Bei ya mafunta yapanda laandika gazeti la leo 'The Guardian". Bei ya mafuta nchi nzima imepanda ghafla na sasa inauzwa kati ya Tshs. 1,600/= mpaka 1,800/= kwa lita moja ya mafuta aina ya petroli kutoka kwenye wastani wa Tshs. 1,400/= mwezi uliyopita. Kulikoni? Tatizo ni uwezo mdogo wa bandari katika kupakua mafuta? Je, Tatizo ni TRA? au tatizo ni wafanyabiashara katika kustage 'shortage' ya mafuta? Kumbuka walianza kwa kudai kwamba bandari inawachelewesha katika kupakua mafuta. Wengine walienda mbali na kudai kwamba 'meli ya mafuta ya IPTL ilipewa kipaumbele'. Duh utafikiri tuko land locked, yani lita ya petroli ni zaidi ya dola moja Dar es salaam.
Kwa mwendo huu maendeleo Tanzania yatabaki kama msamiati wa kigeni.
Kwa mwendo huu maendeleo Tanzania yatabaki kama msamiati wa kigeni.