Ikulu Yetu Na Mpangaji Wake.........

CAMARADERIE

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
4,419
1,920
Msanii wa Kizazi Kipya hapa nchini ,maarufu kama Bongo Flavour, Bi Rehema Chalamila anaejulikana zaidi kama Ray C, jana mchana amefika Ikulu ya Dar-Es-Salaam kumshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa msaada mkubwa wa matibabu yake ambayo yanafanyika jijini Dar-Es-Salaam chini ya uangalizi maalum.

.

RAY%2BC%2Bakimishukur%2BRais%2BKikwete.JPG
 
Rais wa watu huyo!! Halafu yeye ndiye anaonekana kufurahi zaidi utadhani ndiye anayesaidiwa na huyo RC wake! (oooh sorry, Ray C).
 
Ningekuwa JK ningemwambia Ray C awataje waliomuuzia madawa ili wakamatwe na washitakiwe na sio kutabasamu tu........hivi mateja wengine vipi? Hawana msaada wa ikulu? Manake wako pale ferry hardly 100 metres from his own bedstead!
 
Mla unga? Teja? Ikulu?badala ya jela?nchi hii bwana!!fisadi ni muungwana!mwizi ni shujaa!mwasherati ni kiongozi mahiri!TEJA ni mgeni mashuhuri wa ikulu!!!ikulu hakunaga kazi za kufanya?sababu kama mkulu asingepata ugeni huo mkubwa ungeskia yuko zake kulee anakopendaga kwenda.
 
Umanitangulia ndg yangu, yaani Tanzania inazidi kuongeza kumbux2
 
Yaani toka Jk ameingia hapo ikulu wageni wa hapo wengi kama si wote ni watu ambao kiungwana kabisa tunaweza kusema ni wa hovyohovyo!! Kama mafisadi waliothibitika,wezi wa mali za umma,wazinzi maarufu,watu wanaotetea ushoga,mateja,mabongo fever&muvi,wauza pembe za ndovu na washirikina kina yahya(RIH).
 
Nataka kujua Ray C kapata matibabu wapi?? Maana hiyo ni quick recover kama vipe tupeleke masela wa huku kitaa maana hali n mbaya sana.
Rais msaada huku kwetu kila mzazi analia .
 
kurugenzi ya wasioelewana Ikulu!!!
Wapo busy wanauza sura ya Jh kaya.....mara amepiga picha na kilema, mara amepiga picha na wabwia unga...
ilimradi tu atoke kwenye front page..!!!
 
Ray c hakupiga show kweli hapo.. Yaani hata chorus! Haiwezekani!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Habari ndio hiyo, nilimuona juzi nikatamani kulia.

Nilikuwa convinced kabisa kuwa kaacha...alibadili marafiki almost wote waliokuwa wanrisk yeye kurudia madawa, akaanzisha foundation kusupport waathirika wengine waachane na madawa, he was clean kwa muda wa kutosha tu. Sijui nini kimetokea! Nina wasiwasi Ray C naye kueleka uko, amekuwa detached maisha halisi kwa muda mrefu, si ahisi kucope haraka haraka hivyo..
 
Msanii wa Kizazi Kipya hapa nchini ,maarufu kama Bongo Flavour, Bi Rehema Chalamila anaejulikana zaidi kama Ray C, jana mchana amefika Ikulu ya Dar-Es-Salaam kumshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa msaada mkubwa wa matibabu yake ambayo yanafanyika jijini Dar-Es-Salaam chini ya uangalizi maalum.

.

RAY%2BC%2Bakimishukur%2BRais%2BKikwete.JPG

Badala ya kuwa na mipango ya kitaifa ya kusaidia wananchi na matatizo yao kwa ujumla, jamaa anasaidia mmoja mmoja kwa vigezo visivyoeleweka kitu ambacho sio sifa ya Rais wa nchi kama Tanzania. Sasa na wengine waje hapo Ikulu kuomba msaada? Hivi kama ni pesa ya mlipa kodi CAG ataiona kwenye vitabu vya serikali?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom