Ikulu na Hoja Nyepesi

Kichankuli

JF-Expert Member
Dec 18, 2008
887
189
Gazeti la Mwananchi leo limechapisha kile kilichoitwa majibu ya Ikulu kwa Maaskofu. Sehemu ya taarifa ya ikulu iliyonukuliwa na gazeti hilo inasomeka hivi:

"Mtu akikuonya kuwa nyumbani kwako kumeonekana nyoka, huanzi kwa kuuliza kama ni kweli, ni wa rangi gani? Unatakiwa kushtuka na kujiandaa kumsaka kwa nia ya kumwondosha nyumbani kwako, hata ikibidi umuue ili asije akaleta madhara makubwa kwako na kwa familia yako," imeeleza sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza.................................."

kwa habari kamili bofya kwenye kiunganishi hapa chini


Ikulu yawajibu maaskofu CCT

Binafsi naona kwamba maelezo yaliyotolewa na Ikulu ni mepesi sana. Hivi ukisoma huo mfano wa nyoka unaweza kweli kusema unalingana na kauli ya kusema kwamba Viongozi wa dini wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya? Nijuavyo mimi nyoka akionekana sehemu hukimbia na kujificha na siyo rahisi kumtofautisha nyoka mmoja na mwingine (wa aina moja). Lakini viongozi wa dini wanajulikana kwa majina na mpaka ifike Rais wa nchi anatamka jambo inamaana tayari jambo hilo limefanyiwa kazi na kuthibitika kuwa ni la ukweli. Ikulu ni sehemu nzito ambayo kwa mtizamo wangu haiwajibiki kuongelea tuhuma, hiyo ni kazi ya DPP na vijana wake. Sasa leo Rais wa nchi ametamka jambo halafu mwemaji wake anatwambia wanaojishuku wajisalimishe, au anawaambia Viongozi wa Dini waanze kujichunguza wenyewe (kumsaka nyoka) ili kubaini nani miongoni mwao anahusika na tuhuma hizo.

Ifike wakati wahusika wa Ikulu waelewe kwamba Ikulu ni Ofisi kubwa ambayo haipaswi kuwa inatoa maelezo ya vitu ambavyo havina uhakika au vitu vyenye uzito mdogo
 
:majani7:Eti wewe mkuu ulitegemea wajibu nini? Hata hapo wamejitahidi sana make kwa kawaida huwa wanatukana!

Anakuja mtu, mnafanya uamzi , anawekeza; mnaendelea! (Hotuba ya rais wenu JK jana.)
 
Hiyo ikulu ya miaka hii ni aibu tupu; ikulu enzi za nyerere na mwinyi bana sasa hivi wote wababaishaji
 
Back
Top Bottom