Imaginations: Comments za members wa JF yenye verified accounts

Fohadi

JF-Expert Member
Jul 24, 2020
770
2,408
Sasa hivi kila mtu JF ni mbabe, analeta fiction stories, anaandika anachojisikia kwa sababu asilimia kuwa ya members tunatumia fake IDs.

Nawaza ile mara ghafla kila member analog in anakuta amekuwa verified kwa jina lake halisi, hapa najua hapatakalika. Sio nyumbani, sio makazini na wala sio humu ndani. Kuna watu watajikuta walizama PM za wazazi/watoto wao kutongoza, kuna watu watajikuta walitukanana na Baba wenye nyumba zao hapa jukwaani.

Kule nyumbani sasa ndoa hazikaliki. Mke anagundua mmewe kala kimasihara matunda kibao, Mme nae anagundua mkewe ashaliwa mara kibao. Kazini nako maboss watagundua jinsi gani walikuwa snitched na waajiriwa wao. Yaani vita ni vita mura. Hatujakaa sawa tutagundua Kidukulilo alituleteaga fix kibao kama bwana Kilewo na Bibie joyce. Kumbe kidukulilo ni graduate mmoja kigoma anatafuta ajira.

Mara tunagundua kumbe BABA KANYA na BABA KHUMBU hata south beach hajawahi kufika. Watu kama warumi, sijui wataficha sura zao wapi kwa udaku waliowahi kuumwaga.

Comments za wadau humu ndani ndio zitakuwa balaa makavu live maana wanajuana. Hujakaa sawa utasikia;

Extrovert: Kumbe ndiyo wewe Bujibuji uliekuwa unanitolea kauli chafu hapa jukwaani? sasa omba usikutane namimi kule minazini mtaani kwa mzee mtokambali.
Madame B: Yaani kumbe Kigakoyo ulitembea pia na shemeji yako, uliona raha kula kuku na mayai yake?, nilikuona mkwe mwenye busara kumbe bogus, sasa naomba achana na mwanangu haraka sana.

Comments za wadau zitakuwa balaa..hebu tucomments kama tuko kwenye JF yenye verified members


 
Back
Top Bottom