotangulia, Sheria ni mali ya jamii fulani husika ambayo imejitungia.
Kwa mfano, sheria zetu za Tanzania ni mali yetu sisi watanzania kwa ajili ya kuzifuata ili tuweze kudumisha utulivu ndani ya jamii zetu na pia kutulinda sisi wenyewe na mali zetu.

Sheria zote ambazo jamii husika imejiwekea ni kwa matumizi na manufaa ya jamii hiyo. Ni wazi kabisa kuwa katika matumizi au utekelezaji wa sheria kuna pande mbili kubwa ambazo ninaziona ni muhimu.
Kwanza, wananchi wenyewe ambao wanatakiwa wazitumie (apply) katika shughuli zao za kila siku. hapa nina maanisha kuwa jamii inapaswa kuhakikisha inazingatia sheria na kuzifuata.
Upande wa pili kuna vyombo vya kusimamia sheria hiyo. Hizi ni taasisi muhimu ambazo kazi zake ni kutoa tafsiri na kusimamia utekelezwaji wa sheria.
 
Na-assume hapa zinazozungumziwa ni sheria za nchi. Mara nyingi sheria huwa hazina matatizo sana, ila uzuri wa sheria inabidi viende sambamba na umakini na umahiri wa enfocer. Enforcer inabidi awe na will ya kutenda haki na bila kuangalia usoni mlalamikiwa au mlalamikaji.

Nadhani ktk nchi yetu tatizo kubwa lipo kwa law enforcers.
 
Sheria ni ile mambo ya kumfunga mama ntilie miezi sita gerezani kwa kosa la kuuza chakula mtaani, na kumwacha fisadi anaingia hadi bungeni, anachangia hoja na inapigiwa makofi. Hii ndo sheria mzee...
 
Sheria ni ile mambo ya kumfunga mama ntilie miezi sita gerezani kwa kosa la kuuza chakula mtaani, na kumwacha fisadi anaingia hadi bungeni, anachangia hoja na inapigiwa makofi. Hii ndo sheria mzee...

Sheria ya Tanzania only,
Ni maandishi yaliyo jaa kwenye makaratasi kwa ajili ya kuwahukumu wezi wa kuku na mikungu ya ndizi na wagombania mabwana na mahawala!

Sheria hizo ziko tayari kwa ajili ya kupindishwa na kuwaacha mafisadi mtaani wakipeta huku wakiishi juu ya sheria hizo. Inapo bidi sheria mpya hutungwa chap chap kuhakikisha 'ruling class' haisumbuliwi wala kusemwa vibaya wala kutishiwa kuondolewa madarakani (eg mgombea binafsi)
 
sheria ni kwa manufaa ya anaye zitunga na anao watetea. Iwe ana tetea wananchi, makundi fulani au kutetea maslahi yake mwenyewe.
 
Tafsiri mojawapo ya sheria ni:
"Sheria ni chombo cha mabavu cha dola".

Kama ni chombo cha dola tena cha mabavu sisi kupitia wabunge wetu tunatunga sheria na kuwaachia watafsiri sheria, ( mahakama) kuzitumia hizo sheria kwenye kesi/mashauri mbaimbali - ya madai na ya jinai.

Katika kutekeleza sheria kuna vyombo vingi na michakato mingi.Je mwisho wa siku tunapata nini? je ni kweli kuwa tunatunga sheria zenye kuwakilisha matakwa na matarajio yetu? Je, wanaotafsiri hizo sheria, sisi kama wananchi tunawawajibisha vipi? ( nauliza maswali haya ya kifilosofia kuchagiza mjadala)
 
... sisi kupitia wabunge wetu tunatunga sheria

La hasha.

Bunge letu sio la kutunga sheria bali ni muhuri, rubber stamp, ya miswaada au hoja chovu yeyote ya serikali. Mara ya mwisho wabunge kutunga sheria wenyewe ilikuwa zaidi ya miaka kumi na mbili iliyopita, 1997 ( sheria ya Balozi P. Ndobho, NCCR Musoma Vijijiji, sheria ya A. Mrema, NCCR Temeke, sheria ya J. Mungai, CCM Mufindi Kaskazini ) na ukienda nyuma zaidi, 1995, sheria ya Jenerali Ulimwengu, CCM Taifa. Wabunge wanne tu kati ya mamia na mamia ya wabunge waliopata kuchaguliwa miaka 20, 30 iliyopita.

Aibu.
 
Pamoja na kuchagiza mjadala, je hiyo tafsiri ni rasmi? Je, unaweza kutupatia link ili nijiridhishe na tafsiri hiyo?
 
Hapo sasa....
BTW...umenikumbusha enzi za Party supremacy..je Tanzania which organ is supreme..is it the Legislature, Executive or the Judiciary?
 
Pamoja na kuchagiza mjadala, je hiyo tafsiri ni rasmi? Je, unaweza kutupatia link ili nijiridhishe na tafsiri hiyo?

Hii ni mojawapo ya tafsiri za legal positivists wa mwanzo - you can read works of John Austin na Jeremy Bentham..kama unapenda kuelewa zaidi.Au uliza wanasheria waliomo humu maana hata mimi siyo mwanasheria hahahaha ila nina interest kwenye sheria.
 
Back
Top Bottom