Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,194
- 4,116
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo ametoa onyo kwa wauzaji wa mishikaki na vyakula barabarani akiwataka kuacha kufanya biashara hizo katika maeneo hayo na kuhimiza serikali haitarudi nyuma kuchukua hatua dhidi ya watakao kiuka utaratibu.
Amesema kuwa jiji linatumia gharama kubwa kuwalipa mgambo wanaotekeleza zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara hasa wanaochoma mishikaki ambao wanazidi kuongezeka maeneo ya mjini hivyo ni vyema wakatii sheria bila shuruti kwa kuondoka maeneo ambayo siyo rasmi.
Awali wafanyabiashara hao walieleza kuwa wanapitia manyanyaso kwa kukamatwa na mgambo wanaotekeleza zoezi la kuwaondoa kwenye maeneo hayo huku mali zao zikiharibika na hata kupigwa faini ya hadi laki tatu pale wanapokamatwa