Ilinilazimu kutoa rushwa ili kunusuru kazi yangu (trafiki na mradi wa tochi za barabarani)

araway

JF-Expert Member
Sep 26, 2007
534
144
nilipatwa na dharura iliyonifanya nisafiri toka mwanza kwenda dar na kurudi siku ya jumapili juzi ili niwahi kibarua changu ambapo nilitoka bila kuaga katika kituo changu cha kazi.

namshukuru mungu nimerudi salama na sasa nipo kwa kibarua changu. kilichonisibu na hadi kufikia kuandika haya niyasemayo ni huu mradi unaoendeshwa na jeshi la polisi kitengo cha askari wa barabarani (traffic police). kutoka dar-mwanza nimekutana na zaidi ya vizuizi kumi vyahawa jamaa na nilibahatika kusimamishwa zaidi ya mara nane tangu mwanzo wa safari hadi mwisho , na ilinigharimu shilingi 45,000 kama rushwa kwa hawajamaa wanaojiita wazee wa fweza. na ilinikost takriban dakika kumi hadi nusu saa kwa baadhi ya maeneo kubargain kiasi cha rushwa walichokuwa wanaitaji na kwa kuwa nilikuwa nasafari ndefu na usumbufu na kero waliokuwa wananiundia sikuwa na ujanja zaidi ya kuwapa rushwa ambayo naamini wakubwa wao wanahusika katikaa hili moja kwa moja.
makosa ambayo walikuwa wananibambikia karibu yote ni mwendo kasi! hapana siwezi kuuita mwendo kasi ni mwendo zaidi ya km 50 kwa saa na chini ya 80km kwa saa kwa maeneo ambayo hayaruhusiwi.

balaa lilinianzia picha ya ndege baada ya sheli nilikutana na askari wawili wa kike na mmoja wakiume walinisimamisha na mimi kwa kutii amri yao nilisimama na kosa walilonipa ni kuovertake kwenye daraja, kiukweli sehemu wanayoita daraja sina hakika kama kweli ni daraja zaidi ya kuona kingo za pembeni za barabara baada ya kunisumbua kwa muda mrefu niliwapa elfu 5000 wakaniachia .

embu nikatafute msosi ntarudi kuendelea na yaliyonikuta.....
 
pOLE hAO nDIO aSKARI wETU wASIOwEZA kUWAKAMATA wANAOCHINJA vIONGOZI wa kIKRISTO wANABAKI kUHANGAIKA NA wENYE mAGARI bARABARANI.

sHAME oN tHEM aLL.


Bazazi>
 
Back
Top Bottom