Ili Magufuli aibadilishe Tanzania, ni lazima awe Rais kwa zaidi ya miaka kumi

Are we prepaired to take that chance kuwa JPM will be alive for the next 20 to 30 years to come??Can this country rely on that?I think no!
Kwanini tusitengeneze mfumo imara badala ya kutegemea mtu mmoja?
Mkuu, death ni kitu kingine. Na sio kwa Magufuli tu, whether you have 10 or 50 years of presidency
 
Anapewa vipindi 4, ikitokea wapinzani wakapata viti vya bunge 55% na wakaja na hoja ya kuokuwa na imani na rais, kinatokea nini hapo?

Mchezo unaanza upya!;)

Mkuu, note kwamba nilisema huenda tukienda huko tuunganishe vyama vya siasa kwanza, ili wote tuzielekeze nguvu zetu katika lengo moja.
 
Ukabila nao umo, undugu usiseme, huyo ndo JPM halafu umpe miaka 20?? Hainiingii akilini.

Niambie kutoa Nyerere, ni raisi gani wa nchi hii hakufanya uteuzi kufuata ukabila, udini na undugu, na ikiwa Magufuli ndio anaongoza kwa hili. Kuna marasisi hata walichagua wapwa kuwa wakurugenzi, wengine mashemeji kuwa mawaziri, wengine waume wenza, yaani, huko wala usiende.
 
Mkuu, death ni kitu kingine. Na sio kwa Magufuli tu, whether you have 10 or 50 years of presidency
So kwanini tusijenge mfumo imara badala ya kutegemea uhai wa mtu mmoja?Hilo nadhani ni la msingi zaidi,tukifanikiwa hilo tutaweza kuwa hata na mgombea binafsi!
 
Mkuu, simaanishi systems unazozisema wewe - infrastructure. Namaanisha organizational, administrative, legal na management systems.
Labda system ya kuweza kuendelea kubaki madarakani zaidi ya miaka 10,hivi inawezekanaje mtu hajamaliza hata miaka 5 ambayo walau tungeweza mpima kwa milestones alizozifikia tayari mnaanza kushauri atawale zaidi ya miaka 10,thats some bull crap,acheni kwanza ipite miaka mitano tuone amatufikisha wapi
 
Mkuu, kama ikibidi Magufuli aongezewe muda, hawezi kuongezewa muda bila kubadilisha katiba. Believe me, kubadilisha katiba ili magufuli aongezewe muda ni kitu kidogo sana. Huenda kikao kimoja tu cha Bunge. Katiba haiko cast in iron my friend, sio msaafu ule. Usijikite sana katika kufikiri ni jambo ambalo haliwezekani. Na kumbuka BUnge lina wingi wa wabunge wa CCM ambao Magufuli anaweza kutumia watu wake watoe hilo pendekezo na likapita.

Katika Afrika, suala la kuongezewa au kutooneza muda wa vipindi vya uraisi ni raisi alieyepo madarakani anaamua, ili mradi anajua chama chake kitamuunga mkono. Au hukuona Rwanda?
Sawa hilo linaeleweka kuwa katiba inaweza kubadilishwa,lakini hizi time limits za ngwe za kutawala hazikuwekwa tu kimakosa ama bila sababu ya msingi,sasa unapobadili kipengele kama hichi lazima ulete sababu ya msingi ya kujustify mabadiliko hayo,pia lazima uelewe kwamba serikali ni mfumo,sio mtu mmoja sasa kama unaona jamaa anafaa sana basi atengeneze mfumo mzuri ambao hata akimaliza mikala 5/10 utaweza kuiendesha nchi vizuri hata bila ya yeye kuwapo.
 
Nimebaini kuna baadhi ya member huwa wanafungiwa kimakosa. Mtu unaweza jikuta unachangia kwa lugha isoyo kuwa ya staha kutokana na mada husika kukuchefua ama kuwa ya kukinaisha kiasi kwamba badala ya kufikiria huenda uelewa tunatofautiana ama ni mtu kafanya maksudi kabisa kwa kile aonacho yeye kinamnufaishaje. Na hili suala la watu kutembea na move sijui litaisha lini.
Tuliambiwa aliye pita yuko vizuri kuliko tulivyo dhania hadi kuelezwa kuwa ni chaguo la Mungu. Hadi kuelezwa kuwa pasipo kusafiri nje huwezi kuendesha nchi baada ya wingi wa safari kupigiwa kelele. Leo huyu hasafiri pamoja na mambo yote wanageuka na kusifia hadi kuomba hata katiba ibadirishwe ili awe wa kudumu. Ghafla tumekuwa na mawazo ya kiimla!!?
Sisi ni taifa la kifalme ama? Wamepita wangapi?
Na yeye kapatikana kutoka kundi la watu wangapi? Hata kama ni mzuri kama mnavyo taka wote tuamini.
Mmetupima kwa kipi hadi kujua ktk raia wote tulio baki hakuna mwenye uwezo zaidi yake?
Dah! Nchi yangu Tanzania. We have a long way to go!
 
Magufuli ni Rais mzuri sana na anakubalika na kuheshimika kila sehemu hata nje ya Tanzania

Lakini akitaka kuharibu sifa yake Basi abadilishe katiba na kutaka kugombea miaka kumi mingine.

Pia Rais akumbuke kwamba maadui wake wengi wanatoka ndani na si nje hivyo akikosea tu hao hao wa ndani ndio watamharibia

Wananchi sio maadui wa Rais kwani ni wachache sana wenye kumchukia lakini wengi wanampenda na kumkubali.

Rais ana mapungufu yake kama binadamu na kama tutataka Rais asie na mapungufu Basi tuchague Rais Rais malaika atuongoze, vinginevyo Rais yuko vizuri na anapiga Kazi vizuri sana.

Kuna baadhi ya mambo Rais kama akibadilisha basi sio yeye atakaomba kugombea miaka zaidi ya kumi Bali wananchi wenyewe watamuomba afanye hivyo.

Naweza kuorodhoresha mambo hayo.

1. Njaa na maisha kuwa magumu ni janga la Taifa, kama Rais atarekebisha maisha hilo wala hatokaa asiekie kelele za wananchi ye aendelee na madaraka yake.

2. Visasi..... Kuna kauli nyingi sana zimeenea sehemu nyingi kwamba Rais wetu ni mtu wa bifu na unatumia madaraka yake kumkomesha mtu ambae ana bifu nae, kweli hili ni jambo baya na sidhani kama Rais ana tabia hiyo ila lisemwalo limo. Tumesikia katika issue ya Manji kuwa ni uonevu na issue nyingine , sasa Rais kama Rais vizuri angesimamia kauli yake Siku anaapishwa tulofurahi sana aliposema yeye ni Rais wa watu wote, Chadema,Cuf, Tlp na hata wale wasiokuwa na chama yeye ni Rais wao, kauli hii ina maana kubwa sana kwa ndani

Katika maana yake Mimi nilielewa Rais anaaanisha kuwa Mimi ni Rais ya hata wale wanaonichukia na walinikwamisha katika kampeni zangu Leo nimekuwa Rais siwezi kuwasumbua kwa lolote lile labda kama wataendelea kunisumbua nikiwa teyari ni Rais. Ukishakuwa Rais basi wewe una nguvu kubwa sana ya kifanya chochote kile na hawao kina Manji ni watu wadogo sana kwako basi waangalie tu na kuwasamehe.

3. Mimi sio chama pinzani lakini naamini tumefika hapa kwaajili ya wapinzani, hivyo wana nafasi zao katika moyo zetu, mfano mambo mengi sana mabaya yanayofanywa na CCM tunayajua kupitia wapinzani, na CCM inayarekebisha kwa kuogopa wapinzani kupiga kelele, hivyo sina hakika lakini kama kweli Rais unawaminya wapinzani tunaomba uwaachie kidogo bora wasivunje amani.

Pamoja yote hayo Rais ana positive result nyingi sana tumeziona na tunamuunga mkono sana aendelee

Ushauri

Rais aandae mtu ambae atakuwa kama yeye na atafanya Kazi mzuri kama yeye nafikiri Waziri mkuu anaweza kuwa Rais baada ya Magufuli, lakini Leo tumepata Rais mzuri mnasema abadilishe katiba na agombee miaka 20 Je sindio itakiwa system ya kila Rais akishakuwa ktk power anabadilisha katiba?


Tanzania yetu itaishia katika vita vikubwa sana, tusikubali kitu cha namba hiyo
 
Rasimu ya Warioba iwe katiba, Tume huru, bunge huru, mahakama huru na serikali yenye miundo imara ya kufanya maamuzi na checks and balances. Kwa mfano CAG aliye na kamati yake na wakitoa maamuzi ya accounts hakuna wa kumbishia. Raisi lazima awe na kitu kama congress juu yake inayomthibiti ambayo imechaguliwa na watu pamoja na kuwa na wabunge wanaoweza kuthibitiwa na watu waliowachagua.
Tanzania must griw we cannot go back 50 years and feel happy that thinga are going right.
Just because they are right for you it does not mean that they are right for others.
Haya mambo ya rais ama waziri kufanya kazi nzuri ni sawa na hii iwe ni madai yetu kwa yeyote tunayemchagua. Hii siyo tuzo ni wajibu.
Kama kweli magufulini kiongozi na siyo dikteta kama wengi wanavyodhani basi aweke hizo systems na awe tayari kuondoka wakati wake ukifika.
Rais asiyependa kupingwa hata ndani ya chama chake nina wasiwasi naye kabisa.
Already nchi hii watu wake hawana furaha kabisa. Hospitali asili mia ya wenye pressure imeongezeka sana.
Please wahurumieni watu!!!!
 
Wasomi wote tudai rasimu ya warioba iwe katiba, tudai tume huru. Tuache huu uzembe tunaotaka kuleta wa kurudisha democrasia ya nchi nyuma.
Katika watu milioni 50, tuseme watu wazima milioni 40 hatuwezi kusema kuwa kutakosa mtu mzuri. Kila miaka mitano ama kumi.
Hilo wazo la kuongeza muda lifutwe kabisa kwani kikomo ni miaka 10 and full stop.
Hakuna watu wanaoomba.
Kwa kawaida ni mtu mwenyewe analobby kisirisiri kwa rafiki zake.ama mtu moja anayetaka kujipendekeza anaanza uzi hui na mwenyewe rais anayetawala anapata tamaa na kuamini kuwa kweli yeye ni mzuri kuliko wengine.
Tusirudi nyuma.
Tanzania ilikomboa nchi nyingi za kiafrika tusikubali kurudi nyuma kidemocrasia.
Tunachohitaji ni elimu elimu elimu kuanzia chekechea kuhusu uzalendo, ethics za kazi na accountability. Hii tu ndiyo misingi ya utawala bora hakuna kingine.
 
Mkuu kwanza nikupongeze kwa makala ndefu
Lakini umetolea mfano way out of context
1. Singapore na Malysia huwezi kuziweka kwenye kundi moja la maendeleo hutajifunza kitu hapo, Singapore wako mbali hadi basi yaani
2. Singapore waliendelea kwa ku take advantage of their location, wali tengeneza bandari zao, viwanja vya ndege , walipunguza kodi na regulations za ajabu, wali ifumua elim yao na kuilenga kwenye kuvutia uwekezaji, wao walikuwa ni urban country toka kitambo lakin pia serikali ilipiga kazi kwenye kuwekeza.
2. Malaysia wao wana natural resources kama sisi bongo, halafu wao kidogo hata system zao za siasa ni ngum kidogo na kuna mchanganyiko wa watu mbali mbali so ku wamange ni shida, Malaysia wao wali anza kama Magufuli eti wanatoa rushwa, lakini wataalam wao waka waambia hakuna correlation kati ya rushwa na umaskini wao, walicho fanya ni kuwekeza kwenye madini na mafuta na kilimo, waka ifumua elimu yao na kuwekeza kwenye sayansi mfano kila mwaka wanafunzi wanao graduate vyuo vikuu asilimia 30% wana graduate mechanical engeneering, waka wekeza kwenye kujenga miundo mbinu mizuri kwa ajili ya uwekezaji, pia waka weka mazingira ya kuvutia wataalm wa nje kwenye nafasi za juu za makampuni yao. Japo Malaysia wanakua kwa kasi bado haija ingizwa kwenye kundi la developed countries.

*japo umejitahidi kumtetea Magufuli hakuna chochote anacho fanya kinacho endana na Malaysia, singapore ndio kabsaa. So sijajua case ya Rwanda labda wenzetu walifanya anacho fanya Magufuli. Lakini this man is failing moja kwa moja
Unaonekana ww ni mpinzani, na si mwana maendeleo jamaa kaandika uzi mzuri kwa sababu ww ni mpinzan bac unapinga so hebu wapinzani siku muandike uzi ambao unaonesha mikakati ambayo inatakiwa ichukuliwe ili taifa letu lipige hatua ili tu compare na hii ya sasa na iiiyopita
Sio mnakuwa mnatafuta kiki kwa kupinga vile ambavyo watu wanajitaidi kushauri
Mfano wa vitu vilivyopigwa pasipo kuleta mkakati mbadala wa kutatua :
Vyeti feki
Watumishi hewa
Mimba mashuleni
Makinikia
 
Nimefuata mtoa maada alicho kisema tena nimetoa na mfano,
Wenzenu malaysia walidhani ufisadi ndio chanzo cha umasikin wao lakin waliambiwa sio.
Nimetoa mfano jinsi walivo tumia madini na kuimarisha muliundo mbinu.
Wenzetu walibadilika ki sera, sasa magufuli sera gani au sheria gani kabadilisha!!, wao walishusha kodi na regulatuons pia.
Hivi Magufuli kabadilisha nini!!? Sheria gan imechange!!?,sera ipi ime change, tuna faidika na madini?, umeona elim kama ina badilishwa!!?

Mi siyo hater wa Magufuli nimecheki mada nimeunganisha facts nimeona hakuna anacho fanya.
Mfano:waki isha wafanyakazi hewa tuta faidikaje ki uchumi!!?

So utafaidikaje na madini wakati mikataba ilikua inatunyonya so amebadili sheria so hapo je...
Na kwa akili ya kawaida ,hizo pesa zilizokuwa zinatumika kulipia watumishi hewa saiv zitakuwa zinawafaidisha wa kenya kiuchumi?
Na ufisadi sio chanzo cha umaskini?
 
Ni upuuzi mtupu kuilinganisha Rwanda na Tanzania.

Rwanda ni kama kamkoa kamoja tu ka Tanzania .
Hatuwezi kuilinganisha Rwanda na Tanzania.
Rwanda wanatumia kila mbinu kuihujumu kongo na rasilimali zake.
Kwa hiyo hatuwezi kujilinganisha na kanchi ka kiporaji.
Kujenga Barabara ya Lami kutoka Mtwara mpaka Karagwe ni sawa na kujenga barabara zote za Rwanda mpaka zile za majumbani kutoka jikoni kwenda chooni kwa kiwango cha lami. Gharama za Kutoa umeme wa gridi ya Taifa kutoka Ubungo mpaka Mwanza ni sawa na kuwawekea wanyarwanda wote umeme na vyombo vya umeme bure majumbani mwao.

Kujenga Bomba la Ges kutoka Mtwara mpaka Dsm ni sawa na kumpatia gesi ya bure kila mnyarwanda nyumbani kwake.
Kujenga Bomba la maji toka ziwa viktoria mpaka Kahama ni sawa na kumwekea maji bure kila Mnyarwanda.
N.k.n.k.
Kulinganisha Rwanda na Tanzania ni sawa na kulinganisha jua na Karabai.

Kuhusu Magufuli kutawala zaidi ya miaka kumi hiyo ni kauli ya uchochezi na ya kitoto kabisa.
Tatizo la waafrika ni unafiki.
Hata kundi la JK nao walimfurahia sana na kumwona kuwa ameiletea Tanzania na watanzania maisha bora na maendeleo makubwa.
Tatizo kila mtu anampenda kiongozi anayetawala kutokana na nafasi anayopewa. Ukipata ukuu wa wilaya kwenye awamu inayokuwepo basi unatamani aliyekuchagua aishi na kutawala milele.

Nyerere alipotaka kustaafua aliwaambia waliokuwa wanamsifia na kumtaka asing'atuke kwa kuwcla eti hatapatikana wa kuongoza nchi, aliwaambia kuwa wanataka aendelee kwa sababu wanahofia kupoteza nafasi zao.

Uislam ni dini inayokua kwa kasi sana na kila muislam muda wote anailinda na kuinusiru dini yake kutokana na sheria za dini hiyo ndani ya koran. Sheria na Katiba ndio kitu cha muhimu sana kwa nchi yenye watu wa dini na makabila tofauti.
Kama Magufuli anataka kuiacha nchi vizuri au kuinyoosha vizuri basi alete maadili na miiko ya uongozi kwenye katiba ili kila mtu ajipime kama anastahili kuwa kiongozi.
Kwa sasa kuna watu bado hawastahili kuwa madarakani lakini hakuna miiko ya kuwabana
Nimependa maon yako but resource inatakiwa viwe propotional na maendeleo
 
Tuna kazi kubwa ya kufufua uchumi wetu, ikiwemo kujenga viwanda na kuimarisha miundombinu kazi ambayo jemedari wetu anaiongoza vema.

Kuna ubaya gani kama tutampa kiongozi muda hadi maono yake ya msingi ambayo ameyatanabahisha mara kwa mara yakamilike.

Najua kuna ukomo wa kikatiba, lakini katiba si msahafu na inaweza kufanyiwa marekebisho wakati wowote kulingana na mahitaji ya wakati.

Kazi aliyoianza Rais wetu inahitaji zaidi ya miaka 10 kuweza kukamilika na kwahiyo sisi kama wananchi tunapaswa kumuunga mkono ktk kila hatua.

Nichukue fursa hii kuwapongeza wanachama wa vyama pinzani waliojitoa kimasomaso kumuunga mkono Rais Magufuli, nikianza na madiwani wa Arusha, wanachadema wa Misungwi na Ukerewe na bila ya kuwasahau wabunge wa Ukawa walio ktk ziara ya waziri mkuu.

Tanzania kwanza vyama baadae, ahsante!
 
Huyu Ngosha kuna watu wako radhi wamuachie wake zao awazalishe...

Na kama wake zao watagoma, wako radhi wajitoe wao wenyewe...

Ngosha mwenyewe katulia anachapa kazi, vimjamaa vinamshobokea tu wakati ye mwenyewe alishawaambia hajaribiwi wala hapangiwi...
 
Back
Top Bottom